Add parallel Print Page Options

23 Mafundisho niliyowafundisha ni yale yale niliyopokea kutoka kwa Bwana, ya kwamba usiku ule ambao Bwana Yesu alikamatwa, aliuchukua mkate 24 na akashukuru. Kisha akaumega na kusema, “Huu ni mwili wangu; ni kwa ajili yenu. Uleni mkate huu kwa ajili ya kunikumbuka mimi.” 25 Kwa namna hiyo hiyo, baada ya wote kula, Yesu alichukua kikombe cha divai na akasema, “Divai hii inawakilisha agano jipya ambalo Mungu anafanya na watu wake, linaloanza kwa sadaka ya damu yangu. Kila mnywapo divai hii, fanyeni hivi kwa ajili ya kunikumbuka mimi.”

Read full chapter