Yohana Mbatizaji Akatwa Kichwa

14 Wakati huo, mfalme Herode alisikia habari za Yesu; akawaam bia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji, amefufuka kutoka kwa wafu; ndio sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumweka gere zani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, kaka yake. Kisa che nyewe ni kwamba Yohana alikuwa amemwambia Herode kuwa, “Si halali kwako kumwoa huyo mwanamke.” Herode alitaka sana kumwua Yohana lakini akaogopa watu kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. Lakini siku ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu walioalikwa akamfurahisha sana Herode. Naye akaahidi kwa kiapo kumpa huyo binti lo lote atakaloomba. Kwa kushawishiwa na mama yake, huyo binti akasema, “Nipatie kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” Mfalme akajuta; lakini kwa ajili ya kile kiapo alichoapa mbele ya wageni, aliamuru kwamba ombi lake litekelezwe. 10 Akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani, 11 na kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.

12 Wanafunzi wa Yohana wakaja, wakauchukua mwili wake wakau zika. Kisha wakaenda, wakamwambia Yesu.

Yesu Alisha Zaidi Ya Watu Elfu Tano

13 Yesu aliposikia haya, aliondoka kwa mashua akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu wal ipata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu, kutoka mij ini. 14 Yesu alipofika kando ya bahari aliona umati mkubwa wa watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.

15 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walimfuata wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na siku imekwisha. Waage watu waondoke ili wakajinunulie chakula vijijini.” 16 Yesu akasema, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.” 17 Wakamjibu, “Hapa tuna mikate mitano na samaki wawili tu.” 18 Akawaambia, “Leteni hapa.” 19 Akaagiza wale watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akaibariki. Akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 20 Wote wakala, wakatosheka. Na wanafunzi wake wakakusanya vipande vipande vilivyosalia, waka jaza vikapu kumi na viwili. 21 Idadi ya watu waliokula, bila kuhesabu wanawake na watoto, ilikuwa kama wanaume elfu tano.

Yesu Atembea Juu Ya Maji

22 Baadaye Yesu akawaambia wanafunzi wake watangulie kwe nye mashua waende ng’ambo ya pili ya ziwa, wakati yeye anawaaga wale watu. 23 Baada ya kuwaaga, akaenda mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa hapo peke yake. 24 Wakati huo ile mashua ilikwisha fika mbali, ikisukwa sukwa na mawimbi kwa sababu upepo ulikuwa mkali.

25 Ilipokaribia alfajiri, Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26 Lakini wanafunzi wake walipom wona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu. Wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga mayowe kwa hofu. 27 Lakini mara moja Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo. Ni mimi; msiogope.”

28 Petro akamjibu, “Bwana, kama ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.” 29 Yesu akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka katika mashua, akatembea juu ya maji akimfuata Yesu. 30 Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”

31 Mara Yesu akanyoosha mkono wake, akamshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini ulikuwa na shaka?” 32 Na walipoingia katika mashua, upepo ukakoma. 33 Wote waliokuwamo katika mashua wakamwabudu wakisema, “Hakika, wewe ni Mwana wa

Yesu Awaponya Wagonjwa Genesareti

34 Walipokwisha kuvuka, wakafika Genesareti. 35 Watu wa eneo lile walipomtambua Yesu, walipeleka habari sehemu zote za jirani na watu wakawaleta wagonjwa wote kwake 36 wakamsihi awaru husu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa, waliponywa.

Herode Adhani Yesu ndiye Yohana Mbatizaji

(Mk 6:14-29; Lk 9:7-9)

14 Katika wakati huo, Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia ambacho watu walikuwa wanasema kuhusu Yesu. Hivyo akawaambia watumishi wake, “Nadhani hakika mtu huyu ni Yohana Mbatizaji. Lazima amefufuka kutoka kwenye kifo, na ndiyo sababu anaweza kutenda miujiza hii.”

Kifo cha Yohana Mbatizaji

Kabla ya wakati huu, Herode alimkamata Yohana. Akamfunga kwa minyororo na kumweka gerezani. Alimkamata Yohana kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, kaka yake Herode. Yohana alikuwa amemwambia, “Si sahihi kwako kumwoa Herodia.” Herode alitaka kumwua, lakini aliwaogopa watu. Waliamini kuwa Yohana alikuwa nabii.

Siku ya kuzaliwa Herode, bintiye Herodia[a] alicheza mbele yake na kundi lake. Herode alifurahishwa naye sana. Hivyo aliapa kuwa atampa kitu chochote atakachotaka. Herodia alimshawishi binti yake kitu cha kuomba. Hivyo bintiye akamwambia Herode, “Nipe hapa kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sahani kubwa.”

