Petro Na Yohana Wakamatwa

Walipokuwa bado wanasema na watu, makuhani, mkuu wa walinzi wa Hekalu na Masadukayo waliwajia wakiwa wamekasirika kwa sababu Petro na Yohana walikuwa wakiwafundisha watu kwamba kufu fuka kwa Yesu kunadhihirisha kwamba wafu watafufuka. Wakawaka mata wakawaweka jela mpaka kesho yake kwa maana ilikuwa jioni. Lakini wengi wa wale waliosikia mahubiri yao waliamini; idadi ya wanaume walioamini ilikuwa kama elfu tano.

Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria walikusanyika Yerusalemu. Walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa , Yohana, Aleksanda na ndugu zake Kuhani Mkuu. Wakawaleta wale mitume wawili katikati yao wakawauliza, “Ni kwa uwezo gani au mmetumia jina la nani kufanya jambo hili?” Petro, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu akajibu, “Waheshimiwa viongozi na wazee wa watu, kama mnatuhoji kuhusu mambo mema aliyotendewa kilema, na jinsi alivyoponywa, tungependa ninyi na watu wote wa 10 Israeli mfahamu kwamba, ni kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha lakini Mungu akam fufua kutoka kwa wafu, kwa uwezo wa Yesu, huyu mtu anasimama mbele yenu akiwa mzima kabisa. 11 Huyu Yesu ndiye ‘lile jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilikataa, ambalo limekuwa jiwe kuu la pembeni.’ 12 Wokovu unapatikana kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani ambalo wamepewa wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina hilo peke yake tunaweza kuokolewa!”

Ujasiri Wa Petro Na Yohana Washangaza Watu

13 Wale viongozi na wazee walipoona ujasiri wa Petro na Yohana na kufahamu ya kuwa walikuwa watu wa kawaida wasio na elimu walishangaa sana. Wakatambua kwamba hawa watu walikuwa na Yesu. 14 Lakini kwa kuwa walimwona yule kilema aliyeponywa ame simama nao hawakuweza kusema lo lote kupinga maneno yao. 15 Wakawaamuru watoke nje ya ule ukumbi. 16 Kisha wakaanza kuulizana, “Tuwafanye nini watu hawa? Hatuwezi kukanusha muujiza huu mkubwa walioufanya ambao ni dhahiri kwa kila mtu Yerusalemu. 17 Lakini tunaweza kuzuia jambo hili lisiendelee kuenezwa kwa watu kama tukiwakanya wasiseme tena na mtu ye yote kwa jina la Yesu.” 18 Kwa hiyo wakawaita tena ndani wakawaamuru wasiseme au kufundisha watu tena kwa jina la Yesu.

Bora Kumtii Mungu Kuliko Wanadamu

19 Ndipo Petro na Yohana wakawajibu, “Ninyi amueni wenyewe lililo bora kutenda mbele za Mungu: kuwatii ninyi au kumtii Mungu. 20 Lakini sisi hatuwezi kuacha kusema yale tuliyoyaona na kuyasikia.”

21 Wale viongozi wakawaonya tena kwa vitisho, kisha waka waacha waende. Hawakuona njia ya kuwaadhibu kwa kuwa waliwaogopa wale watu ambao walishuhudia ule muujiza uliotendeka, nao wali kuwa wakimsifu Mungu. 22 Na yule mtu aliyeponywa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka arobaini.

23 Mara Petro na Yohana walipoachiliwa, walirudi kwa waamini wenzao wakawaeleza waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee. 24 Waamini wote waliposikia maneno yao walimwomba Mungu kwa pamoja wakasema, “Wewe Bwana Mtukufu, uliyeumba mbingu na nchi na bahari na kila kiumbe kilichopo, 25 wewe ulitamka kwa njia ya Roho wako mtakatifu kupitia kwa baba yetu Daudi mtumishi wako, aliposema, ‘Mbona mataifa wanaghadhabika, na watu wanawaza mambo yasiyo na maana? 26 Wafalme wa dunia wamejiandaa na watawala wamekusanyika wampinge Bwana na Masihi wake.’ 27 Ndiyo sababu katika mji huu Herode na Pontio Pilato walikutana na Waisraeli wote na watu wa mataifa juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, 28 wakaamua kumfanyia yale yote ambayo wewe ulikuwa umekusudia tangu awali na kupanga kwa uweza wako yatendeke.

