Kuokoka Kwa Sauli

Wakati huu wote Sauli alikuwa bado anaendelea na vitisho vyake vya kuwaangamiza kabisa wanafunzi wa Bwana. Akaenda kwa Kuhani Mkuu, akamwomba ampe barua ya kumtambulisha kwa masina gogi ya huko Dameski, ili akiwapata wafuasi wa ile ‘Njia Basi katika safari yake, alipokuwa akikaribia Dameski, ghafla nuru kutoka mbinguni iliangaza kumzunguka! Akaanguka chini! Na aka sikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona unanitesa?” Sauli akajibu, “Ni nani wewe, Bwana?” Ile sauti ikasema, “Mimi ni Yesu ambaye unamtesa. Lakini sasa inuka uingie mjini nawe utaambiwa la kufanya.” Wale waliokuwa wakisafiri na Sauli wakasimama kwa mshangao, wala hawakuweza kusema neno kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. Sauli akainuka na alipojaribu kufungua macho, hakuweza kuona kitu. Basi wakamshika mkono wakamwongoza mpaka Dameski. Na kwa muda wa siku tatu akawa haoni kabisa, na hakula kitu wala kunywa cho chote.

10 Huko Dameski alikuwepo mfuasi mmoja jina lake Anania. Bwana akamwita Anania katika ndoto, “Anania! ” Akaitika, “Nipo hapa Bwana.” 11 Bwana akamwambia, “Amka uende barabara iitwayo Nyofu ukaulizie katika nyumba ya Yuda kuhusu mtu aitwaye Sauli wa Tarso. Yeye hivi sasa anaomba, na katika maono anamwona mtu 12 aitwaye Anania akija na kuweka mikono juu yake ili aweze kuona tena.” 13 Anania akajibu, “Bwana, nimesikia kutoka kwa watu wengi mambo ya kutisha ambayo mtu huyu anawatendea wataka tifu wako huko Yerusalemu. 14 Naye amekuja hapa Dameski akiwa na kibali kutoka kwa Kuhani Mkuu awakamate wote wanaotaja jina lako.” 15 Lakini Bwana akamwambia Anania, “Nenda, kwa maana nimemchagua awe mtumishi wangu wa kulitangaza jina langu kwa mataifa na wafalme na kwa wana wa Israeli; 16 nami nitamwonyesha atakavyoteseka sana kwa ajili ya jina langu .” 17 Anania akaenda, akaingia mle nyumbani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu yangu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea njiani ame nituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.” 18 Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka machoni mwa Sauli, akapata kuona tena. Akasimama, akabatizwa. 19 Kisha akala chak ula, akapata nguvu tena. Alikaa siku kadhaa pamoja na wanafunzi huko Dameski na 20 bila kukawia akaenda katika sinagogi akawash uhudia watu kwamba, “Yesu ni Mwana wa Mungu.”

Sauli Ahubiri Dameski

21 Watu wote waliomsikia Sauli walishangaa wakasema, “Huyu si yule mtu aliyekuwa akiwatesa watu waliotaja jina la Yesu huko Yerusalemu, na ambaye amekuja hapa kwa shabaha ya kuwakamata na kuwapeleka wakiwa wamefungwa kwa makuhani wakuu?” 22 Lakini Sauli alizidi kuhubiri kwa nguvu zaidi akathibitisha kabisa kwamba Yesu ndiye Kristo; hata Wayahudi walioishi Dameski hawa kuwa na lo lote la kupinga. 23 Baada ya siku nyingi kupita, Way ahudi walifanya mpango wa kumwua Sauli. 24 Lakini Sauli akapata habari za mpango huo. Wayahudi walikuwa wakilinda milango yote ya kutokea mjini, mchana na usiku ili akitoka wamwue. 25 Lakini wanafunzi wake wakamtoa nje ya mji usiku kwa kumpitisha mahali palipokuwa na nafasi katika ukuta wa mji, akiwa ndani ya kapu kubwa.

