Paulo Aenda Korintho

18 Baada ya haya, Paulo aliondoka Athene akaenda Korintho. Huko alimpata Myahudi mmoja jina lake Akila, mzaliwa wa Ponto, ambaye alikuwa amewasili karibuni kutoka Italia pamoja na mkewe Prisila, kwa sababu mfalme Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Rumi. Paulo akaenda kuwaona. Akakaa nao na kufanya kazi na Akila kwa sababu wote wawili walikuwa mafundi wa kutengeneza mahema. Kila siku ya sabato Paulo alikwenda katika sinagogi akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki waamini. Sila na Timotheo walipofika kutoka Makedonia walimkuta akihubiri na kuwashuhudia Wayahudi na Wagiriki, kuwa Yesu ndiye Kristo. Wal ipombishia na kumtukana alikung’uta mavazi yake akawaambia, “Mimi sina lawama, mkipotea , lawama iko juu yenu wenyewe. Tangu sasa nitawahubiria mataifa neno la Mungu.” Kwa hiyo Paulo akaondoka akaenda kwenye nyumba ya mtu anayeitwa Titio Yusto ali yekuwa mcha Mungu. Nyumba yake ilikuwa karibu sana na sinagogi. Kiongozi wa hilo sinagogi aliyeitwa Krispo akamwamini Bwana pamoja na jamaa yake; na Wakorintho wengi waliomsikia Paulo wakaamini na kubatizwa. Usiku mmoja Bwana akazungumza na Paulo katika ndoto akamwambia, “Usiogope, endelea kuhubiri wala usi kate tamaa. 10 Kwa maana mimi niko pamoja nawe, wala hakuna mtu atakayeweza kukushambulia na kukudhuru; kwa kuwa kuna watu wengi walio wangu katika mji huu.” 11 Kwa hiyo Paulo akakaa Korintho kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, akiwafundisha waamini neno la Mungu. 12 Lakini wakati Galio alipofanywa kuwa Liwali wa Akaya, Wayahudi waliungana kumshambulia Paulo, Wakamkamata na kumpeleka Mahakamani. 13 Wakamshitaki wakisema, “Mtu huyu anawashawishi watu wamwabudu Mungu kinyume cha sheria zetu.” 14 Paulo alipo taka kujitetea Galio akawaambia Wayahudi, “Kama mashtaka yenu yalihusu makosa ambayo mtu huyu amefanya au kama yangehusu ujam bazi, ningewasikiliza. 15 Lakini kwa kuwa kesi hii inahusu maneno na majina yaliyo katika sheria zenu, itawabidi muiamue wenyewe. Nakataa kabisa kujihusisha na jambo hili.” 16 Akawafu kuza kutoka mahakamani. 17 Wakamkamata Sosthene, kiongozi wa sinagogi, wakampiga mbele ya mahakama. Wala Galio hakuingilia kati.

Paulo Arudi Antiokia

18 Baada ya haya Paulo alikaa huko Korintho kwa siku nyingi zaidi kisha akaagana na wale ndugu waamini akasafiri kwa meli kuelekea Siria akiongozana na Prisila na Akila. Walipofika Kenk rea Paulo alinyoa nywele zake kwa maana alikuwa ameweka nadhiri. 19 Walipofika Efeso Paulo aliwaacha Prisila na Akila, akaenda katika sinagogi akawa akijadiliana na Wayahudi. 20 Walipomwambia akae nao kwa muda mrefu zaidi alikataa, 21 lakini alipokuwa aki waaga aliwaambia, “Nitarudi kama Mungu akipenda.” Akasafiri kwa meli kutoka Efeso. 22 Alipofika Kaisaria alikwenda kuwasalimu ndugu katika kanisa kisha akaelekea Antiokia. 23 Alikaa Antiokia kwa muda, na baadaye aliondoka akatembelea makanisa huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha waamini wote.

