Kutoka Kwa Mzee. Kwa mpendwa wangu Gayo, nimpendaye katika kweli. Mpendwa, ninakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kwamba uwe na afya njema ya mwili; kwa maana najua roho yako ni salama. Nilifurahi sana walipokuja ndugu kadhaa wakashuhudia jinsi ulivyo mwaminifu katika kweli na jinsi unavyoendelea kuishi katika kweli. Hakuna kitu kinachonifurahisha zaidi kuliko kusi kia kwamba watoto wangu wanafuata kweli.

Uaminifu Wa Gayo

Mpendwa, wewe umekuwa mwaminifu kwa yote unayowatendea hao ndugu, ingawaje wao ni wageni kwako. Wamelishuhudia kanisa kuhusu upendo wako. Tafadhali wasaidie waendelee na safari yao kwa namna itakayompendeza Mungu. Kwa maana wanasafiri kwa ajili ya Bwana na wamekataa kupokea cho chote kutoka kwa watu wasiomjua Mungu . Kwa hiyo tunawajibu wa kuwasaidia watu wa namna hiyo ili tuwe watenda kazi pamoja nao kwa ajili ya kweli.

Diotrefe Na Demetrio

Niliandika barua kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe apendaye kujiweka mbele kama kiongozi wao, hatambui mamlaka yangu. 10 Kwa hiyo nitakapokuja nitaeleza mambo anayofanya; na kuhusu maneno maovu anayosema juu yangu. Wala hatosheki na hayo bali anakataa kuwakaribisha ndugu. Pia anawazuia wale ambao wanataka kuwakarib isha na anawafukuza kutoka katika kanisa. 11 Mpendwa, usiige ubaya bali iga wema. Atendaye mema ni wa Mungu. Atendaye uovu hajapata kumwona Mungu. 12 Demetrio anashuhudiwa wema na kila mtu na hata kweli yenyewe inamshuhudia. Mimi pia ninamshuhudia wema, na wewe unajua kwamba ushuhuda wangu ni wa kweli.

Salamu Za Mwisho

13 Ninayo mengi ya kukuandikia, lakini afadhali nisitumie kalamu na wino. 14 Natarajia kukuona karibuni na tutaongea uso kwa uso.

Salamu toka kwa mzee.[a]

Kwa rafiki mpendwa gayo, mtu ni mpendae kwa dhati.

Rafiki yangu mpendwa, najua kwamba unaendelea vizuri kiroho, kwa hiyo ninaomba kuwa mengine yote yaendelee vizuri pia nawe uwe na afya njema. Baadhi ya waamini walikuja na kunieleza juu ya kweli[b] iliyo katika maisha yako. Waliniambia kuwa unaendelea kuifuata njia ya kweli. Hili lilinifanya nijisikie furaha sana. Daima hili hunipa furaha iliyo kuu ninaposikia kuwa wanangu wanaifuata njia ya kweli.

Rafiki yangu mpendwa, inapendeza kuwa unaonesha uaminifu wako katika kazi yako yote miongoni mwa waaminio. Wengine ambao huwajui. Hao waliliambia kanisa juu ya upendo ulio nao. Tafadhali wasaidie kuendelea na safari yao. Wasaidie katika njia ambayo itampendeza Mungu. Safari hiyo waliyoenda ni ya kumtumikia Kristo. Hawakupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini. Hivyo inatupasa kuwasaidia. Tunapowasaidia, tunashiriki kazi yao katika ile kweli.

Niliandika barua kwa kanisa, ila Diotrefe hasikilizi yale tunayosema. Yeye daima anataka kuwa kiongozi. 10 Nitakapokuja, nitaongea naye mbele ya kanisa juu ya hiki anachokifanya. Anadanganya na kusema mambo mabaya juu yetu, lakini hayo siyo yote. Anakataa kuwapokea na kuwasaidia wanaoamini wanaosafiri kwenda huko. Na hawaruhusu watu wengine kuwasaidia. Kama wakifanya hivyo, anawazuia wasikusanyike na kanisa tena.

11 Rafiki yangu mpendwa, usiige lililo baya; bali iga lililo jema. Yeyote anayetenda yaliyo mema hutoka kwa Mungu. Ila yeyote anayetenda maovu bado hajamjua Mungu.

12 Kila mtu azungumza yaliyo mema juu ya Demetrio, na kweli inakubaliana na yale wasemayo. Pia, twasema mema juu yake. Na unafahamu kuwa tusemayo ni kweli.

13 Nina mambo mengi nataka kukueleza. Lakini sipendi kutumia kalamu na wino. 14 Natumaini kukutembelea hivi karibuni. Hapo tunaweza kukaa pamoja na kuongea uso kwa uso. 15 Amani kwako. Rafiki walio pamoja nami hapa wakutumia upendo wao. Tafadhali wapatie upendo wetu kila rafiki waliopo huko.

Footnotes

  1. 1:1 mzee Huyu huenda alikuwa ni Mtume Yohana. “Mzee” ina maana ya mtu aliye mtu mzima au kiongozi maalumu katika kanisa (kama vile katika Tit 1:5).
  2. 1:3 kweli Kweli au “habari njema” za Yesu Kristo zinazo waunganisha waamini wote pamoja. Pia katika mstari wa 8,12.