Yesu akaendelea kuwaambia, ‘ ‘Ninawahakikishia kuwa wapo watu hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”

Yesu Ageuka Sura

Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana akawapeleka juu ya mlima mrefu ambapo walikuwa faraghani, peke yao. Na huko, wakiwa wanamtazama, Yesu akageuka sura. Mavazi yake yakametameta kwa weupe, yakang’aa, yakawa meupe kuliko ambavyo dobi ye yote duniani angaliweza kuyang’aarisha. Musa na Eliya wakawatokea nao walikuwa wakizungumza na Yesu.

Petro akamwambia Yesu , “Mwalimu, ni vizuri kwamba sisi tuko hapa. Tutengeneze vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Musa na kingine cha Eliya.” Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana.

Ndipo pakatokea wingu, likawafunika, na sauti kutoka katika wingu hilo ikasema, “Huyu ni mwanangu nimpendaye, msikilizeni yeye.” Mara walipotazama huku na huku hawakuona mtu mwingine tena isipokuwa Yesu.

Walipokuwa wakiteremka mlimani, Yesu akawakataza wasim wambie mtu ye yote mambo waliyoona, mpaka yeye Mwana wa Mungu atakapofufuka kutoka kwa wafu. 10 Wakatii agizo hilo, lakini wakawa wanajadiliana kati yao maana ya ‘Kufufuka kutoka kwa wafu.’ 11 Wakamwuliza, “Kwa nini walimu wa sheria husema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza kabla mambo haya hayajatokea?’ ’ 12 Yesu akawajibu, “Ni kweli, Eliya anakuja kwanza kusawazisha mambo yote. Hata hivyo, mbona imeandikwa kwamba Mimi, Mwana wa Adamu ni lazima niteseke sana na kudharauliwa? 13 Lakini nina waambia, Eliya amekwisha kuja na wamemtendea walivyopenda, kama Maandiko yasemavyo juu yake.”

Yesu Amponya Mvulana Mwenye Pepo

14 Walipowafikia wale wanafunzi wengine, waliwakuta wame zungukwa na umati mkubwa wa watu na baadhi ya walimu wa sheria wakibishana nao. 15 Mara wale watu walipomwona Yesu, walistaaj abu sana, wakamkimbilia, wakamsalimu. 16 Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nini nao?”

17 Mtu mmoja katika ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nimemleta kwako mtoto wangu wa kiume kwa maana amepagawa na pepo ambaye amemfanya kuwa bubu. 18 Kila mara pepo huyo amwingiapo mwanangu, humwangusha chini na kumfanya atokwe povu mdomoni na kusaga meno, kisha mwili wake hukauka. Nimewaomba wanafunzi wako wamtoe pepo huyo, lakini hawakuweza.”

19 Yesu akawaambia, “Ninyi kizazi kisicho na imani! Nita kuwa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni huyo mtoto kwangu!” 20 Wakamleta. Yule pepo alipomwona Yesu, alimtia yule mvulana kifafa, akaanguka chini akajiviringisha viringisha huku akitokwa na povu mdomoni. 21 Yesu akamwuliza baba yake, “Mwanao amekuwa na hali hii tangu lini?” Akamjibu, “Tangu utoto wake. 22 Na mara nyingi huyo pepo amemwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kuangamiza maisha yake. Lakini kama wewe unaweza kufanya cho chote, tafadhali tuonee huruma, utusaidie.” 23 Yesu akasema, “Kama unaweza! Kila kitu kinawezekana kwa mtu mwenye imani.” 24 Ndipo yule baba akasema kwa sauti, “Ninaamini. Nisaidie niweze kuamini zaidi!” 25 Naye Yesu ali poona umati wa watu unazidi kusongana kuja hapo walipokuwa, akam kemea yule pepo mchafu akisema, “Wewe pepo bubu na kiziwi, naku amuru umtoke, usimwingie tena!” 26 Yule pepo akapiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu kisha akatoka. Yule mvulana alionekana kama amekufa; kwa hiyo watu wengi wakasema, “Amekufa.” 27 Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua, naye akasimama.

28 Walipokwisha kuingia ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza wakiwa peke yao, “Mbona sisi hatukuweza kumtoa huyo pepo?” 29 Yesu akawajibu, “Pepo wa aina hii hawezi kutoka isi pokuwa kwa maombi.”

