Yesu Awaonya Na Kuwafariji Wanafunzi

12 Wakati huo, maelfu ya watu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu alizungumza na wanafunzi wake kwanza, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao.

“Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.

“Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi. Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: mwogopeni yule ambaye baada ya kumwua mtu ana mamlaka ya kumtupa motoni. Naam: huyo, mwogopeni! Mnajua kwamba mbayuwayu watano huuzwa kwa bei ndogo sana. Lakini Mungu anamjali kila mmoja wao. Mungu anafahamu hata idadi ya nywele zilizoko katika vichwa vyenu. Kwa hiyo msiogope: ninyi mna thamani zaidi kuliko mbayuwayu wengi. “Ninawaambia, kila atakayenikiri mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkiri mbele ya malaika wa Mungu. Lakini kila anayenikana mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkana mbele ya malaika wa Mungu. 10 Na kila atakayesema neno baya kunihusu mimi Mwana wa Adamu atasamehewa. Lakini mtu anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. 11 “Na watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu mtakavyojitetea au mtakavyosema: 12 kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”

Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”

13 Na mtu mmoja katika umati akasema, “Bwana, mwambie ndugu yangu anigawie urithi aliotuachia baba yetu.” 14 Yesu akamwam bia, Rafiki, ni nani aliyenifanya mimi niwe hakimu wenu au mga wanyaji wa urithi wenu?” 15 Ndipo akawaambia, “Jihadharini na jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana uhai wa mtu hautokani na wingi wa mali aliyo nayo.”

16 Kisha akawaambia mfano, “Shamba la tajiri mmoja lilizaa sana. 17 Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Maana sina mahali pa kuweka mavuno yangu.’ 18 Kisha akasema, ‘Nitafanya hivi: nitabomoa maghala yangu na kujenga maghala makubwa zaidi na huko nitaweka mavuno yangu yote na vitu vyangu. 19 Na nitasema moy oni, ‘Hakika nina bahati! Ninayo mali ya kunitosha kwa miaka mingi. Sasa nitapumzika: nile, ninywe na kustarehe.’ 20 Lakini Mungu akamwambia, ‘Mjinga wewe! Usiku huu huu utakufa! Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea vitakuwa vya nani?’ 21 Hivi ndivyo itakavy okuwa kwa mtu ye yote anayehangaika kujikusanyia utajiri duniani lakini si tajiri mbinguni kwa Mungu.”

22 Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Kwa hiyo ninawaambia, msihangaikie maisha yenu, kwamba mtakula nini; au miili yenu kwamba mtavaa nini. 23 Uhai ni zaidi ya chakula; na mwili ni zaidi ya mavazi. 24 Chukueni mfano wa kunguru! Wao hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala po pote pa kuweka nafaka, lakini Mungu anawalisha. Ninyi ni bora zaidi kuliko ndege! 25 Na ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha anaweza kujiongezea urefu wa maisha yake hata kwa saa moja? 26 Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo; kwa nini basi mhangaikie hayo mengine? 27 Yata zameni maua yanavyostawi: hayafanyi kazi, wala kujitengenezea nguo; lakini ninawaambia, hata Sulemani katika ufahari wake wote, hakuwahi kuvishwa vizuri kama ua mojawapo! 28 Ikiwa Mungu huyav isha hivi majani ambayo leo yapo shambani na kesho yanachomwa moto; ataachaje kuwavisha ninyi hata zaidi? Mbona mna imani ndogo! 29 Wala msihangaike mtakula nini au mtakunywa nini. Msiwe na wasiwasi juu ya haya. 30 Watu wasiomjua Mungu huhan gaika sana juu ya vitu hivi. Lakini Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnavihitaji. 31 Basi, tafuteni Ufalme wa Mungu; na hivyo vyote atawapatia.”

32 “Ninyi kundi dogo, msiogope kwa maana Mungu amependa mtawale naye katika ufalme wake. 33 Uzeni mali zenu muwape mas kini; ili mjipatie mikoba isiyochakaa, na kujiwekea hazina mbin guni ambapo mwizi hafiki wala nondo haharibu. 34 Kwa maana unapoiweka akiba yako ndipo na moyo wako utakapokuwa.”

