Karama Za Unabii Na Lugha

14 Fuateni upendo na kutaka sana karama za Roho, hasa karama ya unabii. Kwa maana anayesema kwa lugha, hasemi na watu bali anasema na Mungu. Hakuna mtu anayemwelewa, kwani anasema siri katika Roho. Lakini anayetamka neno la Mungu anasema na watu akiwasaidia kupata nguvu, na kuwatia moyo na kuwafariji. Anayesema katika lugha anajijenga mwenyewe, lakini anayetoa neno la Mungu analijenga kanisa. Ningependa ninyi nyote mseme kwa lugha ngeni, lakini ningependa zaidi nyote muweze kutoa una bii kwa kuhubiri neno la Mungu. Kwa kuwa anayehubiri neno la Mungu ni mkuu kuliko anayesema kwa lugha, isipokuwa kama kuna mtu wa kutafsiri, ili kanisa zima liweze kusaidika.

Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha ngeni, nitapata faida gani kama sikuwaletea mafunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho? Hata vyombo vya muziki visivyo na uhai kama vile filimbi au kinubi, visipotumiwa kwa mpangilio wa sauti, ni nani atakayeweza kufahamu ni wimbo gani unaimbwa? Na kama baragumu ikitoa sauti isiyoeleweka, ni nani atakayej iandaa kwenda vitani? Hali kadhalika na ninyi. Kama mkisema kwa lugha isiyoeleweka, watu watafahamuje mnachosema? Kwa maana mta kuwa mnasema hewani.

10 Bila shaka ziko lugha nyingi ulimwenguni, na hakuna lugha isiyo na maana. 11 Lakini ikiwa sielewi maana ya lugha inayotu mika nitakuwa mgeni kwa yule anayezungumza, naye atakuwa mgeni kwangu. 12 Hali kadhalika na ninyi. Kwa kuwa mna hamu ya kuwa na karama za Roho, wekeni bidii katika karama zinazolijenga kanisa.

13 Kwa hiyo anayesema kwa lugha aombe kupewa kipawa cha kutafsiri lugha. 14 Kwa maana nikiomba kwa lugha roho yangu inaomba, lakini akili yangu haishiriki. 15 Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho na nitaomba kwa akili yangu pia. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia. 16 Vinginevyo, kama mkim sifu Mungu katika roho, mtu mwingine ambaye anashiriki katika mkutano wenu na ambaye haelewi atawezaje kusema, ‘Amina 17 Mnaweza kuwa mnatoa shukrani kweli, lakini huyo mtu mwingine hajengeki. 18 Namshukuru Mungu kwamba mimi ninasema kwa lugha kuliko ninyi nyote. 19 Lakini hata hivyo, nikiwa kanisani, ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno elfu kumi kwa lugha.

20 Ndugu zangu, msiwe kama watoto wadogo katika kufikiri kwenu. Kuhusu uovu muwe kama watoto wachanga, lakini katika kufi kiri, muwe watu wazima. 21 Imeandikwa katika sheria, “Kwa njia ya watu wenye lugha ngeni na kupitia midomo ya wageni, nitazun gumza na hawa watu, lakini hata hivyo hawatanisikiliza, asema Bwana.”

Bwana.”

22 Kwa hiyo lugha ngeni ni ishara kwa watu wasioamini, na si kwa ajili ya waamini. Lakini unabii ni kwa ajili ya waamini, na si kwa ajili ya wasioamini. 23 Kwa hiyo kama kanisa lote likiku tana na wote wakasema kwa lugha, kisha akaingia mgeni au asi yeamini, je, si atadhani wote mna kichaa? 24 Lakini ikiwa wote wanahubiri unabii wa neno la Mungu, na akaingia mtu asiyeamini au mgeni, atakuwa na uhakika kuwa yeye ni mwenye dhambi kutokana na yale yanayosemwa na wote, 25 na siri zote za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akisema, “Kweli Mungu yupo pamoja nanyi!”

Kumwabudu Mungu Kwa Mpango

26 Tuseme nini basi ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mtu ana wimbo, au neno la mafundisho, mafunuo, ujumbe katika lugha ngeni, au tafsiri ya lugha. Kila jambo lifanyike kwa sha baha ya kujengana. 27 Kama mtu akisema kwa lugha, basi waseme si zaidi ya wawili au watatu, mmoja baada ya mwingine; na lazima awepo mtu wa kutafsiri. 28 Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, huyo mzungumzaji akae kimya kanisani na aseme na nafsi yake mwe nyewe na Mungu. 29 Watu wawili au watatu walio na unabii wa neno la Mungu waseme, na wengine wapime kwa makini yale yanayosemwa. 30 Kama mmoja wa wale waliokaa akipata mafunuo kutoka kwa Mungu, anayezungumza aache kusema. 31 Kwa maana wote mnaweza kutoa una bii, mtu mmoja mmoja, ili kila mtu anayesikiliza apate kufund ishwa na kutiwa moyo. 32 Roho za unabii ziko chini ya mamlaka ya manabii. 33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani. Kama ilivyo desturi katika mikutano ya watu wa Mungu,

34 wanawake wanapaswa kukaa kimya kanisani. Hawaruhusiwi kusema, bali wanyenyekee kama sheria inavyosema. 35 Kama wakitaka kuu liza kitu, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza kanisani. 36 Je, mnadhani neno la Mungu lil itoka kwenu? Au ni ninyi tu ambao neno la Mungu limewafikia?

