Kiti Cha Enzi Kilichoko Mbinguni

Baada ya hayo nilitazama, nikaona mlango ulio wazi mbin guni. Na ile sauti niliyokuwa nimeisikia ikisema nami kama tar umbeta ikasema, “Njoo huku juu nami nitakuonyesha yatakayotokea baada ya haya. ” Ghafla nilikuwa katika Roho, na mbele yangu kilikuwapo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa. Aliyeketi kwenye kiti hicho cha enzi alionekana kama jiwe zuri jekundu na akiki, na upinde wa mvua ulizunguka kile kiti cha enzi, ukione kana kama zumaridi. Kiti hicho kilizungukwa na viti vingine ishirini na vinne vya enzi ambavyo juu yake walikaa wazee ishi rini na wanne waliokuwa wamevalia mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani. Na katika kile kiti cha enzi kulitoka umeme, ngurumo na sauti. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya kile kiti cha enzi, ambazo ni zile roho saba za Mungu. Mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na kitu kinachofanana na bahari ya kioo iking’aa kama jiwe la kioo. Katikati, kuzunguka kile kiti cha enzi, walikuwapo viumbe hai wanne, wenye macho kila mahali, mbele na nyuma.

Kiumbe hai wa kwanza alifanana na simba, wa pili alifanana na ng’ombe dume, wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu, wa nne alifanana na tai arukaye. Na hawa viumbe hai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita na macho kila mahali, hata chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kuimba, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”

Kila mara viumbe hao wanne walipomtukuza na kumheshimu na kumshukuru yeye aliyeketi kwenye kiti cha enzi na aishie milele na milele, 10 wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele zake yeye aliyeketi kwenye kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Wakaziweka taji zao mbele ya kile kiti cha enzi wakisema, 11 “Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ni wewe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako vitu vyote viliumbwa na vinapata kuwapo.”

Yohana Aiona Mbingu

Kisha nikatazama, na mbele yangu ulikuwepo mlango uliokuwa wazi mbinguni. Na nikasikia sauti iliyosema nami mwanzoni. Ilikuwa sauti iliyosikika kama tarumbeta. Ilisema, “Njoo huku juu, nitakuonesha yale ambayo ni lazima yatokee baada ya hili.” Ghafla Roho akanichukua, na huko mbinguni kilikuwepo kiti cha enzi na mmoja amekaa juu yake. Aliyekikalia alikuwa mzuri kama mawe ya thamani, kama yaspi na karneli. Pande zote kuzunguka kiti cha enzi kulikuwa upinde wa mvua wenye rangi kama zumaridi.

Vilikuwepo viti vingine vya enzi ishirini na nne kuzunguka kiti cha enzi vilivyokaliwa na wazee ishirini na nne. Wazee walikuwa wamevaa nguo nyeupe na taji za dhahabu vichwani mwao. Mianga na ngurumo za radi vilitoka katika kiti cha enzi. Mbele ya kiti cha enzi zilikuwepo taa saba zikiwaka, ambazo ndizo Roho saba za Mungu. Pia mbele ya kiti cha enzi kilikuwepo kitu kilichoonekana kama bahari ya kioo, iiliyo angavu sana.

Mbele ya kiti cha enzi na kukizunguka pande zake zote walikuwepo viumbe wenye uhai wanne. Walikuwa na macho kila mahali. Kiumbe wa kwanza alikuwa kama simba. Wa pili alikuwa kama fahali. Wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu. Wa nne alikuwa kama tai anayeruka. Kila mmoja wa hawa wenye uhai wanne alikuwa na mabawa sita. Walikuwa na macho kila mahali, ndani na nje. Usiku na mchana hawaachi kusema:

“Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu Mwenye nguvu zote.
    Daima amekuwepo, yupo na anakuja.”

Wenye uhai hawa wanne walikuwa wanampa utukufu, heshima na shukrani yule anayekaa kwenye kiti cha enzi, anayeishi milele na milele. Na kila wakati walifanya hivyo, 10 wazee ishirini na nne waliinama mbele ya[a] yule anayekaa kwenye kiti cha enzi. Wanamwabudu anayeishi milele na milele. Wanaweka taji zao mbele ya kiti cha enzi na kusema:

11 “Bwana wetu na Mungu!
    Unastahili kupokea utukufu, heshima na nguvu.
Uliumba vitu vyote.
    Kila kinachoishi kiliumbwa kwa sababu ulitaka.”

Footnotes

  1. 4:10 waliinama mbele ya Yaani, “walimsujudia”.