Ombi Kuhusu Maombezi

Hatimaye, ndugu wapendwa, tuombeeni ili neno la Mungu lienee upesi na kukubaliwa kama ilivyokuwa kwenu. Ombeni pia kwamba tuokolewe kutokana na watu waovu na wasio na haki, kwa maana si watu wote wanaamini. Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana na yule mwovu. Nasi tuna tumaini kubwa kwa Bwana juu yenu, kwamba mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. Bwana aielekeze mioyo yenu kwenye upendo wa Mungu na katika ustahimilivu wa Kristo.

Onyo Kuhusu Uvivu

Ndugu wapendwa, katika jina la Bwana Yesu Kristo, tuna waagiza mjitenge na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapeni. Maana ninyi wenyewe mnafa hamu jinsi mnavyopaswa kuiga mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa nanyi wala hatukula chakula cha mtu ye yote pasipo kulipa. Bali tulifanya kazi kwa juhudi usiku na mchana ili tusimlemee mtu ye yote kati yenu. Hatukufanya hivi kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada wenu, bali tulitaka tuwape mfano wa kuiga. 10 Maana tulipokuwa pamoja nanyi tuliwapa amri hii: “Ikiwa mtu hatafanya kazi, basi asile.”

11 Tumesikia kwamba baadhi yenu ni wavivu, hawana shughuli maalumu isipokuwa kusengenya wenzao. 12 Sasa tunawaagiza na kuwaonya watu hao katika jina la Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi ili wajipatie chakula wanachokula. 13 Ndugu wapendwa, ninyi msi choke kutenda mema.

14 Ikiwa mtu atakataa kutii maagizo tunayotoa katika barua hii, mwangalieni vema mtu huyo, mjitenge naye, ili apate kuona aibu. 15 Lakini msimhesabu kama adui bali mkanyeni kama ndugu.

Salamu Za Mwisho

16 Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa njia zote. Bwana na awe nanyi nyote.

17 Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwe nyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote.

Tuombee nasi

Na sasa, ndugu zangu, mtuombee. Ombeni kwamba mafundisho ya Bwana yaendelee kuenea haraka na kwamba watu watayaheshimu, kama ilivyotokea kwenu. Mtuombee tupate ulinzi kutokana na watu wabaya na waovu. Mnafahamu, siyo wote wanamwamini Bwana.

Lakini Bwana ni mwaminifu. Atawapa nguvu na ulinzi dhidi ya Mwovu. Tuna uhakika kwa sababu ya Bwana mnayemtumikia na mtaendelea kuyafanya yale tunayowaamuru. Tunaomba kwamba Bwana atasababisha mjisikie upendo wa Mungu na kukumbuka subira ya ustahimilivu wa Kristo.

Wajibu wa Kufanya kazi

Kwa mamlaka ya Bwana wetu Yesu Kristo tunawaambia kukaa mbali na mwamini yeyote anayekataa kufanya kazi. Watu kama hao wanaokataa kufanya kazi hawafuati mafundisho tuliyowapa. Ninyi wenyewe mnafahamu kwamba mnatakiwa kuishi kwa kuiga mfano wetu. Hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi wala hatukuishi pasipo utaratibu unaofaa. Hatukupokea chakula kutoka kwa yeyote bila ya kukilipia. Tulifanya kazi ili tusiwe mzigo kwa yeyote. Tulifanya kazi usiku na mchana. Tulikuwa na haki ya kuomba mtusaidie. Lakini tulifanya kazi ili tuwe mfano wa kuigwa nanyi. 10 Tulipokuwa nanyi, tuliwapa kanuni hii: “Yeyote asiyefanya kazi asile.”

11 Tunasikia kwamba watu wengine katika kundi lenu wanakataa kufanya kazi. Hawashughuliki kufanya kazi badala yake wanashughulika kwa kuyafuatilia maisha ya wengine. 12 Maagizo yetu kwao ni kuwakataza kuwasumbua wengine, waanze kufanya kazi na kupata chakula chao wenyewe. Ni kwa mamlaka ya Bwana Yesu Kristo tuwaagize kufanya hivi. 13 Msichoke kabisa kutenda wema.

14 Wakiwapo wengine huko wanaokataa kufanya tunayowaambia katika barua hii, basi mkumbuke wao ni kina nani. Msichangamane nao. Ndipo pengine wanaweza kujisikia aibu. 15 Lakini msiwafanye kama adui. Washaurini waachane na tabia hiyo kama watu wa nyumbani mwake Mungu.

Maneno ya Mwisho

16 Tunaomba kwamba Bwana wa amani awape amani wakati wote na kwa njia yo yote. Bwana atakuwa pamoja nanyi nyote.

17 Hizi ni salamu zangu kwa mwandiko wangu: Paulo. Ninafanya hivi katika barua zangu zote kuonesha zinatoka kwangu. Hivi ndivyo ninavyoandika.

18 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote.