Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni

18 Wakati huo, wanafunzi walimjia Yesu wakamwuliza, “Ni nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa mbinguni?” Yesu akam wita mtoto mdogo akamsimamisha mbele yao. Kisha akasema, “Nawa hakikishieni kwamba msipobadilika na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni. Kwa hiyo mtu ye yote anayejinyenyekeza akawa kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa mbinguni.

“Na ye yote anayemkaribisha mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, ananikaribisha mimi. Lakini kama mtu ye yote anamsabab isha mmojawapo wa hawa wadogo wanaoniamini atende dhambi, ingali kuwa nafuu kwake afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake akazam ishwe katika kilindi cha bahari. Ole kwa ulimwengu, kwa sababu ya mambo yanayosababisha watu kutenda dhambi! Mambo hayo lazima yawepo, lakini ole wake mtu yule ambaye huyaleta. Ikiwa mkono wako au mguu wako unakusababisha utende dhambi, ukate, uutupilie mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja au mguu mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na miguu miwili lakini ukatupwa katika moto wa milele. Na kama jicho lako lina kusababisha utende dhambi ling’oe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa katika moto wa Jehena.

10 “Angalia usimdharau mmojawapo wa hawa wadogo, kwa maana nawaambieni, malaika wao mbinguni wanaonana daima na Baba yangu aliye mbinguni.” [ 11 Maana mimi Mwana wa Adamu nilikuja kuokoa kilichopotea.]

Mfano Wa Kondoo Aliyepotea

12 “Mnaonaje? Kama mtu ana kondoo mia moja na mmoja wao akapotea, hatawaacha wale tisini na tisa mlimani aende kumtafuta yule aliyepotea? 13 Na akisha mpata, nawaambia kweli, anafurahi zaidi kwa ajili ya huyo kondoo mmoja kuliko kwa wale tisini na tisa ambao hawakupotea. 14 Hali kadhalika, Baba yenu wa mbin guni hapendi hata mmojawapo wa hawa wadogo apotee.”

Ndugu Yako Akikukosea

15 “Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwambie kosa lake mkiwa ninyi wawili peke yenu. Akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. 16 Kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili kusudi wawepo mashahidi wawili au watatu wa kuthi bitisha jambo hilo. 17 Akikataa kuwasikiliza, liambie kanisa. Kama akikataa kulisikiliza kanisa, basi mhesabu yeye kama ni mpa gani au mtoza ushuru.

18 “Nawaambieni kweli, lo lote mtakalokataza duniani lita kuwa limekatazwa mbinguni. Na lo lote mtakaloruhusu duniani litaruhusiwa mbinguni.

19 “Tena ninawaambia, ikiwa wawili kati yenu mtakubaliana hapa duniani kuhusu jambo lo lote mnaloomba, Baba yangu wa mbin guni atawatimizia. 20 Kwa maana wanapokutana watu wawili au watatu katika jina langu, hapo mimi nipo pamoja nao.”

Hakuna Mwisho Wa Kusamehe

21 Kisha Petro akaja kwa Yesu akamwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami niendelee kumsamehe? Hata mara saba?” 22 Yesu akamjibu, “Sikuambii mara saba, bali saba mara sabini.”

Mfano Wa Mdaiwa Asiyesamehe

23 “Kwa hiyo Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kukamilisha hesabu zake za fedha na watumishi wake. 24 Alipoanza kukagua hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa na deni la mamilioni ya shilingi, aliletwa kwake. 25 Na kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake aliamuru kwamba auzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vyote alivyo navyo, ili zipatikane fedha za kulipa deni lake.

26 “Yule mtumishi akapiga magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nitakulipa deni lako lote.’ 27 Yule bwana akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwachilia.

28 “Lakini yule mtumishi alipotoka, alikutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha shilingi chache. Akamkamata, akam kaba koo akimwambia, ‘Nilipe deni langu!’

29 “Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nitakulipa deni lako lote.’ 30 Lakini akaka taa. Badala yake akampeleka afungwe gerezani mpaka aweze kulipa hilo deni.

31 “Watumishi wenzake walipoona mambo haya, walisikitika sana. Wakamwendea bwana wao wakamweleza yote yaliyotokea.

32 “Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu, uliponisihi, nilikusamehe deni lako lote. 33 Je, hukupaswa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhuru mia?’ 34 Kwa hasira yule bwana akamkabidhi yule mtumishi kwa askari wa gereza mpaka atakapomaliza kulipa deni lote.

35 “Na hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ambaye hatamsamehe ndugu yake kwa moyo.”