37 Kama mtu anadhani yeye ni nabii, au ana karama za kiroho, basi akubali kwamba haya ninayoandika ni amri kutoka kwa Bwana. 38 Kama mtu asipotambua haya hatatambuliwa. 39 Kwa hiyo ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii na msikataze watu kusema kwa lugha. 40 Lakini kila kitu kitendeke kwa utaratibu mzuri.

Zitumieni Karama za Roho Kulisaidia Kanisa

14 Upendo uwe lengo la maisha yenu, lakini mnapaswa pia kuzitaka karama za Roho. Na itakeni sana karama ya unabii. Nitafafanua ni kwa nini. Wenye karama ya kusema kwa lugha zingine hawazungumzi na watu. Huzungumza na Mungu. Hakuna anayewaelewa kwa sababu huzungumza mambo ya siri kupitia Roho. Lakini wanaotabiri huzungumza na watu. Huwasaidia watu kuwa imara katika imani, na huwatia moyo na kuwafariji. Wanaosema kwa lugha hujiimarisha wao wenyewe. Lakini wanaotabiri huliimarisha kanisa lote.

Ningependa ninyi nyote muwe na karama ya kusema kwa lugha zingine. Lakini ninachotaka zaidi ni ninyi kutabiri. Yeyote anayetabiri ni wa muhimu zaidi kuliko wale wanaosema kwa lugha zingine. Hata hivyo, ikiwa wanaweza kufasiri lugha hizo, basi kanisa linasaidiwa kutokana na kile wanachosema.

Ndugu zangu, je, itawasaidia nikija kwenu na kusema kwa lugha zingine? Hapana, itawasaidia pale tu nitakapowaletea ufunuo mpya au maarifa fulani, unabii au mafundisho. Hii ni kweli hata kwa vitu visivyo na uhai vinavyotoa sauti kama filimbi na kinubi. Ikiwa muziki hauchezwi kwa ufasaha, hutaweza kujua ni wimbo gani unaopigwa. Na katika vita, ikiwa tarumbeta haitatoa ishara vizuri, askari hawawezi kujua kuwa ni wakati wa kujiandaa kwa mapigano.

Ndivyo ilivyo hata kwenu ninyi. Watu hawataweza kuelewa unachosema, ikiwa utazungumza katika lugha tofauti wasiyoitambua. Utakuwa unazungumza hewani tu! 10 Ni dhahiri kuwa kuna lugha nyingi ulimwenguni, na zote zina maana. 11 Lakini ikiwa sielewi maana ya maneno wanayosema wengine, kwangu itakuwa sauti ya ajabu tu, na nitasikika kama ninayetoa sauti za ajabu. 12 Kwa kuwa mna nia kuhusu karama za Kiroho, muwe na hamu ya kulisaidia kanisa kuwa imara.

13 Hivyo wenye karama ya kusema kwa lugha waombe ili waweze kufasiri yale wanayosema. 14 Ninapoomba kwa lugha zingine, roho yangu inaomba, lakini akili yangu haifanyi chochote. 15 Hivyo nifanye nini? Nitaomba kwa roho yangu, lakini pia nitaomba kwa akili yangu. Nitaimba kwa roho yangu, lakini pia nitaimba kwa akili yangu. 16 Unaweza ukawa unamshukuru Mungu kwa roho yako. Lakini mtu mwingine ambaye haielewi lugha unayotumia hawezi kusema “Amina” kwa maombi yako ya shukrani. 17 Unaweza ukawa unamshukuru Mungu katika njia nzuri, lakini isiwasaidie wengine kuwa imara.

18 Ninamshukuru Mungu kwamba nimepewa karama ya kusema lugha aina nyingi mbalimbali kuliko yeyote kati yenu. 19 Lakini wakati wa mikutano ya kanisa napenda kuzungumza maneno matano ninayoyaelewa kuliko maelfu ya maneno katika lugha zingine. Ni afadhali nizungumze nikiwa katika uelewa wangu ili niwafundishe wengine.

