0Wakati alipokuwa akifukiza uvumba umati mkubwa wa watu walikuwa nje wakiomba. wakitumia maelezo ya wale wal ioshuhudia mambo haya kwa macho yao na wale waliotabiri habari hizo. Lakini, mimi pia, nimezichunguza habari hizi kuanzia mwanzo. Nami nimeona ni vema nikuandikie kwa mpango, muhtasari huu, ili upate kuwa na hakika ya mambo yote uliyofundishwa.

Utabiri Kuhusu Yohana Mbatizaji

Historia ya mambo haya ilianzia katika jamaa ya kuhani mmoja Myahudi aliyeitwa Zakaria. Yeye aliishi wakati Herode ali pokuwa mfalme wa Yudea na alihudumu katika kikundi cha ukuhani cha Abia. Mkewe Zakaria aliitwa Elizabeti naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni. Zakaria na Elizabeti walikuwa watu wenye kumcha Mungu, wakitii amri zake zote na kutimiza maagizo yake yote kika milifu. Lakini hawakuwa na watoto, maana Elizabeti alikuwa tasa; na wote wawili walishapita umri wa kuzaa. 8-9 Siku moja, kikundi cha Zakaria kilikuwa na zamu Hekaluni na Zakaria alikuwa anafanya huduma yake ya ukuhani kwa Mungu. Walipopiga kura, kama ilivyokuwa desturi, ili wamchague atakayeingia kufukiza uvumba madhabahuni, Zakaria alichaguliwa. 11 Ghafla, malaika wa Bwana akamtokea Zakaria. Akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia uvumba. 12 Zakaria alipomwona huyo mal aika alishtuka akajawa na hofu.

13 Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zakaria! Kwa maana Mungu amesikia maombi yako, na mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yohana. 14 Nawe utakuwa na furaha kubwa moyoni wakati huo na watu wengi watashangilia kuzaliwa kwake. 15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana, hataonja divai wala kinywaji cho chote cha kulevya; atajazwa Roho Mtakatifu hata kabla ya kuzaliwa kwake. 16 Naye atawavuta Wayahudi wengi warudi kwa Bwana, Mungu wao. 17 Yeye atamtangulia Bwana akiongozwa na Roho na nguvu ya nabii Eliya. Atawapatanisha akina baba na watoto wao. Atawarejesha waasi katika njia ya wenye haki na kuandaa watu wa Bwana kwa ajili ya kuja kwake.” 18 Zakaria akamwambia mal aika, “Jambo hilo linawezekanaje? Mimi ni mzee na mke wangu pia ana umri mkubwa!” 19 Malaika akamjibu, akamwambia, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu. Yeye ndiye aliyenituma kwako nikuambie habari hizi njema. 20 Sikiliza! Kwa sababu huku niamini, utakuwa bubu, hutaweza kusema mpaka maneno yangu yataka pothibitishwa wakati mtoto huyo atakapozaliwa.” 21 Wakati mambo haya yakitokea mle Hekaluni, watu waliokuwa nje wakimngojea Zakaria walikuwa wakishangaa kwa nini alikawia kutoka. 22 Hati maye alipotoka hakuweza kusema nao. Wakatambua ya kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Kwa kuwa alikuwa bubu, akawaashiria kwa mikono. 23 Muda wake wa zamu Hekaluni ulipomalizika, akarudi nyumbani kwake. 24 Kisha baada ya muda si mrefu, Elizabeti mkewe alipata mimba, naye akajificha kwa miezi mitano akisema: 25 “Bwana amekuwa mwema kwangu. Maana ameniondolea aibu yangu mbele za watu.”

Kuzaliwa Kwa Yesu Kwatabiriwa

26 Miezi sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alim tuma malaika Gabrieli aende katika mji wa Nazareti, ulioko Gali laya, 27 kwa msichana bikira aliyeitwa Mariamu. Yeye alikuwa ameposwa na mtu mmoja aliyeitwa Yusufu, wa ukoo wa Mfalme Daudi.

28 Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu, akamwambia: “Sal aamu, ewe binti uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”

29 Mariamu alifadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, maana ya salamu hizi ni nini. 30 Ndipo malaika akamwam bia, “Usiogope, Mariamu, Mungu amependezwa nawe. 31 Sikiliza, utapata mimba, nawe utazaa mtoto wa kiume; na utamwita jina lake Yesu. 32 Mtoto huyo atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Mfalme Daudi, baba yake. 33 Atatawala juu ya nyumba ya Yakobo daima; na ufalme wake hau takuwa na mwisho!”

