Add parallel Print Page Options

Je, Masihi ni Mwana wa Daudi?

(Mt 22:41-46; Lk 20:41-44)

35 Yesu alipokuwa akifundisha katika mabaraza ya Hekalu, alisema, “Inawezekana vipi walimu wa Sheria kusema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 36 Daudi mwenyewe kwa kupitia Roho Mtakatifu alisema,

‘Bwana Mungu alimwambia Bwana Mfalme wangu:
Keti karibu nami upande wangu wa kuume,
    nami nitawaweka adui zako chini ya udhibiti wako.’[a](A)

37 Daudi anamwita Masihi ‘Bwana’. Itakuwaje tena Kristo awe yote Bwana na pia mwana wa Daudi?”

Hapo lilikuwepo kundi kubwa la watu liliokuwa likimsikiliza kwa furaha.

Read full chapter

Footnotes

  1. 12:36 chini ya udhibiti wako Mafundisho ya Yesu katika Lk 10:25-37 yanaonesha kwa uwazi kuwa hii ni pamoja na yeyote mwenye uhitaji.