Yesu Afufuka Kutoka Kwa Wafu

16 Sabato ilipomalizika, Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake Yakobo na Salome walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu. Asubuhi na mapema, siku ya Jumapili, walikwenda kaburini jua likiwa linaanza kuchomoza. Njiani wakawa wanaulizana, “Ni nani atatuondolea lile jiwe kwenye mlango wa kaburi?” Lakini walipotazama, wakaona jiwe lile, ambalo lilikuwa kubwa sana, limekwisha ondolewa.

Walipoingia kaburini, walimwona kijana amekaa upande wa kulia akiwa amevaa vazi jeupe. Wakashtuka. Yule mtu akawaambia, “Msishtuke. Mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulubiwa. Amefufuka! Hayuko hapa! Tazameni mahali alipokuwa amelazwa.

Lakini nendeni mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, kwamba anatangulia kwenda Galilaya na huko mtamwona, kama alivyowaam bia.” Wale wanawake wakiwa wanashangaa na kutetemeka kwa hofu, wakatoka pale kaburini mbio! Hawakumweleza mtu ye yote jambo lo lote kwa maana walikuwa wanaogopa.

Read full chapter