Maagizo Kwa Wazee Na Vijana

Ninawasihi wazee waliomo miongoni mwenu, nikiwa mzee mwenzenu na shahidi wa mateso ya Kristo na mshiriki katika utu kufu utakaofunuliwa. Lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, si kwa tamaa ya fedha bali kwa moyo wenu wote. Msijifanye mabwana wakubwa kwa wale mnaowa chunga bali muwe vielelezo kwa kundi hilo. Naye Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa mtapokea taji ya utukufu isiyofifia.

Kadhalika ninyi vijana watiini wazee. Jivikeni unyenyekevu, mnyenyekeane kwa maana, “Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu.” Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu wenye nguvu, ili wakati wake ufaao utakapotimia, awainue.

Mwekeeni yeye fadhaa zenu zote kwa maana yeye hujishughul isha sana na mambo yenu.

Kaeni macho. Kesheni, maana adui yenu Ibilisi, huzunguka- zunguka akinguruma kama simba, akitafuta mtu atakayemmeza. Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkifahamu kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayo hayo. 10 Na mkisha kuteseka kitambo kidogo, Mungu wa neema yote ambaye amewaita katika utukufu wake wa milele katika Kristo, yeye mwenyewe atawa kamilisheni na kuwathibitisha na kuwatia nguvu. 11 Uweza ni wake milele na milele. Amina.

Salamu

12 Nimewaandikia kwa kifupi kwa msaada wa Silvano, ndugu ambaye namtambua kuwa mwaminifu, nikiwaonya na kuwashuhudia kuwa hii ndio neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo. 13 Mwenzenu mteule hapa Babiloni anawasalimu pamoja na mwanangu Marko .

Kondoo wa Mungu

Sasa nina jambo la kuwaambia wazee walio katika kundi lenu. Mimi pia ni mzee nami mwenyewe nimeyaona mateso ya Kristo. Na nitashiriki katika utukufu utakaodhihirishwa kwetu. Hivyo ninawasihi, mlitunze kundi la watu mnalowajibika kwalo. Ni kundi lake Mungu.[a] Basi lichungeni kwa moyo wa kupenda na si kwa kulazimishwa. Hivi ndivyo Mungu anavyotaka. Fanyeni hivyo kwa sababu mnafurahi kutumika, na si kwa sababu mnataka pesa. Msiwaongoze wale mnaowasimamia kwa kuwaamrisha. Lakini muwe mfano mzuri wa kuiga kwao. Ili Kristo aliye Mchungaji Mkuu atakapokuja, mpate taji yenye utukufu na isiyopoteza uzuri wake.

Vijana, nina jambo la kuwaambia ninyi pia. Mnapaswa kutii mamlaka ya wazee. Na ninyi nyote mnapaswa kuwa wanyenyekevu ninyi kwa ninyi.

“Mungu yu kinyume na wanaojivuna,
    lakini ni mwema kwa wanyenyekevu.”(A)

Hivyo mjinyenyekeze chini ya mkono wa Mungu wenye nguvu. Kisha, wakati sahihi utakapofika, atawalipa kwa kuwainua. Mpeni Mungu masumbufu yenu yote, kwa sababu Yeye anawajali.

Iweni na kiasi na muwe waangalifu! Shetani ni adui yenu naye huzunguka zunguka kama simba anayeunguruma akimtafuta yeyote wa kumshambulia na kumla. Mpingeni ibilisi. Kisha msimame imara katika imani yenu. Mnafahamu kwamba ndugu zenu ulimwenguni kote wanapitia mateso sawa na hayo mliyonayo.

10 Ndiyo, mtateseka kwa muda mfupi. Lakini baada ya hapo, Mungu ataweka kila kitu sawa. Atawatia nguvu, atawasaidia na kuwashika msianguke. Yeye ni Mungu ndiye chanzo cha neema yote. Aliwachagua mshiriki katika utukufu wake ndani ya Kristo. Utukufu huo utadumu milele. 11 Uwezo wote ni wake milele. Amina.

Salamu za Mwisho

12 Sila ataileta barua hii kwenu. Nafahamu kwamba ni ndugu mwaminifu katika familia ya Mungu. Niliandika barua hii fupi kuwatia moyo na kuwaambia kuwa hii ni neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.

13 Kanisa lililoko Babeli[b] linatuma salamu kwenu. Wameteuliwa kama ninyi. Marko, ambaye ni kama mwanangu kwangu katika Kristo, anawasalimu pia. 14 Mpeni kila mmoja wenu salamu maalumu[c] mnapokutana.

Amani iwe kwenu ninyi nyote mlio katika Kristo.

Footnotes

  1. 5:2 kundi lake Mungu Watu wa Mungu. Ni kama kundi la kondoo linalotakiwa kutunzwa.
  2. 5:13 Kanisa lililoko Babeli Pengine hapa inamaanisha Kanisa lililo Rumi.
  3. 5:14 salamu maalumu Kwa maana ya kawaida, “busu”.