Mfalme Herode alihuzunika sana. Lakini alikuwa ameahidi kumpa binti kitu chochote alichotaka. Na watu waliokuwa wakila pamoja na Herode walikuwa wamesikia ahadi yake. Hivyo Herode aliamuru kitu ambacho alikuwa ameomba apatiwe. 10 Akawatuma wanaume gerezani, ambako walikikata kichwa cha Yohana. 11 Na watu wakakileta kichwa cha Yohana kwenye sahani kubwa na kumpa yule msichana. Kisha yeye akakipeleka kichwa kwa mama yake, Herodia. 12 Wafuasi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wa Yohana na kuuzika. Kisha wakaenda na kumwambia Yesu kilichotokea.

Yesu Awalisha Watu Zaidi ya 5,000

(Mk 6:30-44; Lk 9:10-17; Yh 6:1-14)

13 Yesu aliposikia kilichotokea kwa Yohana, aliondoka kwa kutumia mtumbwi. Alikwenda peke yake mpaka mahali ambapo hakuna aliyekuwa akiishi. Lakini watu walisikia kuwa Yesu alikuwa ameondoka. Hivyo waliondoka katika miji na kumfuata. Walikwenda mahali alikokwenda kupitia nchi kavu. 14 Yesu alipotoka katika mtumbwi, aliwaona watu wengi. Akawahurumia, na kuwaponya waliokuwa wagonjwa.

15 Baadaye mchana huo, wafuasi walimwendea Yesu na kusema, “Hakuna anayeishi katika eneo hili. Na tayari muda umepita, hivyo waage watu ili waende katika miji na kujinunulia chakula.”

16 Yesu akasema, “Watu hawahitaji kuondoka. Wapeni ninyi chakula wale.”

17 Wafuasi wakajibu, “Lakini tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”

18 Yesu akasema, “Leteni kwangu mikate na samaki.” 19 Kisha akawaambia watu waketi chini kwenye nyasi. Akaichukua mikate mitano na samaki wawili. Akatazama mbinguni na akamshukuru Mungu kwa ajili ya chakula. Kisha akaivunja mikate katika vipande, akawapa wafuasi wake nao wakawapa watu chakula. 20 Kila mmoja alikula mpaka akashiba. Walipomaliza kula, wafuasi walijaza vikapu kumi na mbili vya vipande vilivyosalia. 21 Walikuwepo wanaume 5,000, pamoja na wanawake na watoto waliokula.

Yesu Atembea Juu ya Maji

(Mk 6:45-52; Yh 6:16-21)

22 Mara baada ya hili Yesu akawaambia wafuasi wake wapande kwenye mtumbwi. Akawaambia waende upande mwingine wa ziwa. Aliwaambia angekuja baadaye, alikaa pale ili kuwaaga watu. 23 Baada ya Yesu kuwaaga watu, alikwenda kwenye vilima peke yake kuomba. Ikawa jioni na alikuwa pale peke yake. 24 Wakati huu mtumbwi ilikuwa mbali kutoka pwani. Kwa kuwa upepo ulikuwa unavuma kinyume na mtumbwi, mtumbwi ulikuwa unapata msukosuko kwa sababu ya mawimbi.

25 Kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi, wafuasi wa Yesu walikuwa bado ndani ya mtumbwi. Yesu akaenda kwao akitembea juu ya maji. 26 Iliwatisha walipomwona anatembea juu ya maji. Wakapiga kelele kwa woga “Ni mzuka!”

27 Lakini haraka Yesu akawaambia, “Msihofu! Ni mimi! Msiogope.”

28 Petro akasema, “Bwana, ikiwa hakika ni wewe, niambie nije kwako juu ya maji.”

29 Yesu akasema, “Njoo, Petro.”

Kisha Petro akauacha mtumbwi na kutembea juu ya maji kumwelekea Yesu. 30 Lakini Petro alipokuwa anatembea juu ya maji, aliyaona mawimbi na upepo. Aliogopa na kuanza kuzama katika maji. Akapiga kelele, “Bwana, niokoe!”

31 Haraka Yesu akamshika Petro kwa mkono wake. Akasema, “Imani yako ni ndogo. Kwa nini ulisita?”

32 Baada ya Petro na Yesu kuingia kwenye mtumbwi, upepo ukakoma. 33 Kisha wafuasi wakamwabudu Yesu na kusema, “Hakika wewe ni Mwana wa Mungu.”

Yesu Awaponya Watu Wengi Wagonjwa

(Mk 6:53-56)

34 Baada ya kuvuka ziwa, wakafika pwani katika eneo la Genesareti. 35 Baadhi ya watu pale wakamwona Yesu na wakamtambua kuwa ni nani. Hivyo wakatuma ujumbe kwa watu wengine katika eneo lote kuwa Yesu amekuja. Watu wakawaleta wagonjwa wao wote kwake. 36 Walimsihi Yesu awaruhusu waguse tu upindo wa vazi lake ili waponywe. Na wagonjwa wote waliogusa vazi lake waliponywa.

Footnotes

  1. 14:6 Herodia Josephus, Mwana historia wa Kiyahudi anamwita binti huyu Salome.