Paulo Atetea Huduma Yake

10 Mimi Paulo nawaandikia nikiwasihi kwa unyenyekevu na upole wa Kristo, mimi ambaye ni mpole ninapokuwa pamoja nanyi, lakini mwenye ujasiri nikiwa mbali nanyi! Nawaomba msinifanye niwe mkali nitakapofika kwenu, kama ninavyotarajia kuwa mkali kwa watu fulani, ambao wanadhani kwamba nafuata kawaida za dunia katika mwenendo wangu. Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani kama watu wa ulimwengu. Silaha zetu si za kidunia, bali silaha zetu zina nguvu ya kimungu iwezayo kubomoa ngome. Tunaharibu hoja na mabishano yaliyo kinyume cha kumjua Mungu. Tunateka mawazo yote na kuyafanya yamtii Kristo, na tutakuwa tayari kuadhibu uasi wo wote baada ya kuhakikisha utii wenu. Tazameni vizuri mambo yaliyo mbele ya macho yenu. Kama mtu ye yote anaamini kuwa yeye ni wa Kristo, basi ajiangalie tena, kwa maana na sisi pia ni wa Kristo kama yeye alivyo. Kwa sababu hata kama tunajivunia mno madaraka tuliyo nayo, ambayo Bwana ametupatia kwa ajili ya kuwa jenga na sio kuwagandamiza, sitaona haya kuyatumia. Sitaki ionekane kama nataka kuwatisha kwa barua zangu. 10 Kwa maana wengine wanasema, “Barua zake zina uzito na ni kali lakini mtu mwenyewe ni mdhaifu na kuzungumza kwake hakuvutii.” 11 Watu kama hao wajue ya kuwa, wanavyotuona katika barua tukiwa hatupo nanyi, ndivyo tulivyo, na ndivyo tutakavyofanya tutakapo kuwa pamoja nanyi. 12 Hatuthubutu kujiweka kwenye kundi moja au kujilinganisha na hao wanaojiona kuwa wao ni wa maana sana. Wana pojilinganisha wenyewe kwa wenyewe, wanaonyesha ya kuwa hawana busara. 13 Lakini sisi hatujajivuna kupita kiasi, bali majivuno yetu yatakuwa katika mipaka ambayo Mungu ametuwekea, na mipaka hiyo inawafikia hata na ninyi. 14 Kwa maana hatupiti mipaka tunapowajumlisha katika huduma yetu kwa sababu tulikuwa wa kwanza kuwaletea Injili ya Kristo. 15 Hatupiti mipaka na kujivunia kazi ya watu wengine. Lakini matumaini yetu ni kwamba, imani yenu inavyozidi kukua, huduma yetu kwenu itaendelea kupanuka, 16 ili tuweze kuhubiri Injili hata nchi zilizopakana nanyi, bila kujivu nia kazi iliyokwisha fanywa katika sehemu ya mtu mwingine. 17 “Anayejivuna na ajivune katika Bwana.” 18 Kwa maana sio mtu anayejisifu ambaye anapata kibali, bali ni mtu ambaye Bwana anamsifu.

Paulo Aitetea Huduma yake

10 Mimi, Paulo, ninawasihi kwa unyenyekevu na upole wa Kristo. Wengine wanasema kuwa nina ujasiri ninapowaandikia nikiwa mbali, lakini ni mwoga kusema jambo lo lote ninapokuwa pamoja nanyi. Wanadhani sababu ya kutenda yale tunayoyafanya ni kama zile za kidunia. Ninapanga kuwa jasiri sana kinyume chao watu hao hapo ninapokuja kwenu. Tafadhali ninawaomba, sitahitaji kutumia ujasiri huo kwenu. Tunaishi katika ulimwengu huu, lakini hatupigani vita yetu kama ulimwengu unavyopigana. Silaha tunazozitumia si za kibinadamu. Silaha zetu zina nguvu kutoka kwa Mungu na zinaweza kuharibu ngome za adui. Tunaharibu mabishano ya watu, na tunasambaratisha kila wazo la kiburi linalojiinua kinyume cha elimu ya Mungu. Pia tunateka kila wazo na kulitiisha ili limtii Kristo. Tuko tayari kumwadhibu kila mtu asiyetii, lakini tunataka ninyi muwe watiifu ipasavyo kwanza.

Mnatakiwa kuchunguza ukweli halisi wa mambo ulio mbele ya macho yenu. Ikiwa mna uhakika kuwa ninyi ni wa Kristo, mnapaswa kukumbuka kuwa na sisi ni wa Kristo kama ninyi mlivyo wa Kristo. Inaweza kuonekana kana kwamba tunajivuna sana kupita kiasi kidogo kuhusu mamlaka ambayo Bwana ametupa sisi. Lakini alitupa mamlaka hii ili kuwatia nguvu ninyi, na sio kuwaumiza. Hivyo sitaona haya kwa lolote ambalo tumejisifu kwalo. Sitaki mfikiri kuwa najaribu kuwatisha kwa barua zangu. 10 Wengine wanasema, “Barua za Paulo zina shuruti na matakwa mengi, Lakini anapokuwa pamoja nasi, ni mdhaifu na msemaji asiyefaa.” 11 Watu hao wanapaswa kulielewa jambo hili: tutakapokuwa pamoja nanyi, tutatenda mambo kwa ujasiri ule ule tunaouonyesha sasa katika barua zetu.

12 Hatujaribu kujiweka katika daraja moja na wale wanaojisifu wenyewe. Hatujilinganishi na watu hao. Wao wanatumika wenyewe kwa kujipima wenyewe, na wanajilinganisha miongoni mwao wenyewe. Hili linadhihirisha kuwa hawajui lolote.

13 Lakini hatutajisifia lolote nje ya kazi tuliyopewa kuifanya. Tutaweka ukomo wa kujisifia kwetu katika kazi aliyotupa Mungu kuifanya, lakini kazi hii inajumuisha kazi yetu kwenu. 14 Tungekuwa tunajivuna zaidi na zaidi ikiwa tungekuwa hatujafika kabisa kwenu. Lakini tulikuwa wa kwanza kufika kwenu na Habari Njema ya Kristo. 15 Tumeweka ukomo wa kujivuna kwetu katika kazi ambayo ni yetu. Hatujivunii kazi ambayo wameifanya watu wengine. Tunatumaini kuwa imani yenu itaendelea kukua. Tunatumaini kuwa mtaisadia kazi yetu kukua zaidi na zaidi. 16 Tunataka kuieneza habari njema katika maeneo ya mbali zaidi kupita mji wenu. Hatutaki kujisifia juu ya kazi ambayo imefanywa na mtu mwingine katika eneo lake. 17 “Yeyote anayejisifu na ajisifu juu ya Bwana tu.”(A) 18 Kile watu wanachosema kuhusu wao wenyewe hakina maana yeyote. Cha muhimu ni ikiwa Bwana anasema kuwa wamefanya vizuri.