Basi, acheni kabisa uovu wote, hila yote, unafiki, wivu na masingizio yote. Kama watoto wachanga, mtamani maziwa safi ya kiroho, ili kwa hayo mpate kukua katika wokovu wenu, kwa maana mmekwisha kuonja fadhili za Bwana.

Jiwe Hai Na Taifa Takatifu

Basi, njooni kwake yeye aliye Jiwe lililo hai, ambalo lili kataliwa na watu bali kwa Mungu ni teule na la thamani kubwa. Ninyi pia, kama mawe hai mjengwe kuwa nyumba ya kiroho, mpate kuwa makuhani watakatifu, mkitoa sadaka za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa maana imeandikwa katika Maandiko: “Tazama, ninaweka jiwe kuu la msingi huko Sayuni; jiwe la pembeni teule na la thamani kubwa, na kila amwaminiye hataaibika.” Kwenu ninyi mnaoamini, yeye ni wa thamani kubwa. Lakini kwao wasioamini, “Lile jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi,” na, “Jiwe ambalo litawafanya watu wajik wae; mwamba ambao utawafanya waanguke.” Wanajikwaa kwa sababu hawatii lile neno, kama walivyopangiwa tangu mwanzo.

Lakini ninyi ni uzao mteule, ukuhani mtukufu, taifa taka tifu, watu pekee wa Mungu mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya aliyewaita kutoka gizani na kuwaingiza katika nuru yake ya ajabu. 10 Hapo mwanzo ninyi mlikuwa si taifa, lakini sasa ninyi ni watu wa Mungu. Hapo mwanzo mlikuwa hamjapata rehema, lakini sasa mme pata rehema.

11 Rafiki wapendwa, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapi taji njia hapa duniani, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupi gana vita na roho zenu. 12 Muwe na mwenendo mwema kati ya watu wasiomjua Mungu, ili kama watawasema kuwa wakosaji, wayaone matendo yenu mema na wamtukuze Mungu siku ile atakapotujia.

Kuwatii Wenye Mamlaka

13 Jinyenyekezeni kwa ajili ya Bwana chini ya mamlaka yote ya wanadamu: ikiwa ni mfalme ambaye ana mamlaka ya mwisho; 14 au ikiwa ni wakuu wengine ambao amewateua kuwaadhibu wahalifu na kuwasifu watendao mema. 15 Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema myazime maneno ya kijinga ya watu wapumbavu. 16 Ishini kama watu huru lakini msitumie uhuru wenu kama kisin gizio cha kutenda uovu; bali muishi kama watumishi wa Mungu. 17 Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu waamini. Mcheni Mungu. Mheshimuni mfalme. 18 Ninyi watumwa, watiini mabwana wenu kwa heshima yote, si wale mabwana walio wapole na wema peke yao, bali hata wale walio wakali. 19 Maana ni jambo jema kwa mtu kuvumilia taabu za maonevu kwa kukumbuka kuwa Mungu yupo. 20 Maana ni sifa gani kwa mtu kustahimili kupigwa kwa kuwa ametenda uovu? Lakini kama mkis tahimili mateso kwa kutenda wema, mnapata kibali mbele za Mungu. 21 Ninyi mmeitwa kwa ajili hiyo, kwa sababu Kristo naye aliteseka kwa ajili yenu akawaachia kielelezo, mzifuate nyayo zake. 22 Yeye hakutenda dhambi wala neno la udanganyifu haliku pita kinywani mwake. 23 Walipomtukana, yeye hakuwarudishia matu kano; alipoteswa, hakuwatishia, bali alimtegemea Mungu ahukumuye kwa haki. 24 Yeye mwenyewe alizibeba juu mtini dhambi zetu mwil ini mwake, ili tuwe wafu kwa mambo ya dhambi na tupate kuishi katika haki. Kwa majeraha yake, ninyi mmeponywa.

25 Kwa maana mlikuwa mmepotea kama kondoo, lakini sasa mmer udi kwa Mchungaji na Mlinzi wa roho zenu.

Jiwe Lililo Hai na Taifa Takatifu

Hivyo acheni uovu wote, pamoja na uongo, hali za unafiki na wivu na aina zote za kashfa. Kama watoto wachanga, mnapaswa kuyatamani maziwa ya kiroho yaliyo safi, ili kwa ajili ya hayo muweze kukua na kuokolewa, kwa vile mmekwisha kuujaribu wema wa Bwana.

