Kutoka kwa Petro, mtume wa Yesu Kristo. Kwa wateule wa Mungu ambao wametawanyika, wanaoishi ugenini huko Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia. Ninyi mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba na kutakaswa na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kunyunyiziwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele.

Tumaini Lenye Uzima

Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema yake kuu ametufanya tuzaliwe upya ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo kutoka kwa wafu; na tupokee urithi usioharibika, usiooza na usiochuja, ambao umewekwa mbinguni kwa ajili yenu. Nanyi, kwa imani, mnalindwa na nguvu ya Mungu mpaka utakapofika wokovu ambao uko tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.

Furahini sana katika hilo, ingawa sasa kwa kitambo kidogo ni lazima mpate majaribu ya kila aina. Majaribu yataifanya imani yenu, ambayo ina thamani kuliko dhahabu, iwe imepimwa na kuthibitishwa kuwa ya kweli kama vile dhahabu ambayo ingawa ni kitu kiharibikacho, hupimwa kwa moto. Ndipo mtapata sifa, utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa. Ingawa hamja pata kumwona, mnampenda. Na ingawa hamumwoni sasa mnamwamini na kujawa na furaha tukufu isiyoelezeka. Maana mnapokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.

10 Manabii waliotabiri kuhusu neema hiyo ambayo ninyi mnge pewa, walitafuta sana na kwa makini habari za wokovu huu. 11 Walijaribu kutafuta kujua ni nani au ni wakati upi uliomaan ishwa na Roho wa Kristo aliyekuwa akisema ndani yao alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu utakaofuata. 12 Walidhihir ishiwa kuwa kazi waliyokuwa wakifanya si kwa faida yao bali ni kwa ajili yenu. Kwa maana walinena nanyi habari za mambo ambayo sasa mmekwisha elezwa na wale waliowahubiria Injili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Hata malaika wanata mani kufahamu mambo haya.

Mwito Wa Kuishi Maisha Matakatifu

13 Kwa hiyo, ziandaeni nia zenu, muwe na kiasi, wekeni tumaini lenu lote katika neema ile mtakayopewa wakati ule Yesu Kristo atakapodhihirishwa. 14 Kama watoto watiifu, msikubali kutawaliwa na tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mkiishi katika ujinga. 15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, kadhalika ninyi muwe watakatifu katika mwenendo wenu; 16 maana imeandikwa: “Muwe watakatifu kwa sababu mimi ni mtakatifu.”

17 Kwa kuwa mnamwita “Baba” yeye ahukumuye matendo ya kila mtu pasipo upendeleo, ishini maisha yenu hapa duniani kama wageni, kwa kumcha Mungu. 18 Maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutokana na maisha duni yasiyofaa ambayo mlirithi kutoka kwa baba zenu. Hamkukombolewa kwa kutumia vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu, 19 bali mlikombolewa kwa damu ya thamani ya Kristo, Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa. 20 Yeye alichaguliwa kabla ya dunia kuumbwa lakini akadhihirishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili yenu. 21 Kwa ajili yake ninyi mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu akampa utukufu, na kwa hiyo imani yenu na matumaini yenu yako kwa Mungu.

22 Na sasa kwa kuwa mmekwisha kujitakasa kwa kuitii ile kweli na kuwapenda ndugu zenu kwa kweli, pendaneni kwa moyo wote. 23 Maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa mbegu isiyoharibika, kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu hata milele. 24 Maana, “Binadamu wote ni kama nyasi na utukufu wao ni kama ua la mwituni. Nyasi hunyauka na ua huanguka, 25 lakini neno la Mungu hudumu milele.” Na neno hilo ni Habari Njema ambayo mlihubiriwa.

Kutoka kwa Petro, mtume wa Yesu Kristo.

Kwa wateule wa Mungu, ambao huonekana kama ni wageni kutoka nchi nyingine, waliotawanyika katika majimbo yote ya Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia, na Bithinia. Kwa kadri ya mpango wa Mungu Baba alioufanya muda mrefu uliopita, mliteuliwa muwe wake kwa kufanywa watakatifu na Roho Mtakatifu. Mliteuliwa kuwa waatiifu kwa Mungu na kutakaswa na kujumuishwa miongoni mwa watu wa Agano Jipya kwa kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo.[a]

Neema na amani ya Mungu viwe pamoja nanyi kwa wingi.

Tumaini Lililo Hai

Atukuzwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Katika rehema zake kuu, Mungu alitufanya sisi tuzaliwe upya ili tuwe na tumaini lililo hai, kwa njia ya ufufuo wa Yesu Kristo kutoka kwa waliokufa, na ili kuwa na urithi usioharibika, ulio safi na usiofifia, uliotunzwa kwa ajili yenu kule mbinguni.