Sauli Atoa Ushuhuda Wake Yerusalemu

26 Sauli alipofika Yerusalemu alijaribu kujiunga na waamini lakini wao walimwogopa kwa maana hawakuamini ya kuwa kweli ali kuwa amemwamini Yesu. 27 Lakini Barnaba akamchukua Sauli akampeleka kwa wale mitume akawaeleza jinsi Sauli alivyokutana na Yesu njiani akienda Dameski na Yesu akasema naye. Pia akawaeleza jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski. 28 Kwa hiyo Sauli akakaa nao akishirikiana nao na aki hubiri wazi wazi kwa jina la Yesu kila mahali huko Yerusalemu.

29 Lakini alipowahubiria Wayahudi wenye asili ya Kigiriki na kubishana nao, wao waliamua kumwua. 30 Waamini wengine walipo pata habari hizi walimchukua hadi Kaisaria wakamsafirisha kwenda Tarso. 31 Ndipo kanisa katika Yudea yote, Galilaya na Samaria likawa na wakati wa amani. Kanisa likapata nguvu likienenda katika kicho cha Bwana; na kwa msaada wa Roho Mtakatifu, idadi yake ikazidi kuongezeka.

Petro Amponya Ainea

32 Petro alipokuwa akiwatembelea waamini sehemu mbalimbali alifika kwa watu wa Mungu walioishi huko Lida. 33 Akamkuta mtu mmoja aitwaye Ainea, ambaye alikuwa amepooza na kwa muda wa miaka minane alikuwa hajaondoka kitandani. 34 Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo anakuponya; inuka utandike kitanda chako.” Na mara Ainea akainuka. 35 Wakazi wote wa Lida na Sharoni wali pomwona Ainea akitembea walimgeukia Bwana.

Petro Amfufua Dorkasi

36 Huko Jopa kulikuwa na mwanafunzi mwanamke aliyeitwa Tabita au kwa lugha ya Kigiriki, Dorkasi, yaani paa. Huyu mama alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. 37 Hata hivyo aliugua akafa. Wakamwosha na kumlaza katika chumba cha ghorofani. 38 Kwa kuwa Jopa hapakuwa mbali sana na Lida, wanafunzi waliposikia kuwa Petro yuko Lida, waliwatuma wenzao wawili wakamwambie, “Tafadhali njoo huku pasipo kukawia.” 39 Kwa hiyo Petro akaharakisha akaenda nao Jopa. Alipowasili wakampeleka hadi kwenye chumba alipokuwa amelazwa marehemu Dor kasi. Wajane wengi walikuwa wamemzunguka marehemu wakilia na kuonyesha mavazi ambayo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa hai. 40 Petro akawatoa wote nje, kisha akapiga magoti akaomba; akaugeukia ule mwili akasema, “Tabita, Amka!” Dorkasi akafumbua macho na alipomwona Petro, akaketi. 41 Petro akamshika mkono akamsaidia kusimama. Ndipo alipowaita wale waamini na wajane aka wakabidhi Dorkasi akiwa hai. 42 Habari hizi zilienea sehemu zote za Jopa. Na watu wengi wakamwamini Bwana. 43 Petro akakaa Jopa kwa muda mrefu, akiishi na mtengenezaji ngozi mmoja aitwaye

Sauli Awa Mfuasi wa Yesu

Huko Yerusalemu Sauli aliendelea kuwatisha wafuasi wa Bwana, na hata kuwaambia kuwa angewaua. Alikwenda kwa kuhani mkuu, na kumwomba aandike barua kwenda kwenye masinagogi yaliyokuwa katika mji wa Dameski. Sauli alitaka kuhani mkuu ampe mamlaka ya kuwatafuta watu katika mji wa Dameski waliokuwa wafuasi wa Njia ya Bwana.[a] Ikiwa angewapata waamini huko, wanaume au wanawake, angewakamata na kuwaleta Yerusalemu.

Hivyo Sauli alikwenda Dameski. Alipoukaribia mji, ghafla mwanga mkali kutoka mbinguni ukaangaza kumzunguka. Akadondoka chini na akasikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli! Kwa nini unanitesa?”

Sauli akasema, “Wewe ni nani, Bwana?”

Sauti ikajibu, “Mimi ni Yesu, unayemtesa. Simama sasa na uingie mjini. Mtu mmoja huko atakueleza unachopaswa kufanya.”