Yesu Azungumzia Tena Kifo Chake

30 Wakaondoka mahali hapo, wakapitia Galilaya. Yesu haku taka mtu ye yote afahamu walipokuwa 31 kwa maana alikuwa anawa fundisha wanafunzi wake. Alikuwa akiwaambia, “Mimi Mwana wa Adamu nitasalitiwa mikononi mwa watu ambao wataniua, lakini siku ya tatu baada ya kuuawa, nitafufuka.” 32 Lakini wao hawakuelewa alichokuwa akisema na waliogopa kumwuliza.

Mabishano Kuhusu Aliye Mkuu

33 Basi wakafika Kapernaumu na baada ya kuingia nyumbani akawauliza, “Mlikuwa mnabishana nini njiani?” 34 Lakini hawa kumjibu, kwa sababu njiani walikuwa wakibishana kuhusu nani kati yao alikuwa mkuu zaidi.

35 Akaketi chini, akawaita wote kumi na wawili akawaambia: “Mtu anayetaka kuwa kiongozi hana budi kuwa wa chini kuliko wote na kuwa mtumishi wa wote.” 36 Kisha akamchukua mtoto mdogo akamweka mbele yao, akamkumbatia akawaambia, 37 “Mtu ye yote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo, ananikaribisha mimi. Na ye yote anayenikaribisha mimi anamkaribisha Baba yangu ali yenituma.”

Kutumia Jina La Yesu

38 Yohana akamwambia, “Mwalimu, tumemwona mtu akitoa pepo kwa jina lako tukamzuia kwa sababu yeye si mmoja wetu.” 39 Yesu akasema, “Msimzuie, ye yote atendaye miujiza kwa jina langu kwani hawezi kunigeuka mara moja na kunisema vibaya. 40 Kwa maana ye yote ambaye si adui yetu yuko upande wetu. 41 Ninawahakikishia kwamba mtu atakayewapa japo maji ya kunywa kwa kuwa ninyi ni wafuasi wangu, atapewa tuzo.”

Kuhusu Kuwakwaza Wengine

42 “Na mtu atakayesababisha mmojawapo wa hawa wadogo waniaminio kupoteza imani yake, ingalikuwa nafuu kama mtu huyo angefungiwa jiwe kubwa shingoni akatupwa ziwani. 43 Kama mkono wako ukikusababisha utende dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja kuliko kuwa na mikono miwili ukaingia katika moto usiozimika. [ 44 Huko funza hawafi wala moto hauzimiki.] 45 Na kama mguu wako ukikusababisha utende dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kiwete kuliko kuwa na miguu miwili ukaingia katika moto usiozimika. [ 46 Huko funza hawafi wala moto hauzimiki.] 47 Na kama jicho lako litakusababisha utende dhambi, ling’oe. Ni afadhali kuwa chongo ukaingia katika Ufalme wa Mungu kuliko kuwa na macho mawili ukatupwa Jehena. 48 Huko funza hawafi wala moto hauzimiki. 49 Wote watatiwa chumvi kwa moto. 50 “Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake utafanya nini ili iweze kukolea tena? Muwe na chumvi ndani yenu. Muishi pamoja kwa amani.”

Naye Yesu aliwaambia, “Ninawaambia Ukweli: baadhi yenu mnaosimama hapa mtauona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu kabla ya kufa kwenu.”

Yesu Aonekana Akiwa na Musa na Eliya

(Mt 17:1-13; Lk 9:28-36)

Baada ya siku sita, Yesu akamchukua Petro, Yakobo na Yohana na kuwaongoza hadi mlima mrefu wakiwa peke yao tu. Na mwonekano wa Yesu ulibadilika mbele yao. Huko Yesu akabadilika sura nyingine akiwa mbele yao. Mavazi yake yakiwa na mng'ao, na meupe kabisa kuliko mtu anavyoweza kufua nguo kwa sabuni na kuitakatisha. Huko Eliya na Musa pia wakawatokea, na Yesu alizungumza na manabii hao wawili.

Petro akafungua kinywa chake na kumwambia Yesu, “Mwalimu, ni vyema tupo hapa. Tufanye basi vibanda vitatu; moja kwa ajili yako, moja kwa ajili ya Musa na moja kwa ajili ya Eliya.” Petro aliyasema haya kwa sababu hakujua aseme nini, kwa sababu yeye na wenzake walikuwa wamepata hofu.

Ndipo wingu likaja na kuwafunika wote kwa kivuli chake. Na sauti ikatoka mawinguni, ikisema, “Huyu ni mwanangu mpendwa. Msikilizeni yeye.”

Ndipo ghafula walipokuwa wakiangalia huku na huko, hawakuona mtu yeyote akiwa pamoja nao isipokuwa Yesu peke yake.

Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Yesu akawaamuru wasimwambie mtu yeyote kile walichokiona mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka katika wafu.

10 Hivyo hawakuwaeleza wengine juu ya jambo lile bali walijadiliana miongoni mwao wenyewe juu ya maana ya “kufufuka kutoka kwa wafu.” 11 Wakamwuliza Yesu, “kwa nini walimu wa sheria wanasema Eliya lazima aje kwanza?”

12 Yesu akawaambia, “Ndiyo, Eliya atakuja kwanza[a] kuja kuyaweka mambo yote sawa kama jinsi yalivyokuwa hapo mwanzo. Lakini kwa nini imeandikwa juu ya Mwana wa Adamu[b] ya kwamba itampasa kuteswa na kudhalilishwa? 13 Lakini ninawaambia, Eliya amekuja,[c] na walimtendea kila kitu walichotaka, kama vile ilivyoandikwa[d] kuhusu yeye.”

Yesu Amweka Huru Mvulana Kutoka Pepo Mchafu

(Mt 17:14-20; Lk 9:37-43a)

14 Wakati Yesu, Petro, Yakobo, na Yohana walipowafikia wanafunzi wengine, waliliona kundi kubwa la watu lililowazunguka na wakawaona walimu wa Sheria wakibishana nao. 15 Mara tu watu wote walipomwona Yesu, walishangazwa, na wakakimbia kwenda kumsalimia.

16 Akawauliza, “Mnabishana nao kitu gani?”

17 Na mtu mmoja kundini alimjibu, “Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako ili umponye. Yeye amefungwa na pepo mbaya anayemfanya asiweze kuzungumza. 18 Na kila mara anapomshambulia humtupa chini ardhini. Naye hutokwa mapovu mdomoni na kusaga meno yake, huku akiwa mkakamavu. Nami niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze kutoka ndani yake, lakini hawakuweza.”

19 Kisha Yesu akajibu na kuwaambia, “ninyi kizazi kisichoamini, kwa muda gani niwe pamoja nanyi? Kwa muda gani nitapaswa kuchukuliana nanyi? Mleteni huyo mvulana kwangu.”

20 Wakamleta yule mvulana kwake. Na yule pepo alipomwona Yesu, kwa ghafula akamtingisha yule mvulana ambaye alianguka chini kwenye udongo, akivingirika na kutokwa povu mdomoni.

21 Yesu akamwuliza babaye, “Kwa muda gani amekuwa katika hali hii?”

Yule babaye akajibu akisema, “amekuwa katika hali hii tangu utoto. 22 Mara nyingi anamtupa katika moto ama katika maji ili kumwua. Lakini ikiwa unaweza kufanya kitu chochote, uwe na huruma na utusaidie.”

23 Yesu akamwambia, “Una maana gani kusema ‘ikiwa unaweza’? Kila kitu kinawezekana kwake yeye anayeamini.”

24 Mara, babaye yule mvulana alilia kwa sauti kubwa na kusema, “Naamini! Nisaidie kutokuamini kwangu.”

25 Yesu alipoona lile kundi likizidi kuwa kubwa, alimkemea yule pepo mchafu na kumwambia, “Wewe pepo uliyemfanya mvulana huyu asiweze kusikia na asiweze kusema, nakuamuru, utoke ndani yake, na usimwingie tena!”

26 Na pepo yule alilia kwa sauti, akamtupa yule mvulana chini katika mishituko ya kutisha, kisha akatoka, naye akawa kama mtu aliyekufa, kiasi kwamba watu wengi wakadhani ya kuwa amekufa. 27 Lakini Yesu akamshika yule mvulana mikononi, na kumwinua naye akasimama.

28 Baada ya Yesu kuingia nyumbani, wanafunzi wake walimwuuliza wakiwa peke yao, “Kwa nini sisi hatukuweza kumfukuza pepo yule?”

29 Naye akawaambia, “Aina hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa maombi.”[e]

Yesu Azungumza Kuhusu Kifo Chake

(Mt 17:22-23; Lk 9:43-45)

30 Wakaondoka mahali pale na kusafiri kupitia Galilaya. Yesu hakutaka mtu yeyote kujua walikuwa huko, 31 alitaka kuwafundisha wanafunzi wake peke yake. Na Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kuwekwa mikononi mwa watu wengine, nao watamwua. Kisha siku tatu baada ya kuuawa atafufuka.” 32 Lakini hawakuuelewa usemi huu, na walikuwa wanaogopa kumuuliza zaidi.

Nani ni Mkuu Zaidi?