34 Mariamu akamwuliza malaika, “Lakini, nitapataje mimba, na mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu ata kujilia na nguvu za Mungu zitakufunika kama kivuli, na kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu na ataitwa Mwana wa Mungu. 36 Tena, miezi sita iliyopita binamu yako Elizabeti, aliyeitwa tasa, amepata mimba ingawa ni mzee sana. 37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilo wezekana.”

38 Mariamu akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema.’ ’ Kisha malaika akaondoka.

Mariamu Aenda Kumtembelea Elizabeti

39 , 40 Baada ya siku chache, Mariamu aliharakisha kwenda mji mmoja katika milima ya Yudea. Akaingia nyumbani kwa Zakaria akamsalimu Elizabeti. 41 Naye aliposikia salaamu za Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake aliruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42 akasema kwa sauti kubwa: “Umebarikiwa wewe zaidi ya wanawake wengine wote, naye mtoto utakayemzaa amebari kiwa. 43 Sikustahili heshima hii ya kutembelewa na mama wa Bwana wangu! 44 Mara tu niliposikia salaamu zako, mtoto aliyeko tum boni mwangu aliruka kwa furaha. 45 Wewe umebarikiwa kwa kuwa uliamini kwamba Bwana atatimiza yale aliyokuambia.” 46 Mariamu akasema: “Namtukuza Bwana, 47 na roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu. 48 Kwa kuwa ameutambua unyonge wa mtumishi wake. Tangu sasa vizazi vyote wataniita niliyebarikiwa. 49 Kwa maana, yeye Mwenye Uwezo, amenitendea mambo ya ajabu! Jina lake ni taka tifu. 50 Rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwao wamchao. 51 Kwa mkono wake ametenda mambo makuu. Wenye kiburi mioyoni mwao amewatawanya. 52 Amewaangusha wafalme kutoka katika viti vyao vya enzi na kuwainua wanyonge. 53 Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri na matajiri amewafukuza mikono mitupu. 54 Amem saidia mtumishi wake Israeli, akiikumbuka rehema yake, 55 kama alivyowaahidi baba zetu Ibrahimu na uzao wake daima.” 56 Mar iamu akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyum bani kwake.

Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji

57 Ikawa siku za kujifungua kwake Elizabeti zilipotimia, alizaa mtoto wa kiume . 58 Habari zikawafikia majirani na jamaa jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu. Nao wakafurahi pamoja naye. 59 Mtoto alipokuwa na umri wa siku nane, watu wakaja kuhudhuria tohara yake. Wote wakataka wampe yule mtoto jina la Zakaria, yaani jina la baba yake. 60 Lakini mama yake akakataa na kusema, “La si hilo. Jina lake litakuwa Yohana.” 61 Wakamjibu, “Mbona hakuna mtu katika jamaa yako mwenye jina kama hilo?” 62 Basi wakaamua kumwuliza Zakaria kwa ishara kwamba yeye angependa mtoto aitwe nani. 63 Akaomba mahali pa kuandikia, naye akaandika: “Jina lake ni Yohana.” Watu wote wakastaajabu. 64 Papo hapo uwezo wa kusema ukamrudia Zakaria naye akaanza kumsifu Mungu. 65 Watu wote walioshuhudia jambo hili wakastaajabu mno, na habari hii ikaenea sehemu zote za wilaya ile ya Yudea. 66 Na kila aliyezisikia habari hizi aliwaza moyoni: “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.

Utabiri Wa Zakaria

67 Zakaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akata biri akisema: 68 “Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake ili awakomboe. 69 Naye ametusimamishia nguvu ya wokovu katika ukoo wa Daudi mtumishi wake; 70 kama alivy oahidi kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani: 71 kwamba atatuokoa na maadui zetu na kututoa kutoka katika mikono ya wote watuchukiao. 72 Aliahidi ataonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka agano lake takatifu 73 aliloagana na baba yetu Ibrahimu: 74 kutuokoa kutoka katika mikono ya adui zetu na kutuwezesha kumtumikia pasipo woga, 75 katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote. 76 Na wewe mwanangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu, kwa kuwa utamtangulia Bwana na kumwandalia njia; 77 na kuwafahamisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao, 78 kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu. Nuru ya jua itatujia kutoka mbinguni na 79 kuwaangazia wote waishio katika giza na katika uvuli wa mauti na kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.” 80 Yule mtoto akakua na kuko maa kiroho; akaishi nyikani hadi alipoanza kuwahubiria Waisraeli hadharani.