Apolo Ahubiri Efeso Na Korintho

24 Basi Myahudi mmoja jina lake Apolo, mwenyeji wa Aleksan dria alikuja Efeso. Yeye alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuhu biri na pia aliyajua Maandiko barabara. 25 Alikuwa amefundishwa njia ya Bwana naye akiwa amejaa moto wa kiroho alifundisha kwa usahihi juu ya Yesu. Lakini ujuzi wake uliishia kwenye ubatizo wa Yohana. 26 Apolo alihubiri kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi. Lakini Prisila na Akila walipomsikiliza walimchukua nyumbani kwao wakamfundisha njia ya Mungu kwa ukamilifu zaidi. 27 Na alipoamua kwenda Akaya, ndugu wa Efeso walimtia moyo wakampa na barua ya kumtambulisha kwa ndugu wa huko. Alipofika aliwasaidia sana watu wengi ambao kwa neema ya Mungu walikuwa wameamini; 28 maana kwa uwezo mkubwa aliwakanusha hadharani Wayahudi waliokuwa wakipinga Habari Njema kwa kuwaonyesha kutoka katika Maandiko kuwa Yesu ndiye Kristo.

Paulo Akiwa Korintho

18 Baadaye, Paulo aliondoka Athene na kwenda katika mji wa Korintho. Akiwa huko alikutana na Myahudi aliyeitwa Akila, aliyezaliwa katika jimbo la Ponto. Lakini yeye na mke wake aliyeitwa Prisila, walikuwa tu ndiyo wamehamia Korintho kutoka Italia. Waliondoka Italia kwa sababu Kaisari Klaudio alikuwa ametoa amri Wayahudi wote waondoke Rumi. Paulo alikwenda kuwatembelea Akila na Prisila. Walikuwa watengenezaji wa mahema,[a] kama alivyokuwa Paulo, hivyo alikaa na kufanya kazi pamoja nao.

Kila siku ya Sabato Paulo alikwenda kwenye sinagogi na kuzungumza na Wayahudi na Wayunani, akijaribu kuwashawishi wamwamini Yesu. Lakini baada ya Sila na Timotheo kufika kutoka Makedonia, Paulo alitumia muda wake wote kuuhubiri ujumbe wa Mungu kwa Wayahudi, akiwaeleza kuwa Yesu ndiye Masihi. Lakini walimpinga Paulo na wakaanza kumtukana. Hivyo Paulo akakung'uta mavumbi kutoka kwenye nguo zake.[b] Akawaambia, “Msipookolewa, itakuwa makosa yenu ninyi wenyewe! Nimefanya yote ninayoweza kufanya. Baada ya hili nitawaendea watu wasio Wayahudi tu.”

Paulo aliondoka katika sinagogi na kuhamia nyumbani kwa Tito Yusto, mtu aliyekuwa anamwabudu Mungu wa Kweli, nyumba yake ilikuwa jirani na sinagogi. Krispo aliyekuwa kiongozi wa sinagogi lile, pamoja na watu wote waliokuwa wanaishi nyumbani mwake walimwamini Bwana Yesu. Watu wengi katika mji wa Korintho walimsikiliza Paulo, wakaamini na wakabatizwa.

Wakati wa usiku, Paulo aliona maono. Bwana alimwambia, “Usiogope, na usiache kuzungumza na watu. 10 Niko pamoja nawe, na hakuna atakayeweza kukudhuru. Kuna watu wangu wengi katika mji huu.” 11 Paulo alikaa pale kwa mwaka mmoja na nusu akiwafundisha watu ujumbe wa Mungu.

Paulo Afikishwa Mbele ya Galio

12 Galio alipokuwa gavana wa Akaya, baadhi ya Wayahudi walikusanyika wakawa kinyume cha Paulo. Wakampeleka mahakamani. 13 Wakamwambia Galio, “Mtu huyu anawafundisha watu kumwabudu Mungu kwa namna ambavyo ni kunyume na sheria yetu!”