(Mt 18:1-5; Lk 9:46-48)

33 Kisha wakaja Kapernaumu. Na Yesu alipokuwa ndani ya nyumba aliwauliza, “Je, mlikuwa mnajidiliana nini njiani?” 34 Lakini wao walinyamaza kimya, kwa sababu njiani walikuwa wamebishana juu ya nani kati yao alikuwa ni mkuu zaidi.

35 Hivyo Yesu aliketi chini, akawaita wale kumi na mbili, na akawaambia, “Ikiwa yupo mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza, inapasa basi awe wa mwisho kuliko wote na mtumishi wa wote.”

36 Akamchukua mtoto mdogo mikononi mwake na kumsimamisha mbele yao. Akimkumbatia mtoto huyo, Yesu alisema, 37 “Yeyote atakayemkaribisha mtoto mdogo kama huyu hapa kwa sababu ya jina langu basi ananikaribisha na mimi pia. Yeyote anayenikubali mimi hanikubali mimi tu bali anamkubali pia yeye aliyenituma.”

Yeyote Ambaye Hayuko Kinyume Chetu Yuko Pamoja Nasi

(Lk 9:49-50)

38 Yohana akamwambia Yesu, “Mwalimu tulimwona mtu akifukuza pepo kwa jina lako. Nasi tulijaribu kumzuia, kwa sababu hakuwa mmoja wetu.”

39 Lakini Yesu akawaambia, “Msimzuie, kwa sababu hakuna atendaye miujiza kwa jina langu kisha mara baada ya hilo aseme maneno mabaya juu yangu. 40 Yeye ambaye hapingani na sisi basi yuko pamoja na sisi. 41 Yeyote anayewapa ninyi kikombe cha maji kwa sababu ninyi ni wake Kristo.[f] Hakika ninawaambia ukweli kwamba, hatapoteza thawabu yake.

Yesu Aonya Kuhusu Chanzo cha Dhambi

(Mt 18:6-9; Lk 17:1-2)

42 Yeyote anayemsababisha mmoja wa hawa walio wadogo ambao wananiamini mimi kujikwaa na kuanguka, itakuwa bora kwake ikiwa atatupwa baharini huku amefungwa jiwe la kusagia shingoni mwake. 43 Ikiwa mkono wako unakusababisha ufanye dhambi, ukate. Ni bora kwako kuingia katika uzima wa milele ukiwa na mkono mmoja kuliko kuwa na mikono miwili na kuenda Jehanamu, ambako kuna moto usiozimika. 44 [g] 45 Na ikiwa mguu wako utakusababisha ufanye dhambi, ukate. Ni bora kwako kuingia katika uzima wa milele ukiwa mlemavu kuliko kuwa na miguu miwili na kutupwa Jehanamu. 46 [h] 47 Na kama jicho lako litakusababisha ufanye dhambi, liondoe. Ni bora uingie katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja kuliko kuwa nayo macho mawili na kutupwa Jehanamu, 48 ambapo waliomo watatafunwa na funza wasiokufa na kuchomwa na moto usiozimika kamwe.(A)

49 Kwa kuwa kila mmoja atatiwa chumvi kwa moto.[i]

50 Chumvi ni njema. Lakini ikiwa chumvi itaharibika, utawezaje kuifanya chumvi tena? Muwe na chumvi miongoni mwenu na muishi kwa amani ninyi kwa ninyi.”

Footnotes

  1. 9:12 atakuja kwanza Ama atatangulia.
  2. 9:12 Mwana wa Adamu Jina lingine alilojitambulisha Yesu.
  3. 9:13 Eliya amekuja Habari hii inamhusu Yohana Mbatizaji.
  4. 9:13 kama vile ilivyoandikwa Hii inahusu maandiko ya Agano la Kale.
  5. 9:29 maombi Nakala zingine za Kiyunani zina “maombi na kufunga”.
  6. 9:41 Kristo Mpakwa mafuta au masihi, aliyechaguliwa na Mungu.
  7. 9:44 Nakala zingine za Kiyunani zinaongeza mstari wa 44, ambao ni sawa na mstari 48.
  8. 9:46 Nakala zingine za Kiyunani zinaongeza mstari wa 46, ambao ni sawa na mstari 48.
  9. 9:49 Nakala zingine za Kiyunani zinaongeza, “Kila dhabihu itatiwa chumvi.” Katika Agano la Kale chumvi ilinyunyiziwa kwenye dhabihu. Mstari huu unaweza kuwa na maana kuwa wanafunzi wa Yesu watajaribiwa kwa mateso na kwamba wanapaswa kujitoa wenyewe kwa Mungu kama dhabihu.