Yesu Afufuka Kutoka Kwa Wafu

16 Sabato ilipomalizika, Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake Yakobo na Salome walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu. Asubuhi na mapema, siku ya Jumapili, walikwenda kaburini jua likiwa linaanza kuchomoza. Njiani wakawa wanaulizana, “Ni nani atatuondolea lile jiwe kwenye mlango wa kaburi?” Lakini walipotazama, wakaona jiwe lile, ambalo lilikuwa kubwa sana, limekwisha ondolewa.

Walipoingia kaburini, walimwona kijana amekaa upande wa kulia akiwa amevaa vazi jeupe. Wakashtuka. Yule mtu akawaambia, “Msishtuke. Mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulubiwa. Amefufuka! Hayuko hapa! Tazameni mahali alipokuwa amelazwa.

Lakini nendeni mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, kwamba anatangulia kwenda Galilaya na huko mtamwona, kama alivyowaam bia.” Wale wanawake wakiwa wanashangaa na kutetemeka kwa hofu, wakatoka pale kaburini mbio! Hawakumweleza mtu ye yote jambo lo lote kwa maana walikuwa wanaogopa.

Yesu Anamtokea Mariamu Magdalena

Baada ya Yesu kufufuka, alimtokea kwanza Mariamu Mag dalena, yule aliyemtoa pepo saba. 10 Mariamu akaenda akawaambia wale waliokuwa wakifuatana na Yesu. Wakati huo walikuwa bado wanalia na kuomboleza. 11 Lakini waliposikia kwamba Yesu yu hai na kwamba Mariamu alikuwa amemwona, hawakuamini.

Yesu Awatokea Wanafunzi Wawili

12 Baadaye Yesu aliwatokea kwa namna nyingine wanafunzi wawili walipokuwa wakienda shamba. 13 Nao pia walirudi wakawaam bia wenzao. Lakini pia hawakuamini.

Yesu Anawatokea Wale Wanafunzi Kumi Na Mmoja

14 Mwishowe, Yesu aliwatokea wale wanafunzi kumi na mmoja, wakiwa wanakula chakula. Akawakemea kwa kutokuamini kwao na kwa ugumu wa mioyo yao uliowafanya wakatae kuwasadiki wale waliomwona baada ya kufufuka.

15 Akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote, mkawahubirie watu wote Habari Njema. 16 Ye yote atakayeamini na kubatizwa ataoko lewa. Lakini ye yote ambaye atakataa kuamini, atahukumiwa.

17 “Na hizi ndizo ishara zitakazoandamana na wale wata kaoamini: Kwa kutumia jina langu watafukuza pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 wataweza hata kuwakamata nyoka na kunywa sumu lakini wasidhurike; watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.”

Yesu Apaa Kwenda Mbinguni

19 Yesu alipokwisha kuwaambia maneno haya, alichukuliwa juu mbinguni, akaketi upande wa kulia wa Mungu.