20 Ndugu zangu, msiwaze kama watoto wadogo. Iweni kama watoto wachanga katika mambo maovu, lakini katika kuwaza kwenu muwe kama watu wazima, waliokua. 21 Kama Maandiko[a] yanavyosema,

“Kwa kutumia wanaozungumza lugha tofauti
    na kutumia midomo ya wageni,
nitazungumza na watu hawa,
    hata hivyo, hawatanitii.”(A)

Hivi ndivyo Bwana anasema.

22 Na kutokana na hili tunaona kwamba matumizi ya lugha zingine ni ishara kuonesha namna ambavyo Mungu anawashughulikia wasioamini, na si walioamini. Na unabii unaonesha namna ambavyo Mungu hutenda kazi kupitia wanaoamini, na si wasioamini. 23 Chukulieni kuwa kanisa lote limekusanyika nanyi nyote mkaanza kusema kwa lugha zingine. Ikiwa baadhi ya watu wasio sehemu ya kundi lenu au wasio waamini wataingia katika kusanyiko lenu, watasema ninyi ni wendawazimu. 24 Lakini chukulieni kuwa ninyi nyote mnatabiri na mtu asiyeamini ama asiyekuwa sehemu ya kundi lenu akaingia. Dhambi zao zitawekwa wazi kwao, na watahukumiwa kwa kila kitu mtakachosema. 25 Mambo ya siri katika mioyo yao yatajulikana. Na watapiga magoti na kumwabudu Mungu. Watakiri na kusema, “Pasipo shaka, Mungu yuko hapa pamoja nanyi.”[b]

Mikutano Yenu Inapaswa Kuwasaidia Wote

26 Basi ndugu, mnapaswa kufanya nini? Mnapokusanyika, mtu mmoja ana wimbo, mwingine ana mafundisho na mwingine ana kweli mpya kutoka kwa Mungu. Mmoja anasema kwa lugha nyingine na mwingine anafasiri lugha hiyo. Cho chote mnachofanya lazima kiwe na lengo la kumfanya kila mmoja wenu akue katika imani. 27 Mnapokusanyika, ikiwa kuna yeyote atasema na kanisa katika lugha, iwe watu wawili tu au isiwe zaidi ya watu watatu. Na wanapaswa wanene kwa zamu, mmoja baada ya mwingine. Na mwingine afasiri kile wanachosema. 28 Lakini ikiwa hakuna mfasiri, basi mtu yeyote anayesema kwa lugha nyingine anapaswa kunyamaza kimya. Wanapaswa kuzungumza katika nafsi zao wenyewe ama na Mungu.

29 Na manabii wawili au watatu tu ndiyo wanapaswa kuzungumza. Wengine watathmini kile wanachosema. 30 Na ujumbe kutoka kwa Mungu ukimjia mtu aliyekaa, mzungumzaji wa kwanza anapaswa kunyamaza. 31 Nyote mnaweza kutabiri mmoja baada ya mwingine. Kwa njia hii kila mmoja anaweza kufundishwa na kutiwa moyo. 32 Roho za manabii ziko chini ya udhibiti wa manabii[c] wenyewe. 33 Mungu si Mungu wa machafuko lakini ni Mungu wa amani. Hii ni kanuni kwa ajili ya mikutano yote ya watu wa Mungu.

34 Wanawake wanapaswa kunyamaza katika mikutano hii ya kanisa. Kama Sheria ya Musa inavyosema, hawaruhusiwi kuzungumza pasipo utaratibu bali wawe chini ya mamlaka. 35 Wakiwa na jambo wanalotaka kujua, wawaulize waume zao nyumbani. Ni aibu kwa mwanamke kuzungumza pasipo utaratibu katika mikutano ya kanisa.

36 Je, ni kutoka kwenu neno la Mungu lilikuja ama lilikuja kwa ajili yenu pekee? 37 Ikiwa yeyote kati yenu anafikiri kuwa yeye ni nabii au kwamba ana karama ya kiroho, anapaswa kuelewa kuwa ninachowaandikia ninyi nyote ni amri ya Bwana. 38 Ikiwa yeyote miongoni mwenu hatalikubali hili, basi hatakubaliwa.

39 Hivyo ndugu zangu, mzingatie sana kutabiri. Na msimzuie mtu yeyote kutumia karama ya kusema katika lugha zingine. 40 Lakini kila kitu kifanywe kwa usahihi na kwa utaratibu.

Footnotes

  1. 14:21 Maandiko Kwa maana ya kawaida, “sheria au torati”, ambapo wakati mwingine inamaanisha Agano la Kale.
  2. 14:25 Tazama Isa 45:14 na Zek 8:23.
  3. 14:32 Roho za manabii … udhibiti wa manabii Yaani, manabii wanaweza wakajizuia na kusubiri zamu yao kwa utaratibu mzuri.