Ni kwa ajili yenu ninyi ambao kwa njia ya imani, mnalindwa na nguvu za Mungu ili mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. Hili linawafanya mfurahi sana, hata kama kwa sasa imewalazimu mhuzunishwe kwa kipindi kifupi kwa masumbufu na mateso ya aina mbali mbali. Kwa masumbufu haya imani yenu inajaribiwa na kuithibitishwa kuwa ni ya kweli. Hii inafananishwa na dhahabu pale inapopitishwa kwenye moto kuthibitisha uhalisi wake. Lakini hata dhahabu ya kweli inaweza kuharibiwa. Hivyo imani ina thamani zaidi kuliko dhahabu. Pale imani yenu inapothibitika kuwa ni ya kweli, matokeo yake ni sifa, utukufu na heshima kwa Mungu wakati wa kurudi kwake Yesu Kristo.

Hata kama hamjamwona Yesu, lakini mnampenda. Hata kama hamuwezi kumuona kwa sasa, lakini mnamwamini yeye na mmejazwa na furaha ya ajabu isiyoweza kuelezwa kwa maneno. Mnaupokea wokovu wenu ambao ni lengo la imani yenu.

10 Manabii waliotabiri juu ya neema ambayo ingeoneshwa kwenu, walipeleleza kwa makini na kwa uangalifu wakaulizia habari za wokovu huu. 11 Roho wa Kristo alikuwa ndani yao, naye aliwapa ushuhuda mapema kuhusu Kristo kwamba itamlazimu kuteswa na baada ya hapo atapokea utukufu. Manabii waliuliza kutaka kujua wakati gani na katika mazingira gani mambo haya yangetokea.

12 Ilifunuliwa kwao kwamba walikuwa hawajitumikii wenyewe. Badala yake, waliwatumikia ninyi walipotabiri juu ya mambo haya. Na sasa mmesikia juu ya mambo haya kutoka kwa wale waliyowaambia habari Njema kwa msaada wa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Hata malaika wangetamani sana kufahamu zaidi juu ya mambo haya mliyoambiwa.

Mwito Kwa Maisha Matakatifu

13 Hivyo mkeshe katika fahamu zenu na kuwa na kiasi. Yawekeni kikamilifu matumaini yenu katika baraka mtakazopewa wakati Yesu Kristo atakapofunuliwa. 14 Kama watoto watiifu, msiyaache maisha yenu yandelee kutawaliwa na tamaa mbaya mlizokuwa nazo awali mlipokuwa wajinga. 15 Badala yake, kama ambavyo yeye Mungu aliyewaita alivyo mtakatifu, hata ninyi muwe watakatifu katika kila mnalotenda. 16 Hivyo Maandiko yanasema: “Iweni watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu.”(A)

17 Na kama Baba mnayemwita Mungu anayewahukumu watu bila upendeleo kwa kadri ya matendo ya kila mtu, muishi maisha ya utauwa na hofu kwa Mungu katika miaka yenu ya kukaa humu duniani kama wageni. 18 Mnajua kwamba siyo kwa mambo yaharibikayo kama fedha au dhahabu, kwamba mliokolewa kutoka katika maisha yasiyofaa mliyoyapokea kutoka kwa babu zenu, 19 bali kwa damu ya thamani ya Kristo, kama ile ya mwanakondoo asiye na dosari wala ila. 20 Kristo alichaguliwa kabla ya uumbaji wa ulimwengu, lakini alidhihirishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili yenu. 21 Kupitia Kristo mmekuwa waamini katika Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na kumpatia utukufu. Ili imani yenu na matumaini yawekwe katika Mungu.

22 Sasa kwa vile mmejitakasa wenyewe kwa kuitii kweli hadi mwisho kwamba mtaonesha upendo wa kweli wa kindugu, jitahidini kupendana ninyi kwa ninyi kwa mioyo iliyo safi. 23 Mmezaliwa upya sio kama matokeo ya mbegu inayoharibika, lakini kama matokeo ya mbegu isiyoharibika. Mmezaliwa upya kwa njia ya ujumbe wa Mungu, ambao unaleta uzima ndani yenu. 24 Hivyo, kama Maandiko yanavyosema:

“Watu wote ni kama manyasi,
    na utukufu wao wote ni kama maua pori katika manyasi.
Manyasi yananyauka na kukauka,
    na maua yanapukutika,
25     bali ujumbe wa Bwana unadumu milele.”(B)

Na ujumbe huo ni habari njema iliyohubiriwa kwenu.

Footnotes

  1. 1:2 kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo Katika Kut 24:7-8 Musa aliwanyunyizia damu watu wa Israeli ili kukamilisha agano lao pamoja na Mungu, baada ya kuahidi kutii amri zake zote, Damu ya Yesu inakamilisha Agano Jipya kati ya Mungu na watu wake.