14 Paulo alikuwa tayari kuzungumza, lakini Galio aliwaambia Wayahudi, “Ningewasikiliza ikiwa malalamiko yenu yangehusu dhuluma au kosa jingine. 15 Lakini yanahusu maneno na majina tu, mabishano yanayohusu sheria zenu wenyewe. Ni lazima mtatue tatizo hili ninyi wenyewe. Sitaki kuwa mwamuzi wa jambo hili.” 16 Hivyo Galio akawafanya waondoke mahakamani.

17 Kisha wote kwa pamoja wakamkamata Sosthenesi, kiongozi wa sinagogi. Wakampiga mbele ya mahakama. Lakini Galio hakulijali hili pia.

Paulo Arudi Antiokia

18 Paulo alikaa na waamini kwa siku nyingi. Kisha aliondoka na kusafiri majini kwenda Shamu. Prisila na Akila walikuwa pamoja naye pia. Walipofika Kenkrea Paulo akanyoa nywele zake kwa sababu aliweka nadhiri[c] kwa Mungu. 19 Kisha walikwenda Efeso, ambako Paulo aliwaacha Prisila na Akila. Paulo alipokuwa Efeso alikwenda katika sinagogi na kuzungumza na Wayahudi. 20 Walimwomba akae kwa muda mrefu lakini alikataa. 21 Aliwaacha na kusema, “Nitarudi tena kwenu ikiwa Mungu atataka nirudi.” Na hivyo akaabili kwenda Efeso.

22 Alipofika Kaisaria, alikwenda Yerusalemu na kulitembelea kanisa pale. Baada ya hapo alikwenda Antiokia. 23 Alikaa Antiokia kwa muda kisha akaondoka akipita katika nchi za Galatia na Frigia. Alisafiri kutoka mji mmoja hadi mji mwingine katika mikoa hii, akiwasaidia wafuasi wa Yesu kuimarika katika imani yao.

Apolo Akiwa Efeso na Korintho

24 Myahudi aliyeitwa Apolo alikuja Efeso. Alizaliwa katika mji wa Iskanderia, alikuwa msomi aliyeyajua Maandiko vizuri. 25 Alikuwa amefundishwa kuhusu Bwana na daima alifurahia[d] kuwaeleza watu kuhusu Yesu. Alichofundisha kilikuwa sahihi, lakini ubatizo alioufahamu ni ubatizo aliofundisha Yohana. 26 Apolo alianza kuzungumza kwa ujasiri katika sinagogi. Prisila na Akila walipomsikia akizungumza, walimchukua wakaenda naye nyumbani mwao kisha wakamsaidia kuielewa njia ya Mungu vizuri zaidi.

27 Apolo alitaka kwenda Akaya. Hivyo waamini wa Efeso wakamsaidia. Waliwaandikia barua wafuasi wa Bwana waliokuwa Akaya wakiwaomba wampokee Apolo. Alipofika pale, alikuwa msaada mkubwa kwa wale waliomwamini Yesu kwa sababu ya neema ya Mungu. 28 Alibishana kwa ujasiri na Wayahudi mbele ya watu wote. Alithibitisha kwa uwazi kuwa wayahudi walikuwa wanakosea. Alitumia Maandiko kuonesha kuwa Yesu ndiye Masihi.

Footnotes

  1. 18:3 watengenezaji wa mahema Au pengine “watengenezaji wa sehemu za kufanyia matukio”.
  2. 18:6 akakung'uta … nguo zake Ishara ya onyo au tahadhari kuonesha kuwa Paulo alikuwa amemaliza kuzungumza na Wayahudi haya.
  3. 18:18 akanyoa nywele … nadhiri Ilikuwa desturi ya Wayahudi kunyoa nywele wakati wa kuweka nadhiri. Ina maana ya kiapo cha kujiweka wakfu ama kufanya huduma maalumu kwa Mungu. Tazama Mnazareti katika Orodha ya Maneno.
  4. 18:25 alifurahia Au “Alikuwa katika mito wa Roho Mtakatifu.”