Viongozi Katika Kanisa

Neno hili ni kweli, kwamba mtu akitaka kuwa askofu, anata mani kazi njema. Basi, askofu awe mtu asiye na lawama. Awe mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtaratibu, mkarimu na aju aye kufundisha. Asiwe mlevi, wala mgomvi bali awe mpole; asiwe mbishi wala mtu apendaye fedha. Aweze kuisimamia nyumba yake vizuri akiwafanya watoto wake kuwa wanyenyekevu na wenye heshima katika hali zote. Kwa maana kama mtu hawezi kuitawala nyumba yake mwenyewe atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu? Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajiona na kuhukumiwa kama shetani alivyohukumiwa. Kadhalika, awe mwenye sifa njema kati ya watu wa nje ya kanisa, asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa shetani.

Wasaidizi Katika Kanisa

Vivyo hivyo mashemasi wawe wenye kuheshimika, si wenye kauli mbili au wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha. Wanapaswa kuizingatia ile siri ya imani kwa dhamiri safi. 10 Ni lazima wapimwe kwanza na wakionekana kuwa wanafaa basi waruhusiwe kutoa huduma ya ushemasi. 11 Hali kadhalika, wake zao wawe wenye kuheshimika, si wasengenyaji bali wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote. 12 Shemasi awe mume wa mke mmoja; na aweze kuwatawala watoto wake na jamaa yake vema. 13 Watu wanaotoa huduma njema ya ushemasi hujipatia heshima kubwa na uha kika mkubwa katika imani yao kwa Kristo Yesu.

14 Ninakuandikia mambo haya sasa ingawa natarajia kuwepo pamoja nawe karibuni, 15 ili kama nikicheleweshwa, upate kujua jinsi watu wanavyopaswa kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. 16 Bila shaka yo yote, siri ya dini yetu ni kuu: Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, alithibitishwa katika Roho, alionwa na mal aika, alihubiriwa kati ya mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, aka chukuliwa juu katika utukufu.

Viongozi katika Kanisa

Usemi huu ni wa kweli kwamba yeyote mwenye nia ya kuhudumu kama mzee,[a] anatamani kazi njema. Mzee[b] lazima awe mtu mwema asiyelaumiwa na mtu yeyote. Anapaswa kuwa mwaminifu kwa mke wake.[c] Anapaswa kuwa na kiasi, mwenye busara na mwenye mwenendo mzuri katika maisha, anayeheshimiwa na watu wengine, aliye tayari kuwasaidia watu kwa kuwakaribisha katika nyumba yake. Ni lazima awe mwalimu mzuri. Askofu asizoee kunywa mvinyo wala kuwa mgomvi. Bali awe mpole na mtu wa amani, na asiyependa fedha. Ni lazima awe kiongozi mzuri kwa familia yake mwenyewe. Hii ina maana kwamba watoto wake wanamtii kwa heshima zote. Ikiwa mtu hawezi kuiongoza familia yake mwenyewe, hawezi kulitunza Kanisa la Mungu.

Ni lazima askofu asiwe yule aliyeamini hivi karibuni. Hii inaweza kumfanya awe na kiburi. Kisha anaweza akahukumiwa kwa kiburi chake kama vile Shetani alivyopanga. Pia, ni lazima askofu aheshimiwe na watu walio nje ya Kanisa. Kwa namna hiyo hataweza kukosolewa na kuabishwa na wengine na kunasa kwenye mtego wa Shetani.

Mashemasi

Kwa njia hiyo hiyo, watu wanaoteuliwa kuwa mashemasi inawapasa kuwa wale wanaostahili kuheshimiwa. Wasiwe watu wanaosema mambo wasiokuwa nayo moyoni au wanaotumia muda wao mwingi katika ulevi. Wasiwe watu wanaowaibia fedha watu wengine kwa udanganyifu. Ni lazima waifuate imani ya kweli ambayo Mungu ameiweka wazi kwetu na sikuzote wawe watu wanaotenda mambo yaliyo sahihi. 10 Hao unapaswa kuwapima kwanza. Kisha, ukigundua kuwa hawawezi kushitakiwa jambo lolote baya walilotenda, basi wanaweza kuwa mashemasi.

11 Kwa njia hiyo hiyo wanawake wanaoteuliwa kuwa mashemasi wanapaswa kuwa wale wanaoastahili kuheshimiwa. Wasiwe wanawake wanaosema mambo mabaya juu ya watu wengine. Ni lazima wawe na kiasi. Ni lazima wawe wanawake wanaoweza kuaminiwa kwa kila jambo.

12 Wanaume walio mashemasi lazima wawe waaminifu katika ndoa. Ni lazima wawe viongozi wema wa watoto na familia zao binafsi. 13 Mashemasi wanaofanya kazi yao vyema wanajitengenezea nafasi nzuri ya kuheshimiwa. Nao kwa kiasi kikubwa sana wanajihakikishia imani yao katika Kristo Yesu.

Siri ya Maisha Yetu

14 Ninatarajia kuja kwenu hivi karibuni. Lakini ninakuandikia maneno haya sasa, 15 ili kwamba, hata kama sitakuja mapema, utafahamu jinsi ambavyo watu wanapaswa kuishi katika familia[d] ya Mungu. Familia hiyo ni kanisa la Mungu aliye hai. Na Kanisa la Mungu ni msaada na msingi wa ukweli. 16 Ndiyo, Mungu ametuonesha siri ya maisha yanayompa heshima na kumpendeza Yeye. Siri hii ya ajabu ni ukweli ambao wote tunakubaliana nao:

Kristo[e] alijulikana kwetu katika umbile la kibinadamu;
    alioneshwa na Roho[f] kuwa kama alivyojitambulisha;
alionwa na malaika.
    Ujumbe kuhusu Yeye ulitangazwa kwa mataifa;
watu ulimwenguni walimwamini;
    alichukuliwa juu mbinguni katika utukufu.

Footnotes

  1. 3:1 mwenye nia ya kuhudumu kama mzee Yaani, “Mwenye nia ya kuwa msimamizi.”
  2. 3:2 Mzee Yaani, “mwangalizi”. Tazama Mzee, Wazee katika Orodha ya Maneno.
  3. 3:2 mwaminifu kwa mke wake Kwa maana ya kawaida, “mume wa mke mmoja”, ambayo inaweza kutafsiriwa, “mume wa mke mmoja” au “aliyeolewa mara moja”. Pia katika mstari wa 12.
  4. 3:15 familia Kwa maana ya kawaida, “nyumba”. Hii inaweza kumaanisha kuwa watu wa Mungu ni kama hekalu la Mungu.
  5. 3:16 Kristo Kwa maana ya kawaida, “Yeye ambaye”. Nakala zingine za Kiyunani zimetumia “Mungu”.
  6. 3:16 na Roho Au “katika umbo lake la kiroho”.