Wanaume waliokuwa wanasafiri pamoja na Sauli walisimama pale kimya. Waliisikia sauti, lakini hawakumwona yeyote. Sauli alisimama kutoka chini na kufumbua macho yake, lakini hakuweza kuona. Hivyo wale aliokuwa nao wakamshika mkono na kumwongoza kuingia Dameski. Kwa siku tatu Sauli hakuweza kuona; hakula wala kunywa.

10 Alikuwepo mfuasi wa Yesu katika mji wa Dameski aliyeitwa Anania. Katika maono Bwana alimwita, “Anania!”

Anania alijibu, “Niko hapa, Bwana.”

11 Bwana akamwambia, “Amka na uende katika mtaa unaoitwa Mtaa Ulionyooka. Tafuta nyumba ya Yuda[b] na uliza kuhusu mtu anayeitwa Sauli anayetoka katika mji wa Tarso. Yuko katika nyumba hiyo sasa, anaomba. 12 Ameoneshwa katika maono kuwa mtu anayeitwa Anania anamwendea na kuweka mikono juu yake ili aweze kuona tena.”

13 Lakini Anania akajibu, “Bwana, watu wengi wameniambia kuhusu mtu huyu. Wameniambia kuhusu mambo mengi mabaya aliyowatendea watu wako watakatifu katika mji wa Yerusalemu. 14 Na sasa amekuja hapa Dameski. Viongozi wa makuhani wamempa mamlaka ya kuwakamata watu wote wanaokuamini wewe.”[c]

15 Lakini Bwana Yesu akamwambia Anania, “Nenda, nimemchagua Sauli kwa kazi maalumu. Ninataka ayahubiri mataifa mengine, watawala na watu wa Israeli kuhusu mimi. 16 Nitamwonyesha yote ambayo lazima atateseka kwa ajili yangu.”

17 Hivyo Anania aliondoka na kwenda nyumbani kwa Yuda. Akaweka mikono yake juu ya Sauli na kusema, “Sauli, ndugu yangu, Bwana Yesu amenituma. Ndiye uliyemwona barabarani wakati ukija hapa. Amenituma ili uweze kuona tena, pia ujazwe Roho Mtakatifu.” 18 Ghafla, vitu kama magamba ya samaki vikaanguka kutoka kwenye macho ya Sauli. Akaanza kuona tena! Kisha akasimama na kwenda kubatizwa. 19 Baada ya kula chakula, akaanza kujisikia kuwa na nguvu tena.

Sauli Aanza Kuhubiri Juu ya Yesu Kristo

Sauli alikaa pamoja na wafuasi wa Yesu katika mji wa Dameski kwa siku chache. 20 Baadaye alianza kwenda katika masinagogi na kuwahubiri watu kuhusu Yesu. Aliwaambia watu, “Yesu ni Mwana wa Mungu!”

21 Watu wote waliomsikia Sauli walishangaa. Wakaulizana, “Je, huyu si yule aliyekuwa anajaribu kuwaangamiza watu wanaomwamini Yesu[d] katika mji wa Yerusalemu? Na hakuja hapa ili awakamate wafuasi wa Yesu na kuwarudisha kwa viongozi wa makuhani?”

22 Lakini Sauli aliendelea kuwa nguvu katika kuthibitisha kwamba Yesu ndiye Masihi. Uthibitisho wake ulikuwa na nguvu kiasi kwamba Wayahudi walioishi Dameski hawakuweza kubishana naye.

Sauli Awatoroka Wayahudi

23 Baada ya siku nyingi kupita, baadhi ya Wayahudi waliweka mpango wa kumwua Sauli. 24 Waliyalinda malango ya mji usiku na mchana. Walitaka kumwua Sauli, lakini aliambiwa kuhusu mpango wao. 25 Usiku mmoja baadhi ya wafuasi ambao Sauli aliwafundisha walimsaidia kuondoka mjini. Walimweka katika kikapu, wakamtoa kwa kumshusha kupitia kwenye tundu lililokuwa kwenye ukuta wa mji.

Sauli Katika Mji wa Yerusalemu

26 Kisha Sauli alikwenda Yerusalemu. Akajaribu kujiunga na kundi la wafuasi, lakini wote walimwogopa. Hawakuamini kuwa naye amekuwa mfuasi wa Yesu. 27 Lakini Barnaba alimkubali Sauli, akamchukua na kumpeleka kwa mitume. Akawaeleza namna ambavyo Sauli alimwona Bwana akiwa njiani na namna ambavyo Bwana aliongea naye. Kisha akawaambia namna ambavyo Sauli amehubiri kwa ujasiri kuhusu Yesu katika mji wa Dameski.

