A A A A A
Bible Book List

Luka 22 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

22 Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ili kuwa imekaribia. Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu kwa siri kwa sababu waliwaogopa watu.

Shetani akamwingia Yuda aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili. Yuda akaenda kwa makuhani wakuu na wakubwa wa walinzi wa Hekalu akawaeleza jinsi ambavyo angeweza kumsaliti Yesu. Wakafurahi na wakaahidi kumlipa fedha. Naye akaridhika, akaanza kutafuta nafasi nzuri ya kumsaliti Yesu kwa siri. Maandalizi Ya Chakula Cha Pasaka

Ikafika siku ya Mikate isiyotiwa Chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.” Wakam wuliza, “Tukaandae wapi?” 10 Akawajibu, “Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka kwenye nyumba atakayoingia, 11 kisha mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu anauliza, kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka? 12 Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani ambacho kina fanicha zote. Fanyeni maandalizi humo.”

13 Wakaenda wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaam bia. Kwa hiyo wakaandaa chakula cha Pasaka.

14 Wakati ulipofika Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 15 Kisha akawaambia “Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16 Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.” 17 Akapokea kikombe cha divai akashukuru, akasema, “Chukueni mnywe wote. 18 Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.”

19 Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.” 20 Vivyo hivyo baada ya kula, aka chukua kile kikombe cha divai akasema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu. 21 Lakini huyo atakayenisaliti amekaa nasi hapa mezani kama rafiki. 22 Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama ilivyokusudiwa na Mungu, lakini ole wake huyo mtu atakayenisaliti.” 23 Wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao angefanya kitu kama hicho.

Ubishi Kuhusu Ukubwa

24 Pia ukazuka ubishi kati ya wanafunzi kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa kati yao. 25 Yesu akawaambia, “Wafalme wa dunia huwatawala watu wao kwa mabavu na wenye mam laka huitwa ‘Wafadhili.’ 26 Ninyi msifanye hivyo. Aliye mkubwa wenu awe kama ndiye mdogo kabisa; na kiongozi wenu awe kama mtum ishi. 27 Kwani mkubwa ni nani? Yule aketiye mezani au yule anayemhudumia? Bila shaka ni yule aliyekaa mezani. Lakini mimi niko pamoja nanyi kama mtumishi wenu.

28 “Ninyi mmekuwa pamoja nami katika majaribu yangu: 29 na kama Baba yangu alivyonipa mamlaka ya kutawala; mimi nami nina wapa ninyi mamlaka hayo hayo. 30 Mtakula na kunywa katika karamu ya Ufalme wangu na kukaa katika viti vya enzi mkitawala makabila kumi na mawili ya Israeli.”

Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana

31 Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, shetani ameomba ruhusa kwa Mungu awapepete ninyi kama ngano. 32 Lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipotee. Na utakaponirudia mimi, uwatie moyo ndugu zako.”

33 Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda nawe gerezani na hata kufa.” 34 Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika leo usiku, utakana mara tatu kwamba hunijui.”

Kujiandaa Wakati Wa Hatari

35 Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma mwende bila mfuko, wala mkoba wala viatu, mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu, “La.” 36 Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko au mkoba auchukue. Asiye na upanga, auze koti lake anunue upanga. 37 Kwa sababu, nawambieni, yale Maandiko yaliyosema kwamba ‘Alihesabiwa pamoja na wahalifu’ yananihusu mimi na hayana budi kutimizwa. Naam, yale yaliyoandikwa kunihusu mimi yanatimia.” 38 Wakamwambia, “Bwana, tazama hapa kuna mapanga mawili.” Akawajibu, “Inatosha!. Yesu Asali Kwenye Mlima Wa Mizeituni

39 Ndipo Yesu akaondoka kuelekea kwenye mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, na wanafunzi wake wakamfuata. 40 Alipofika huko akawaambia wanafunzi, “Ombeni kwamba msiingie katika majaribu.” 41 Akaenda mbali kidogo nao, kama umbali anaoweza mtu kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 42 akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kwa mapenzi yangu, bali mapenzi yako yafanyike.” [ 43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44 Na alipokuwa katika uchungu mkubwa, akaomba kwa bidii zaidi na jasho lake likawa kama matone ya damu ikidondoka ardhini.] 45 Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wamechoka kwa huzuni. 46 Akawauliza, “Mbona mnalala? Amkeni muombe ili msiingie katika majaribu.”

Yesu Akamatwa

47 Wakati Yesu alipokuwa bado anazungumza, pakatokea kundi la watu likiongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wana funzi kumi na wawili. Akamsogelea Yesu ili ambusu. 48 Lakini Yesu akamwuliza, “Yuda! Unanisaliti mimi Mwana wa Adamu kwa busu?” 49 Wafuasi wa Yesu walipoona yanayotokea, wakasema, “Bwana, tutumie mapanga yetu?” 50 Na mmoja wao akampiga mtum ishi wa kuhani mkuu kwa panga, akamkata sikio la kulia. 51 Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa sikio la yule mtu, akamponya. 52 Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu na wakuu wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mme kuja na mapanga na marungu, kana kwamba mimi ni jambazi? 53 Kila siku nilikuwa pamoja nanyi lakini hamkunikamata. Lakini wakati huu, ambapo mtawala wa giza anafanya kazi, ndiyo saa yenu.”

Petro Amkana Yesu

54 Wakamkamata Yesu, wakamchukua wakaenda naye nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro akawafuata kwa mbali. 55 Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, na Petro akaketi na wale waliokuwa wakiota moto. 56 Msichana mmoja mfanyakazi akamwona Petro ameketi karibu na moto. Akamwangalia kwa makini, kisha akasema, “Huyu mtu pia ali kuwa pamoja na Yesu!” 57 Lakini Petro akakana akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” 58 Baadaye kidogo mtu mwingine akamwona Petro, akasema, “Wewe pia ni mmoja wao.” Petro akajibu, “Bwana, mimi si mmoja wao!” 59 Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akasisitiza, “Kwa hakika huyu mtu alikuwa na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.” 60 Petro akajibu, “Mimi sijui unalosema!” Na wakati huo huo, akiwa bado anazun gumza, jogoo akawika. 61 Yesu akageuka akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka yale maneno ambayo Bwana alimwambia, “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” 62 Akaenda nje, akalia kwa uchungu . Yesu Achekwa Na Kupigwa

63 Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64 Wakamfunga kitambaa usoni kisha wakasema, “Hebu nabii tuambie! Ni nani amekupiga?” 65 Wakamwambia maneno mengi ya kumtukana. Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza

66 Kulipokucha, Baraza la wazee wa Wayahudi, makuhani wakuu na walimu wa sheria wakakutana. Yesu akaletwa mbele yao. 67 Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, tuambie.” Yesu akawa jibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini, 68 na nikiwauliza swali, hamtanijibu. 69 Lakini hivi karibuni, mimi Mwana wa Adamu nita kaa upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi.” 70 Wote wakasema, “Ndio kusema wewe ndiye Mwana wa Mungu?” Akawajibu, “Ninyi ndio mmesema kwamba Mimi ndiye.” 71 Kisha wakasema, “Kwa nini tutafute ushahidi zaidi? Sisi wenyewe tumesikia maneno aliy osema.” Yesu Apelekwa Kwa Pilato

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica

  Back

1 of 1

You'll get this book and many others when you join Bible Gateway Plus. Learn more

Viewing of
Cross references
Footnotes