15 Basi watoza kodi na wenye dhambi wakaja kwa Yesu ili wapate kumsikiliza. Mafarisayo na walimu wa sheria wakaanza kunung’unika, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao!” Ndipo Yesu akawaambia mfano huu: “Tuseme mmoja wenu ana kondoo mia moja halafu mmoja wao apotee. Si ana waacha wale tisini na tisa malishoni aende kumtafuta huyo aliyepotea mpaka ampate? Akisha kumpata atambeba mabegani mwake na kwenda nyum bani. Kisha atawaita marafiki na majirani na kuwaambia, ‘Fura hini pamoja nami; nimempata kondoo wangu aliyepotea.’ Nawaam bieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye na kuacha dhambi zake, kuliko ilivyo kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.”

Shilingi Iliyopotea

“Au tuseme mwanamke ana shilingi kumi halafu apoteze moja. Si atawasha taa afagie nyumba na kutafuta kwa uangalifu mpaka aipate? Na akisha kuipata atawaita marafiki zake na majirani na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimeipata ile shilingi yangu iliyopotea!’ 10 Vivyo hivyo nawaambia, kuna furaha mbele ya mal aika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye na kuacha dhambi.”

Mwana Mpotevu

11 Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu aliyekuwa na watoto wawili wa kiume. 12 Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Basi huyo baba akagawanya mali yake kati yao.

13 “Baada ya muda mfupi yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo akaenda nchi ya mbali akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa. 14 Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote naye akawa hana cho chote. 15 Kwa hiyo akaomba kibarua kwa raia mmoja wa nchi hiyo aliyemtuma shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Akatamani kujish ibisha kwa maganda waliyokuwa wanakula nguruwe, wala hakuna mtu aliyempa cho chote cha kula.

17 “Hatimaye akili zikamrudia, akasema, ‘Ni watumishi wan gapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza nami hapa nakufa kwa njaa! 18 Nitaondoka nirudi kwa baba yangu nikamwambie, ‘Baba, nimetenda dhambi mbele ya Mungu na mbele yako. 19 Sistahili kuitwa mwanao tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’ 20 Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanae, akamkumbatia na kumbusu. 21 Yule mtoto akasema, ‘Baba, nimekosa mbele ya Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.’ 22 Lakini baba yake aka waambia watumishi, ‘Leteni upesi kanzu iliyo bora mumvalishe. Pia mvalisheni pete na viatu. 23 Kisha mleteni yule ndama aliyenona mkamchinje; ili tule tusherehekee. 24 Kwa maana huyu mwanangu alikuwa amekufa, na sasa yu hai tena; alikuwa amepotea na sasa amepatikana.’ Basi wakaanza sherehe.

25 “Wakati huo kaka yake alikuwa shambani. Alipokuwa ana karibia nyumbani akasikia sauti ya nyimbo na ngoma. 26 Akamwita mmoja wa watumishi akamwuliza, ‘Kuna nini?’ 27 Akamwambia, ‘Mdogo wako amekuja, na baba yako amemchinja yule ndama aliyenona kwa sababu amempata mwanawe akiwa mzima.’ 28 Yule kaka akakasi rika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akaenda nje akaanza kumbembeleza. 29 Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Angalia, miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana mbuzi ili nisherehekee na mara fiki zangu. 30 1Lakini huyu mwanao ambaye ametapanya mali yako kwa makahaba amerudi nyumbani nawe umemchinjia ndama aliyenona!’

31 “Baba yake akamwambia, ‘Mwanangu, umekuwa nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32 Lakini ilitubidi tufurahi na kusherehekea kwa sababu mdogo wako alikuwa amekufa na sasa yu hai tena, alikuwa amepotea naye amepatikana.”’ Mfano Wa Meneja Mjanja

Furaha Mbinguni

(Mt 18:12-14)

15 Watoza ushuru na wenye dhambi wengi waliendelea kuja kumsikiliza Yesu. Hivyo Mafarisayo na walimu wa sheria wakaanza kulalamika wakisema, “Mtazameni mtu huyu[a] huwakaribisha wenye dhambi na hata kula pamoja nao!”

Hivyo Yesu akawaambia mfano huu, “Chukulia mmoja wenu ana kondoo mia, lakini mmoja akapotea. Utafanya nini? Utawaacha wale tisini na tisa na kwenda kumtafuta yule mmoja aliyepotea mpaka umpate. Na ukishampata, utafurahi sana. Utambeba mabegani mwako mpaka nyumbani. Kisha utakwenda kwa majirani na rafiki zako na utawaambia, ‘Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimempata kondoo wangu aliyepotea!’ Katika namna hiyo hiyo ninawaambia, kunakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mtu anayeacha dhambi zake. Kuna furaha zaidi kwa ajili ya mtu mmoja anayeacha dhambi kuliko watu wema tisini na tisa ambao hudhani hawahitaji kubadilika.