Kukesha

35 “Muwe tayari mkiwa mmevaa, na taa zenu zikiwaka. 36 Muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka haru sini, ili atakapokuja na kugonga mlango wamfungulie mara moja. 37 Itakuwa ni heri kwa wale watumishi ambao bwana wao akija ata wakuta wanamngoja. Nawaambieni kweli, atajiandaa na kuwaketisha karamuni awahudumie. 38 Itakuwa ni furaha kubwa kwao ikiwa ata wakuta tayari hata kama atakuja usiku wa manane au alfajiri.

39 Fahamuni kwamba kama mwenye nyumba angalijua ni saa ngapi mwizi atakuja, angalijiandaa asiiachie nyumba yake ivunjwe. 40 Kwa hiyo, ninyi pia mkae tayari, kwa maana mimi Mwana wa Adamu nita kuja saa ambayo hamnitegemei.”

Mtumishi Mwaminifu Na Asiye mwaminifu

41 Ndipo Petro akamwambia, “Bwana, mfano huu unatuambia sisi peke yetu au watu wote?” 42 Yesu akamwambia, “Ni yupi wakili mwaminifu na mwenye busara? Ni yule ambaye bwana wake atamfanya mtawala juu ya nyumba yake yote naye awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa. 43 Itakuwa ni furaha kwa mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 44 Ninawahakikishia kwamba atampa mamlaka juu ya vyote alivyo navyo. 45 Lakini kwa mfano, kama yule mtumishi atawaza moyoni mwake, ‘Bwana wangu anachelewa kurudi,’ halafu aanze kuwa piga wale watumishi wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa, 46 bwana wake atarudi siku ambayo hakumtazamia, na saa asiyoijua. Huyo bwana wake atamwadhibu vikali pamoja na wote wasiotii. 47 Na mtumishi ambaye anafahamu mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, pia ataad hibiwa vikali. 48 Lakini mtumishi ambaye hafahamu anachotakiwa kufanya na akafanya kitu kinachostahili adhabu, atapata adhabu ndogo. Mungu atatarajia vingi kutoka kwa mtu aliyepewa vipawa vingi; na mtu aliyekabidhiwa vingi zaidi, atadaiwa zaidi pia.”

49 “Nimekuja kuleta moto duniani! Laiti kama dunia inge kuwa tayari imeshawaka! 50 Lakini kuna ubatizo ambao lazima niu pokee na dhiki yangu ni kuu mpaka ubatizo huo utakapokamilika.

51 “Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambieni sivyo; nimekuja kuleta mafarakano. 52 Kuanzia sasa, katika nyumba ya watu watano kutakuwa na mgawanyiko: watatu wakipingana na wawili, na wawili wakipingana na watatu. 53 Baba atapingana na mwanae na mwana atapingana na babaye; mama atapingana na bin tiye na binti atapingana na mamaye; mama mkwe atapingana na mke wa mwanae ambaye naye atapingana na mama mkwe wake.”

Kutambua majira

54 Kisha Yesu akawaambia watu, “Mkiona wingu likitokea mag haribi, mara moja mnasema, ‘Mvua hiyo inakuja!’ na inakuwa hivyo. 55 Na mnapouona upepo wa kusi ukivuma, mnasema, ‘Kutakuwa na joto!’ Na linakuwepo. 56 Enyi wanafiki! Mnaweza kutambua dalili za hali ya hewa; kwa nini basi hamtambui maana ya mambo yanayoto kea sasa? 57 Kwa nini hamuamui lililo haki kutenda? 58 Kama mtu akikushtaki mahakamani, jitahidi sana kupatana na mshtaki wako wakati mkiwa mnaenda mahakamani, ili asikufikishe mbele ya hakimu, na hakimu akakukabidhi kwa polisi, na polisi wakakutia gerezani. 59 Nakuhakikishia kwamba, hutatoka huko gerezani mpaka umelipa faini yote.”