Mkaribieni Bwana Yesu, aliye Jiwe lililo Hai, lililokataliwa na watu, bali kwa Mungu ni jiwe lililoteuliwa na kuheshimika. Ninyi pia, kama mawe yaliyo hai mnajengwa ili kuwa hekalu la kiroho. Mmekuwa makuhani watakatifu mkimtumikia Mungu kwa kutoa sadaka za kiroho zinazokubalika kwake kwa njia ya Yesu Kristo. Hivyo, Maandiko yanasema,

“Tazameni, naweka katika Sayuni Jiwe la msingi katika jengo,
    lililoteuliwa na kuheshimika,
na yeyote anayeamini hataaibishwa.”(A)

Inamaanisha heshima kwenu mnaoamini, bali kwa wasioamini,

“jiwe walilolikataa wajenzi
    limekuwa jiwe la muhimu kuliko yote.”(B)

Na,

“jiwe linalowafanya watu wajikwae
    na mwamba unaowafanya watu waanguke.”(C)

Walijikwaa kwa sababu hawakuutii ujumbe wa Mungu, na Mungu alisema hilo litatokea wasipotii.

Lakini ninyi ni watu mlioteuliwa, ni Ukuhani unaomtumikia Mfalme. Ninyi ni taifa takatifu nanyi ni watu wa Mungu. Yeye aliwaita Ili muweze kutangaza matendo yake yenye nguvu. Naye aliwaita mtoke gizani na mwingie katika nuru yake ya ajabu.

10 Kuna wakati hamkuwa watu,
    lakini sasa mmekuwa watu wa Mungu.
Kuna wakati hamkuoneshwa rehema,
    lakini sasa mmeoneshwa rehema za Mungu.

Mwishie Mungu

11 Rafiki zangu, ninawasihi kama wapitaji na wageni katika ulimwengu huu kuwa mbali na tamaa za kimwili, ambazo hupingana na roho zenu. 12 Muwe na uhakika wa kuwa na mwenendo mzuri mbele ya wapagani, ili hata kama wakiwalaumu kama wakosaji, watayaona matendo yenu mazuri nao wanaweza kumpa Mungu utukufu katika Siku ya kuja kwake.

Tii Mamlaka Yote ya Kibinadamu

13 Nyenyekeeni kwa mamlaka yo yote ya kibinadamu kwa ajili ya Bwana. Mnyenyekeeni mfalme, aliye mamlaka ya juu kabisa. 14 Na muwatii viongozi waliotumwa na mfalme. Wametumwa ili kuwaadhibu wale wanaokosa, na kuwapongeza wale wanaofanya mazuri. 15 Kwa kuwa mapenzi ya Mungu ni kwamba, kwa kutenda mema mtayanyamazisha mazungumzo ya kijinga ya watu wasio na akili. 16 Muishi kama watu walio huru, lakini msiutumie uhuru huo kama udhuru wa kufanya maovu. Bali muishi kama watumishi wa Mungu. 17 Onesheni heshima kwa watu wote: Wapendeni ndugu zenu na dada zenu waliomo nyumbani mwake Mungu. Mcheni Mungu na mumheshimu mfalme.

Mfano wa Mateso ya Kristo

18 Watumwa mlio nyumbani, watumikieni mabwana wenu kwa heshima yote,[a] siyo tu wale walio wapole na wenye busara, bali hata wale walio wakali. 19 Baadhi yenu mtapata mateso wakati ambapo hamjafanya kosa lolote. Ikiwa utaweza kuvumilia maumivu na kuweka fikra zako kwa Mungu, hilo linampendeza sana Mungu. 20 Kwani kuna sifa gani iliyopo kwako kama utapigwa kwa kutenda mabaya na kuvumilia? Lakini kama utateseka kwa kutenda mema na kustahimili, hili lampendeza Mungu. 21 Ni kwa kusudi hili mliitwa na Mungu, kwa sababu Kristo pia aliteseka kwa ajili yenu na kwa kufanya hivyo aliacha kielelezo kwenu, ili tuweze kuzifuata nyayo zake.

22 “Hakutenda dhambi yo yote,
    wala hakukuwa na udanganyifu uliopatikana kinywani mwake.”(D)

23 Alipotukanwa hakurudishia matusi. Alipoteseka, hakuwatishia, bali wakati wote alijitoa mwenyewe kwa Mungu ahukumuye kwa haki. 24 Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu kwenye mwili wake hadi pale msalabani, ili tuweze kuacha kuishi kwa ajili ya dhambi na kuishi kwa ajili ya haki. Ilikuwa ni kwa njia ya majeraha yake kwamba mliponywa. 25 Kwani mlikuwa kama kondoo wanaotangatanga huko na huko, lakini sasa mmerudi kwa Mchungaji na Mwangalizi wa maisha yenu.

Footnotes

  1. 2:18 kwa heshima yote Au “kwa heshima na taadhima kwa Mungu”.