29 “Sasa Bwana, sikia vitisho vyao na utuwezeshe sisi wat umishi wako kuhubiri neno lako kwa ujasiri mkuu; 30 na unyooshe mkono wako ili tuweze kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miu jiza kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.” 31 Walipokwisha kusali, nyumba waliyokuwa wamekutania ikatikisika na wote wakaja zwa na Roho Mtakatifu, wakahubiri neno la Mungu kwa ujasiri. 32 Waamini wote walikuwa na nia moja na moyo mmoja, wala hakuna aliyeona mali aliyokuwa nayo kuwa yake, bali walishirikiana vitu vyote kwa pamoja. 33 Na kwa uwezo mkubwa mitume wakashuhudia kwa ujasiri habari za kufufuka kwa Bwana Yesu. Mungu akawapa wote neema kuu. 34 Wala hakuwepo mtu ye yote miongoni mwa waamini aliyepungukiwa na kitu kwa sababu wale waliokuwa na mashamba na nyumba waliuza vyote wakaleta fedha waliyopata 35 kwa wale mitume; kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake.

36 Ndivyo ilivyokuwa kwamba Yusufu ambaye mitume walimwita Barnaba, maana yake Mwana wa Faraja, wa ukoo wa Lawi kutoka kisiwa cha Kipro 37 aliuza shamba alilokuwa nalo akaleta fedha alizopata kwa wale mitume.

Mitume Mbele ya Baraza Kuu la Wayahudi

Petro na Yohana walipokuwa wanazungumza na watu, ghafla baadhi ya viongozi wa Kiyahudi waliwaendea. Walikuwepo baadhi ya makuhani, mkuu wa askari wanaolinda Hekalu na baadhi ya Masadukayo. Walikasirika kwa sababu ya mafundisho ambayo Petro na Yohana walikuwa wanawafundisha na kuwaambia watu kuhusu Yesu. Mitume walikuwa wanafundisha pia kwamba watu watafufuka kutoka kwa wafu. Waliwakamata Petro na Yohana. Kwa kuwa ilikuwa jioni tayari, waliwaweka gerezani usiku ule mpaka siku iliyofuata. Lakini watu wengi waliowasikia mitume waliamini walichosema. Na siku hiyo idadi ya watu katika kundi la waamini ikafikia watu 5,000.

Siku iliyofuata, watawala wa Kiyahudi, wazee na walimu wa sheria walikutana Yerusalemu. Kuhani mkuu Anasi alikuwepo. Kayafa, Yohana, Iskanda na jamaa wengine wa kuhani mkuu walikuwepo pia. Waliwasimamisha Petro na Yohana mbele ya watu wote. Wakawauliza maswali mengi, “Mliwezaje kumponya mlemavu wa miguu huyu? Mlitumia nguvu gani? Mmefanya hili kwa mamlaka ya nani?”

Ndipo Petro, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akawaambia, “Enyi watawala nanyi wazee wa watu, mnatuuliza leo ni nini tulifanya kumsaidia huyu mlemavu wa miguu? Mnatuuliza nini kilimponya? 10 Tunataka ninyi nyote na watu wote wa Israeli mtambue kuwa mtu huyu aliponywa na nguvu ya Yesu Kristo kutoka Nazareti. Mlimpigilia Yesu msalabani, lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Mtu huyu alikuwa mlemavu wa miguu, lakini sasa ni mzima. Anaweza kusimama hapa mbele zenu kwa sababu ya nguvu ya Yesu! 11 Yesu ndiye

‘Jiwe[a] ambalo ninyi wajenzi mlilikataa.
    Lakini jiwe hili limekuwa jiwe na msingi.’(A)

12 Yesu peke yake ndiye anayeweza kuokoa watu. Jina lake ndiyo nguvu pekee iliyotolewa kumwokoa mtu yeyote ulimwenguni. Ni lazima tuokoke kupitia yeye!”

13 Viongozi wa Kiyahudi walijua kuwa Petro na Yohana walikuwa watu wa kawaida wasio na elimu yo yote. Lakini walikuwa wanazungumza kwa ujasiri bila woga; viongozi walishangaa. Walitambua pia kuwa Petro na Yohana walikuwa pamoja na Yesu. 14 Walimwona aliyeponywa akiwa amesimama kwa miguu yake mwenyewe pembeni mwa mitume. Na hivyo walishindwa kuzungumza chochote kilicho kinyume na mitume.

15 Viongozi wa Kiyahudi wakawaambia mitume watoke nje ya chumba cha mkutano wa baraza. Kisha viongozi wakajadiliana wao wenyewe juu ya nini wanachopaswa kufanya. 16 Wakaulizana, “Tuwafanye nini watu hawa? Kila mtu katika Yerusalemu anajua kuhusu muujiza walioufanya kama ishara kutoka kwa Mungu. Ni dhahiri, hatuwezi kusema muujiza huo haukufanyika. 17 Lakini ni lazima tuwatishe ili wasiendelee kuwaambia watu kutumia jina lile.[b] Ili tatizo hili lisisambae miongoni mwa watu.”

