Mto Wa Maji Ya Uzima

22 Kisha yule malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima ung’aao kama kioo na kutiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo, kupitia katikati ya barabara kuu ya mji huo. Katika pande zote za mto huo kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, na kuzaa matunda yake kila mwezi. Majani yake ni ya kuwaponya watu wa mataifa. Katika mji huo hakutakuwa na kitu cho chote kilicholaaniwa, bali kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo humo na watumishi wake watamwabudu. Watamwona uso wake na jina lake litakuwa kwe nye vipaji vya nyuso zao. Usiku hautakuwapo tena; wala hawata hitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atakuwa nuru yao, watatawala milele na milele.

Bwana Yesu Anakuja

Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuami nika na ya kweli. Bwana, Mungu wa roho za manabii, amemtuma mal aika wake kuwaonyesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutokea karibuni. Tazama, ninakuja upesi! Amebarikiwa anayesh ika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki.”

Mimi Yohana, ndiye niliyesikia na kuona mambo haya. Na nil ipokwisha kuyasikia na kuyaona, nilianguka kifudifudi penye miguu ya yule malaika aliyenionyesha mambo hayo, nimwabudu. Lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi pamoja na wewe na ndugu zako manabii na wote wanaoshika maneno ya kitabu hiki. Mwabudu Mungu!”

10 Kisha akaniambia, “Usiyawekee muhuri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki maana wakati umekaribia. 11 Mwache atendaye uovu aendelee kutenda uovu, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu; na atendaye mema aendelee kutenda mema na aliye mta katifu aendelee kuwa mtakatifu.”

12 “Tazama, Ninakuja upesi! Nakuja na tuzo yangu, nimpe tuzo kila mtu kulingana na matendo yake. 13 Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa wisho, Mwanzo na Mwisho.” 14 Wamebari kiwa wanaoosha mavazi yao ili wapate haki ya kushiriki mti wa uzima na wapate kuingia katika ule mji kupitia kwenye milango yake. 15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye udanganyifu na kuutenda. 16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ni Shina na Mzao wa ukoo wa Daudi. Mimi ni Nyota ya asubuhi ing’aayo.”

17 Roho na bibi harusi wanasema, “Njoo!” Na kila mtu asi kiaye na aseme, “Njoo!” Na mtu ye yote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na apokee zawadi ya maji ya uzima bure. .

18 Namwonya kila mtu asikiaye maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: mtu ye yote akiyaongezea cho chote, Mungu atamwongezea maafa yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na kama mtu ye yote akipunguza cho chote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang’anya sehemu yake katika mti wa uzima na katika mji mtakatifu, ambayo yameelezwa katika kitabu hiki.

20 Yeye anayeshuhudia mambo haya anasema, “Hakika ninakuja upesi!” Amina. Njoo, Bwana Yesu!

22 Malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima, ulikuwa anga'avu kama kioo. Mto hutiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo. Hutiririka kupitia katika mtaa mkuu wa mji. Mti wa uzima[a] uko kila upande wa mto, na huzaa tunda kila mwezi, mara kumi na mbili kwa mwaka. Majani ya mti ni kwa ajili ya kutibu mataifa.

Katika mji ule hakuna mtu au kitu kitakachokuwa chini ya laana ya Mungu tena. Kiti cha ufalme cha Mungu na Mwanakondoo vitakuwa ndani ya mji. Watumishi wa Mungu watamwabudu yeye. Watauona uso wake. Jina la Mungu litaandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao. Hakutakuwa usiku tena. Watu hawatahitaji mwanga wa taa au mwanga wa jua. Bwana Mungu atawapa mwanga. Watatawala kama wafalme milele na milele.

Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminiwa. Bwana, Mungu awavuviaye manabii, amemtuma malaika wake kuwaonesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee hivi karibuni: ‘Sikiliza, Naja upesi! Heri anayetii maneno ya unabii yaliyo katika kitabu hiki.’”

Mimi ni Yohana. Mimi ndiye niliyesikia na kuyaona mambo haya. Baada ya kuyasikia na kuyaona, niliinama chini kusujudu miguuni pa malaika aliyeyaonesha kwangu. Lakini malaika aliniambia, “Usinisujudie mimi! Mimi ni mtumishi kama wewe na ndugu zako manabii, ni mtumishi kama wale wote wanaoyatii maneno yaliyo katika kitabu hiki. Msujudie Mungu!”

10 Kisha malaika akaniambia, “Usiyafanye siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, wakati umekaribia kwa mambo haya kutokea. 11 Kila atendaye mabaya aendelee kutenda mabaya. Yeyote aliye mchafu aendelee kuwa mchafu. Atendaye mema aendelee kutenda mema. Aliye mtakatifu aendelee kuwa mtakatifu.”

12 “Sikiliza, nakuja upesi! Nakuja na ujira ili kumlipa kila mtu sawa sawa na matendo yake. 13 Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.

14 Heri walioosha kanzu zao.[b] Watakuwa na haki ya kula chakula kutoka kwenye mti wa uzima. Wanaweza kuingia katika mji kwa kupitia katika malango yake. 15 Nje ya mji ni kwa ajili wale waishio kama mbwa; wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wapendao kudanganya na kujifanya wema.

16 Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kukuambia mambo hayo kwa ajili ya makanisa. Mimi ni mzao wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi.”

17 Roho Mtakatifu na bibi arusi wanasema, “Njoo!” Kila asikiaye hili aseme pia, “Njoo!” Wote wenye kiu waje wanywe maji ya uzima bure ikiwa wanataka.

18 Ninamwonya kila mtu anayesikia maneno ya unabii wa kitabu hiki: Ikiwa mtu yeyote ataongeza chochote kwa haya, Mungu atampa mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na ikiwa mtu yeyote akitoa sehemu yoyote ya maneno ya kitabu hiki cha unabii, Mungu ataondoa sehemu ya urithi wa mtu huyo katika mti wa uzima na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

20 Yesu ndiye anayesema kwamba haya yote ni kweli. Sasa anasema, “Ndiyo, naja upesi.”

Amina! Njoo, Bwana Yesu!

21 Neema ya Bwana Yesu iwe pamoja na watu wote.

Footnotes

  1. 22:2 Mti wa uzima Tazama 2:7.
  2. 22:14 walioosha kanzu zao Wamefua kanzu zao. Inamaanisha kwamba walimwamini Yesu na wamesafishwa dhambi zao kwa sadaka ya yake ya damu. Tazama Ufu 5:9; Ebr 9:14; 10:14-22; Mat 22:16; 1 Yoh 1:7.