28 Sauli alikaa na wafuasi na kwenda kila mahali katika mji wa Yerusalemu akihubiri kwa ujasiri kwa ajili ya Bwana. 29 Kila mara alibishana na Wayahudi waliokuwa waliozungumza Kiyunani,[e] ambao walianza kutengeneza mpango wa kumwua. 30 Waamini walipoujua mpango huu, walimchukua Sauli mpaka Kaisaria, na kutoka huko walimsafirisha mpaka katika mji wa Tarso.

31 Kanisa katika Uyahudi yote, Galilaya na Samaria likawa na wakati wa amani. Na kwa msaada wa Roho Mtakatifu, vikundi hivi vya waamini vikawa na nguvu katika imani na kuonesha utii kwa ajili ya Bwana kwa namna walivyoishi. Hivyo kanisa kila mahali liliongezeka kwa idadi.

Petro akiwa Lida na Yafa

32 Petro alikuwa akisafiri katika sehemu zote za Uyahudi, Galilaya na Samaria, na akasimama kuwatembelea waamini[f] walioishi Lida. 33 Huko alikutana na mtu aliyeitwa Ainea, ambaye alikuwa amepooza na hakuweza kutoka kitandani kwa miaka nane. 34 Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo amekuponya. Simama na kiweke kitanda chako vizuri!” Ainea alisimama saa ile ile. 35 Watu wote walioishi Lida na tambarare ya Sharoni walimwona, na wakaamua kumfuata Bwana.

36 Katika mji wa Yafa kulikuwa na mfuasi wa Yesu aliyeitwa Tabitha, Jina lake kwa Kiyunani lilikuwa Dorkasi.[g] Daima aliwatendea watu mambo mema na kuwapa pesa wale wenye mahitaji. 37 Petro alipokuwa Lida, Tabitha aliugua na kufa. Waliusafisha mwili wake na kuuweka chumbani ghorofani. 38 Wafuasi waliokuwa Yafa wakasikia kuwa Petro yuko Lida, mji ambao haukuwa mbali na Yafa. Hivyo waliwatuma watu wawili, waliomsihi Petro wakisema, “Tafadhali njoo kwetu haraka!”

39 Petro alijiandaa na kwenda pamoja nao. Alipofika, walimchukua na kumpeleka kwenye chumba ghorofani. Wajane wote walisimama wakamzunguka huku wakilia na wakamwonesha mavazi ambayo Tabitha alitengeneza alipokuwa hai. 40 Petro akawatoa watu wote chumbani. Akapiga magoti na kuomba. Kisha akaugeukia mwili wa Tabitha na kusema, “Tabitha! Simama.” Akafumbua macho yake. Alipomwona Petro akaketi. 41 Petro akamshika mkono na akamsaidia kusimama. Ndipo akawaita waamini na wajane chumbani. Akawaonyesha Tabitha; akiwa hai!

42 Watu kila mahali katika mji wa Yafa wakatambua kuhusu hili, na wengi wakamwamini Bwana. 43 Petro alikaa Yafa siku nyingi nyumbani kwa mtu mmoja aitwaye Simoni, aliyekuwa mtengenezaji wa ngozi.

Footnotes

  1. 9:2 Njia ya Bwana Ni maneno yaliyotumika ili kuainisha tabia na mafundisho ya Yesu.
  2. 9:11 Yuda Huyu si mmoja wa mitume aliyeitwa Yuda.
  3. 9:14 wanaokuamini wewe Kwa maana ya kawaida, “wanaoliitia jina lako”, ikimaanisha kumwamini Yesu kwa kumwabudu au kumwomba Yeye.
  4. 9:21 wanaomwamini Yesu Kwa maana ya kawaida, “wanaoliitia jina lake”.
  5. 9:29 Kiyunani Au “Kigiriki”.
  6. 9:32 waamini Kwa maana ya kawaida, “watakatifu”, jina kwa ajili ya watu waliomwamini Yesu. Pia katika mstari wa 41.
  7. 9:36 Dorkasi Maana yake ni mnyama aitwaye paa.