18 Hivyo viongozi wa Kiyahudi wakawaita Petro na Yohana ndani tena. Wakawaambia wasiseme wala kufundisha kitu chochote kwa kutumia jina la Yesu. 19 Lakini Petro na Yohana wakawajibu, “Mnadhani kipi ni sahihi? Mungu angetaka nini? Je, tunapaswa kuwatii ninyi au tumtii Mungu? 20 Hatuwezi kukaa kimya. Ni lazima tuwaambie watu kuhusu yale tuliyoona na kusikia.”

21-22 Viongozi wa Kiyahudi hawakupata sababu za kuwaadhibu mitume, kwa sababu watu wote walikuwa wanamsifu Mungu kwa kile kilichotendeka. Muujiza huu ulikuwa ishara kutoka kwa Mungu. Mtu aliyeponywa alikuwa na miaka zaidi ya arobaini. Hivyo viongozi wa Kiyahudi wakawaonya mitume tena na kuwaacha waende wakiwa huru.

Petro na Yohana Warudi kwa Waamini

23 Petro na Yohana waliondoka kwenye mkutano wa viongozi wa Kiyahudi na kurudi kwa waamini wenzao. Wakalieleza kundi la waamini kila kitu walichoambiwa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 24 Waamini waliposikia hili, wote kwa pamoja wakamwomba Mungu wakiwa na nia moja. Wakasema, “Bwana wa wote, wewe ndiye uliyeumba mbingu, dunia, bahari na kila kitu ulimwenguni. 25 Baba yetu Daudi alikuwa mtumishi wako. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu aliandika maneno haya:

‘Kwa nini mataifa yanatenda kwa kiburi?
    Kwa nini watu wanapanga mipango isiyofaa kama hii?
26 Wafalme wa dunia hujiandaa kwa mapigano,
    na watawala hukusanyika pamoja kinyume na Bwana
    na kinyume na Masihi wake.’(B)

27 Ndicho hasa kilichotokea wakati Herode, Pontio Pilato, mataifa mengine na watu wa Israeli walipokusanyika pamoja hapa Yerusalemu wakawa kinyume na Yesu; Masihi, Mtumishi wako mtakatifu. 28 Watu hawa waliokusanyika pamoja kinyume na Yesu waliwezesha mpango wako kukamilika. Ilifanyika kwa sababu ya nguvu zako na matakwa yako. 29 Na sasa, Bwana, sikiliza wanayosema. Wanajaribu kututisha. Sisi ni watumishi wako. Tusaidie ili tuseme yale unayotaka tuseme bila kuogopa. 30 Tusaidie, ili tuwe jasiri kwa kutuonesha nguvu zako. Ponya Wagonjwa. Fanya ishara na maajabu kutokea kwa mamlaka[c] ya Yesu mtumishi wako mtakatifu.”

31 Baada ya waamini kuomba, mahali walipokuwa palitikisika. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, na wakaendelea kuhubiri Habari Njema bila woga.

Ushirika wa Waamini

32 Kundi lote la waamini waliungana katika kuwaza na katika mahitaji yao. Hakuna aliyesema vitu alivyokuwa navyo ni vyake peke yake. Badala yake walishirikiana kila kitu. 33 Kwa nguvu kuu mitume walifanya ijulikane kwa kila mmoja kwamba Bwana Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu. Na Mungu aliwabariki sana waamini wote. 34 Hakuna aliyepungukiwa kitu. Kila aliyemiliki shamba au nyumba aliuza na kuleta pesa alizopata, 35 na kuzikabidhi kwa mitume. Kisha kila mtu akapewa kiasi alichohitaji.

36 Mmoja wa waamini aliitwa Yusufu. Mitume walimwita Barnaba, jina linalomaanisha “Mtu anayewatia moyo wengine.” Alikuwa Mlawi mzaliwa wa Kipro. 37 Yusufu aliuza shamba alilomiliki. Akaleta pesa na kuwapa mitume.

Footnotes

  1. 4:11 Jiwe Alama kumaanisha Yesu.
  2. 4:17 jina lile Yaani, jina la Yesu. Viongozi wa Kiyahudi walikwepa kutamka jina lake. Tazama Lk 15:2 na Mdo 5:28.
  3. 4:30 mamlaka Kwa maana ya kawaida, “Katika jina la Yesu”.