Kutoka kwa Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ahadi ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu. Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Ninakutakia neema, rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

Paulo Amtia Moyo Timotheo

Ninamshukuru Mungu ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyomtumikia baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika sala zangu. Nikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nijazwe furaha. Nakumbushwa kuhusu imani yako ya kweli, imani ambayo walikuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo nina hakika, unayo. Kwa sababu hii nakukum busha ukichochee kile kipawa ulichopewa na Mungu wakati nilipo kuwekea mikono. Maana Mungu hakutupatia roho ya woga bali roho ya nguvu, ujasiri na kiasi.

Basi usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake, bali uishiriki taabu kwa ajili ya Habari Njema kwa kadiri ya nguvu upewayo na Mungu. Yeye ametuokoa na kutuita tupokee maisha ya utakatifu; si kwa sababu ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya makusudio yake na neema yake. Tulipewa neema hii katika Kristo Yesu tangu milele 10 na sasa imedhihirishwa kwa kuja kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu ambaye ameondoa kifo kabisa na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili. 11 Nami nimechaguliwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii. 12 Ndio sababu ninateseka hivi. Lakini sioni aibu kwa maana ninamjua huyo niliyemwamini na nina hakika ya kuwa anaweza kutunza kile nilichomkabidhi, mpaka siku ile.

13 Tumia kama kielelezo cha mafundisho sahihi maneno ya kweli ambayo umeyasikia kutoka kwangu pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu. 14 Linda ile kweli ambayo umekabidhiwa na Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu. 15 Bila shaka unafahamu kuwa watu wote katika jimbo la Asia wameniacha, wakiwemo Filego na Hermogene. 16 Bwana aonyeshe huruma yake kwa jamaa ya Onesiforo kwa sababu alinitia moyo mara nyingi na hakuonea aibu minyororo yangu. 17 Bali alipofika Roma alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata. 18 Bwana amwezeshe kupata rehema kutoka kwa Bwana siku ile. Unafahamu pia jinsi alivyoni saidia huko Efeso.