Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, pamoja na ndugu yetu Timotheo. Tunakuandikia wewe Filemoni mfanyakazi mwenzetu mpendwa, na dada yetu Afia na askari mwenzetu Arkipo, pamoja na kanisa linalokutana nyumbani kwako Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu

Upendo Na Imani Ya Filemoni

Ninamshukuru Mungu wangu kila ninapokuombea kwa sababu ninasikia habari za upendo wako na imani uliyonayo kwa Bwana wetu Yesu na kwa watakatifu wote. Ninakuombea kwamba unaposhirikiana na wengine juu ya imani yako upate kuelewa kikamilifu kila jambo jema ambalo tunapata ndani ya Kristo. Ndugu yangu, upendo wako umenipa furaha kubwa na faraja, kwa maana wewe umechangamsha mioyo ya watakatifu.

Ombi Kuhusu Onesmo

Kwa sababu hii, ingawa nina ujasiri ndani ya Kristo kuku amuru ufanye linalotakiwa, lakini kwa ajili ya upendo, ninaona ni bora zaidi nikuletee ombi. Mimi Paulo, balozi ambaye sasa ni mfungwa kwa ajili ya Yesu Kristo, 10 ninalo ombi kwako kuhusu mwanangu Onesmo; ambaye nimekuwa baba yake wa kiroho nikiwa gere zani. 11 Hapo awali huyu Onesmo alikuwa hakufai, lakini sasa amekuwa wa manufaa kwako na kwangu pia.

12 Ninamrudisha kwako, yeye ambaye ni kama moyo wangu mwe nyewe. 13 Ningelipenda akae nami hapa anisaidie badala yako wakati huu ambapo niko gerezani kwa ajili ya Injili. 14 Lakini sikupenda kufanya lo lote pasipo wewe kuniruhusu maana sipendi unisaidie kwa kulazimishwa, bali kwa hiari yako mwenyewe.

15 Pengine Onesmo aliondoka kwako kwa muda mfupi kusudi uta kapompata tena uweze kuwa naye daima; 16 na asiwe tena kama mtumwa tu, bali kama ndugu mpendwa. Yeye ni wa thamani sana kwangu lakini hasa zaidi kwako, maana pamoja na kuwa mtumwa wako, sasa ni ndugu yako katika Bwana.

17 Kwa hiyo ikiwa unanihesabu kama mshiriki mwenzako, basi mpokee kama vile ambavyo ungenipokea mimi. 18 Kama amekukosea jambo lo lote au ana deni lako, basi unidai mimi. 19 Mimi Paulo ninaandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe, nitalipa. Wala sidhani nina haja ya kukukumbusha kwamba wewe mwenyewe ni mdeni wangu kwa ajili ya nafsi yako. 20 Kwa hiyo ndugu yangu, ninaamini utafanya jambo hili kwa ajili ya Bwana. Burudisha moyo wangu katika Kristo.

21 Naandika nikiwa na hakika ya kuwa utatii ninalokuambia na kwamba utafanya hata zaidi ya haya. 22 Tena nakuomba unitayar ishie chumba cha kukaa, kwa maana natarajia kurudi kwenu kama jibu la Mungu kwa maombi yenu.

23 Salamu zenu kutoka kwa Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu; 24 na kutoka kwa Marko, Aristarko, Dema na

Kutoka kwa Paulo mfungwa kwa kusudi la Kristo Yesu,[a] na kutoka kwa Timotheo ndugu yetu. Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na mtenda kazi pamoja nasi; kwa Afia dada yetu, Arkipo askari mwenzetu na kwa kanisa linalokutania nyumbani mwako.

Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo ziwe pamoja nawe.

Upendo na Imani ya Filemoni

Namshukuru Mungu wangu siku zote kila ninapokukumbuka katika maombi yangu, kwa sababu nasikia juu ya upendo na uaminifu ulionao katika Bwana Yesu na unaouonesha kwa watu wa Mungu. Ninaomba kwamba ile imani unayoishiriki pamoja nasi ikusaidie wewe kuelewa kila fursa tulio nayo ya kutenda mema kama wale tunaomwamini Kristo. Nimepokea furaha kubwa na faraja kutokana na upendo wako, kwa sababu mioyo ya watu wa Mungu imepata nguvu mpya kwa juhudi zako ndugu yangu.

