Mafundisho Sahihi

Lakini wewe, mafundisho yako ni lazima yawe sahihi. Wafundishe wazee kuwa na kiasi, watulivu, wenye busara na tha biti katika imani, upendo na subira. Hali kadhalika akina mama wazee wawe na mwenendo wa unyenyekevu. Wasiwe wachonganishi, wala wasiwe watumwa wa pombe; bali waonyeshe mfano mwema. Hivyo wawafundishe akina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto wao na kuwa wenye kiasi na safi, wakitumia wakati wao kushughulika nyumbani mwao. Wawe wema na watii kwa waume zao, ili neno la Mungu lisije likadharauliwa kwa ajili yao. Vile vile uwahimize vijana kuwa na kiasi. Katika mambo yote wewe mwenyewe uwe kielelezo cha matendo mema. Uonyeshe usa hihi na uthabiti katika mafundisho yako. Maneno yako yawe na kina na mantiki safi, mtu asiweze kuyatoa kasoro na hata yule anayepinga aaibike kwa kukosa lo lote baya la kusema juu yetu.

Wahimize watumwa kuwatii mabwana wao na kuwapendeza katika mambo yote; wasijibishane nao 10 wala kuwaibia, bali watumwa waonyeshe kuwa wanaweza kuaminika kabisa ili katika kila hali mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu yapate sifa njema.

11 Kwa maana neema ya Mungu iletayo wokovu imedhihirishwa kwa watu wote. 12 Neema hiyo inatufundisha kukataa uovu na tamaa za dhambi, tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya kumcha Mungu, katika ulimwengu huu. Wakati huo huo 13 tukingojea tumaini letu lenye baraka - kuja kwa utukufu wa Mungu wetu Mkuu na Mwokozi wetu, Yesu Kristo. 14 Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe katika uasi wote, na kutufanya tuwe safi kwa ajili yake; na tuwe watu wake kabisa, ambao wana juhudi katika kutenda mema.

15 Fundisha mambo haya; himiza na kemea kwa mamlaka yote. Mtu ye yote asikudharau.

Kufuata Mafundisho ya Kweli

Lakini wewe Tito daima uwaambie waaminio mambo yanayokubaliana na mafundisho ya kweli na yenye uzima. Wanaume wazee wanapaswa kuwa na kiasi na kufanya mambo yenye kuleta heshima. Wanapaswa kuwa na busara katika maisha yao. Kuwa na nguvu katika imani kwa Mungu, upendo kwa wengine, na uvumilivu.

Vivyo hivyo wafundishe wanawake wazee wawe na mwenendo mzuri. Wafundishe wasiwe wachochezi na wasiwe watumwa wa mvinyo. Wanapaswa kufundisha yale yaliyo mema. Kwa jinsi hiyo wataweza kuwakumbusha wanawake vijana jinsi wanavyopaswa kuishi. Wanawake vijana wanapaswa kuwaonesha upendo waume zao na kuwapenda watoto wao. Wanapaswa kuwa na busara na wasafi kiroho, wakizitunza nyumba zao, kuwa wakarimu, na kuwa tayari kuwatumikia waume zao wenyewe, ili asiwepo atakayeudharau ujumbe wa Neno la Mungu.

Kadhalika endelea kuwahimiza wanaume vijana kuwa na busara. Katika kila kitu ujioneshe kuwa wewe ni mfano wa matendo mema. Katika mafundisho yako onesha kuwa una moyo safi na uko makini. Ufundishe kile ambacho ni sahihi kwa wazi, ili asiwepo yeyote atakayepinga mafundisho yako. Tumia mazuri ambayo hayatasemwa vibaya ili wale wanaokupinga waaibishwe kwa ajili ya kukosa lo lote baya la kusema dhidi yetu.

Wafundishe watumwa kuwatii bwana zao katika kila jambo, wajitahidi kuwapendeza na sio kubishana nao 10 wala kwa siri wasiwaibie bali waudhihirishe uaminifu kamili, ili katika mambo yote wayapatie sifa njema mafundisho kutoka kwa Mungu, Mwokozi wetu.

11 Maana Mungu ameidhihirisha neema yake inayookoa kwa watu wote. 12 Hiyo inatufundisha kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia ili tuishi katika ulimwengu wa sasa kwa njia ya werevu, haki na kuionesha heshima yetu kwa Mungu, 13 kadri tunavyosubiri ile Siku iliyobarikiwa tunayoitumaini ambapo utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi Yesu Kristo itakapofunuliwa. 14 Alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili aweze kutuweka huru sisi kutoka katika uovu wote na kuweza kutusafisha kwa ajili yake watu walio wake mwenyewe, wale walio na shauku ya kufanya matendo mema.

15 Endelea kufundisha ukihimiza na kukemea kuhusu mambo haya, na fanya hivyo kwa mamlaka yote, na mtu yeyote asikudharau.