Add parallel Print Page Options

Usiseme kwa hasira kwa mtu mzima. Lakini sema naye kama baba yako. Watunze vijana kama kaka zako. Watendee wanawake wazee kama mama zako. Na watendee wanawake vijana kwa heshima zote kama vile ni dada zako.

Kuwatunza Wajane

Watunze wajane ambao hasa wanahitaji msaada. Lakini mjane akiwa na watoto au wajukuu, jambo la kwanza ambalo wanahitaji kujifunza ni hili: kutimiza wajibu waliyonao kwa wanafamilia wao. Kwa kuwapa heshima na kuwahudumia, watakuwa wanawalipa fadhila wazazi wao na pia mababu na nyanya zao. Na haya ndiyo mambo yanaompendeza Mungu. Mjane ambaye hakika anahitaji msaada ni yule ambaye ameachwa pekee yake. Anamuamini Mungu kumtunza katika mahitaji yake. Anayemuomba msaada Mungu wakati wote. Lakini mjane anayetumia maisha yake kujipenda ni hakika amekufa angali hai. Wambie waumini huko kutunza familia zao wenyewe ili kwamba asiwepo yeyote atakayesema wanafanya vibaya. Kila mtu atunze watu wa kwao, muhimu sana watunze familia zao. Kama hawatendi hayo watakuwa hawakubaliani na tunayoamini. Watakuwa wabaya kuliko hata asiyeamini.

Ili kuongezwa kwenye orodha ya wajane, mwanamke ni lazima awe na umri wa miaka 60 au zaidi, awe aliyekuwa mwaminifu kwa mume[a] wake. 10 Ni lazima ajulikane kwa mema aliyoyafanya: kulea watoto, kukaribisha wageni kwenye nyumba yake, kuwasaidia watu wa Mungu wenye uhitaji,[b] wenye shida, na kutumia maisha yake kufanya wema wa aina zote.

11 Lakini usiwaweke wajane wachanga katika orodha. Nguvu zao za mahitaji ya mwili zinawavuta wajiondea kwa Kristo, wanataka kuolewa tena. 12 Kisha watahukumiwa kustahili adhabu kwa kutofanya walichoahidi kutenda hapo kwanza. 13 Pia, wajane hawa vijana wanaanza kupoteza muda wao kwa kujihusisha na mambo ya watu wengine yasiyowahusu. Wanazungumzia mambo ambayo wasingepaswa kuzungumza. 14 Hivyo nataka wajane vijana kuolewa, kuzaa watoto, na kutunza nyumba zao. Kama wakifanya hivi, adui yetu hatakuwa na sababu ya kutupinga kwa sababu yao. 15 Lakini wajane wengine vijana wamegeuka na kumfuata Shetani.

16 Kama yupo mwanamke aliyeamini aliye na wajane katika familia yake, ni lazima awatunze yeye mwenyewe. Ndipo Kanisa halitakuwa na mzigo wa kuwatunza hao bali kuwatunza ambao hawana mtu yeyote wa kuwasaidia.

Mambo mengine zaidi juu ya Wazee na mengineyo

17 Wazee wanaoliongoza Kanisa katika njia nzuri wanapaswa kupokea heshima mara mbili;[c] hasa wale wanaofanya kazi ya kuhubiri na kufundisha. 18 Kama Maandiko yanavyosema, “Mnyama wa kazi akitumika kutenganisha ngano, usimzuie kula nafaka.”(A) Na Maandiko pia yanasema, “Mfanyakazi anatakiwa kupewa ujira wake.”(B)

19 Usimsikilize yeyote anayemshitaki mzee. Unatakiwa kuwasikiliza tu kama wapo wawili au watatu ambao wanaweza kusema alichokosea mzee. 20 Waambie wazee wanaotenda dhambi kwamba wana hatia, ufanye hivi mbele ya kanisa lote ili wengine wapate kuonywa.

21 Mbele ya Mungu na Kristo Yesu na malaika walioteuliwa, nakuambia fanya hukumu hizo bila upendeleo. Mtendee kila mtu sawa sawa.

22 Fikiri kwa makini kabla ya kuweka mikono yako juu ya yeyote kumfanya mzee. Usishiriki dhambi za wengine, na ujitunze uwe safi.

23 Timotheo, acha kunywa maji tu, kunywa na kiasi kidogo cha mvinyo. Hii itakusaidia tumbo lako, na hutaugua mara kwa mara.

24 Dhambi za watu wengine ni rahisi kuziona, hizo zinaonesha kwamba watahukumiwa. Lakini dhambi za wengine zitajulikana tu hapo baadaye. 25 Inafanana na mambo mazuri wanayofanya watu. Zingine ni rahisi kuonekana. Lakini hata kama si dhahiri sasa, hakuna hata moja itakayojificha milele.

Footnotes

  1. 5:9 awe aliyekuwa mwaminifu kwa mume “Mwaminifu kwa mume wake” inamaanisha “mwanamke awe na mtu mmoja.” Au aliyeolewa: Misalaba ya wanawake nyakati za Paulo mara nyingi zilitambulisha kwamba walikuwa wameolewa mara moja tu katika maisha yao. Hili lilitafsiriwa kuwa maisha safi ya heshima ya mwanamke au kuheshimika. Maana ya wazi, “mke wa mume mmoja”, inayoweza pia kutafsiriwa, “mke wa mume mmoja” au “aliyeolewa mara moja tu”.
  2. 5:10 kuwasaidia … uhitaji Kwa maana ya kawaida, “kuosha miguu”, mila ya utamaduni wa karne ya kwanza, kwa sababu watu walivaa viatu vya wazi na kutembea kwenye barabara za vumbi nyingi.
  3. 5:17 heshima mara mbili Au “malipo mara mbili”.