Mpokee Onesimo Kama Kaka

Hivyo hiyo ndiyo sababu nakuagiza wewe kufanya jambo unalopaswa kulifanya. Kwa mamlaka niliyo nayo katika Kristo naweza kukuamuru kufanya hilo. Lakini sikuamuru; bali kwa sababu ya upendo nakusihi ufanye hivyo. Mimi Paulo, niliye mzee wa umri sasa, na sasa mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu. 10 Ninakusihi kuhusu mwanangu Onesimo niliyemleta[b] katika maisha mapya tulio nayo katika Bwana nilipokuwa gerezani. 11 Huyo ambaye siku za nyuma hakuwa wa manufaa kwako, lakini sasa anafaa[c] sio kwako tu bali hata kwangu mimi.

12 Ninamrudisha kwako, kitu ambacho kimekuwa kigumu sawa na kuupoteza moyo wangu.[d] 13 Ningetamani kuendelea kuwa naye hapa, ili aendelee kunihudumia kwa niaba yako nitakapokuwa bado gerezani kwa ajili ya Habari Njema. 14 Lakini sikuwa tayari kufanya jambo lo lote bila ruhusa yako, ili kila jambo lako zuri litendeke bila lazima bali kwa hiari yako mwenyewe.

15 Labda sababu ya Onesimo kutenganishwa nawe kwa kipindi kifupi ni kuwezesha muwe pamoja siku zote, 16 si mtumwa tena, bali ni zaidi ya mtumwa; kama ndugu mpendwa. Nampenda sana lakini wewe utampenda zaidi, sio tu kama kaka katika familia yenu, bali pia kama mmoja wa walio katika familia ya Bwana.

17 Ikiwa unanitambua mimi kama niliye mwenye imani moja nawe, basi mpokee Onesimo na umkubali kama vile ambavyo ungenikubali. 18 Endapo amekukosea jambo lo lote au unamdai kitu cho chote, unidai mimi badala yake. 19 Mimi Paulo naandika kwa mkono wangu mwenyewe ya kwamba nitakulipa. Tena sina sababu ya kukumbusha kuwa una deni kwangu juu ya maisha yako. 20 Kwa hiyo kaka yangu, kama mfuasi wa Bwana, tafadhali nipe upendeleo[e] katika hili. Ndipo itakuwa faraja kuu kwangu kama kaka yako katika Kristo. 21 Ninapokuandikia barua hii nina ujasiri mkubwa kwamba utakubaliana nami na najua kwamba utafanya zaidi ya haya ninayokuomba.

22 Pamoja na hayo naomba uniandalie chumba cha kufikia, kwa sababu nina matumaini kwamba kwa maombi yenu nitaachiliwa na kuletwa kwenu.

Salamu za Mwisho

23 Epafra mfungwa pamoja nami katika Kristo Yesu anakusalimu. 24 Marko, Aristarko, Dema, na Luka watendakazi pamoja nami nao wanakusalimu.

25 Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.

Footnotes

  1. 1:1 Kristo Yesu Au “Mfalme Yesu”. Neno “Kristo” ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania “Masihi”, ambao ni wadhifa wa kifalme. Tazama Mk 15:32: Lk 23:2. Tazama pia Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno.
  2. 1:10 niliyemleta Paulo alimzaa Onesimo katika imani ya Yesu Kristo.
  3. 1:11 anafaa Hapa Paulo anachezea maneno katika jina la Onesimo, lenye maana “anayefaa”. Aidha ni jina lilitumika zaidi kwa watumwa maana waliwafaa mabwana zao.
  4. 1:12 Kwa maana ya kawaida, “Ninamrudisha kwako, kitu ambacho kimekuwa kigumu sawa na kuupoteza moyo wangu.” Hii ni kama njia ya kusema kwamba kumtuma Onesimo ilikuwa kwa Paulo kana kwamba anapoteza kitu muhimu sana kwake kinachotoka ndani mwake.
  5. 1:20 tafadhali nipe upendeleo Paulo hapa anachezea maneno tena katika jina la Onesimo, akitumia kitenzi kinachofanana na jina.