Fikiria kuhusu mwanamke mwenye sarafu kumi za fedha,[b] lakini akapoteza sarafu moja kati ya hizo. Atawasha taa na kuifagia nyumba. Ataitafuta sarafu kwa bidii mpaka aione. Na akiiona, atawaita rafiki na jirani zake na kuwaaambia, ‘Furahini pamoja nami, kwa sababu nimeipata sarafu niliyoipoteza!’ 10 Katika namna hiyo hiyo, ni furaha kwa malaika wa Mungu, mwenye dhambi mmoja anapotubu.”

Simulizi Kuhusu Mwana Mpotevu

11 Kisha Yesu akasema, “Alikuwepo mtu mmoja aliyekuwa na wana wawili. 12 Mwana mdogo alimwambia baba yake, ‘Baba, nipe sehemu ya mali ninayotarajia kurithi baadaye.’ Hivyo baba yake akagawa utajiri wake kwa wanawe wawili.

13 Baada ya siku chache yule mdogo akauza mali zake, akachukua pesa zake na akaondoka. Akasafiri mbali katika nchi nyingine. Huko alipoteza pesa zake zote katika starehe na anasa. 14 Baada ya kutumia vyote alivyokuwa navyo, kukatokea njaa kali katika nchi ile yote. Akawa na njaa na mhitaji wa pesa. 15 Hivyo alikwenda kutafuta kazi kwa mwenyeji mmoja wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Alikuwa anasikia njaa kiasi kwamba alikuwa anatamani kula chakula walichokula nguruwe. Lakini hakuna mtu aliyempa chakula.

17 Alipotambua namna alivyokuwa mjinga, akafikiri moyoni mwake na kusema, ‘Wafanyakazi wote wa baba yangu wana chakula kingi. Lakini niko hapa kama niliyekufa kwa sababu sina chakula. 18 Nitaondoka na kurudi kwa baba yangu. Nitamwambia hivi: Baba, nimemtenda Mungu dhambi na nimekukosea wewe. 19 Sistahili kuitwa mwanao tena. Lakini niruhusu niwe kama mmoja wa wafanyakazi wako.’ 20 Hivyo akaondoka na kurudi kwa baba yake.

Alipokuwa mbali na nyumbani kwao, baba yake alimwona, akamwonea huruma. Akamkimbilia, akamkumbatia na kumbusu sana. 21 Mwanaye akasema, ‘Baba, nimemtenda Mungu dhambi na nimekukosea wewe; sistahili kuitwa mwanao tena.’

22 Lakini baba akawaambia watumishi wake, ‘Fanyeni haraka, leteni vazi maalumu, mvikeni. Pia, mvisheni viatu vizuri na pete kwenye kidole chake. 23 Na leteni ndama aliyenona, mchinjeni ili tule na kusherehekea. 24 Kwa sababu mwanangu alikuwa amekufa, lakini sasa yuko hai tena! Alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.’ Wakaanza kusherehekea.

25 Mwanaye mkubwa alikuwa shambani. Alipoikaribia nyumba, alisikia sauti za muziki na kucheza. 26 Akaita mmoja wa watumishi na akamwuliza, ‘Kuna nini?’ 27 Mtumishi akasema, ‘Mdogo wako amerudi, na baba yako amechinja ndama aliyenona. Anafurahi kwa sababu amempata mwanaye akiwa salama na mzima.’

28 Mwana mkubwa alikasirika na hakutaka kwenda kwenye sherehe. Hivyo baba yake akatoka nje kumsihi. 29 Lakini alimwambia baba yake, ‘Tazama, miaka yote hii nimekutumikia kama mtumishi, kamwe sijaacha kukutii! Lakini hujawahi kunipa hata mbuzi mdogo ili nisherehekee pamoja na rafiki zangu. 30 Lakini alipokuja huyu mwanao aliyepoteza mali zako kwa makahaba, umemchinjia ndama aliyenona!’

31 Baba yake akamwambia, ‘Mwanangu, daima umekuwa pamoja nami, na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32 Lakini tulipaswa kusherehekea. Mdogo wako alikuwa amekufa, lakini sasa ni hai tena. Alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.’”

Footnotes

  1. 15:2 mtu huyu Yaani, Yesu. Adui zake walikuwa wanakwepa kutamka jina lake.
  2. 15:8 sarafu kumi za fedha Kila sarafu, Sarafu ya Kiyunani iliyoitwa drachma ilikuwa na thamani ya ujira au mshahara wa siku moja.