Adhabu Ya Babiloni

17 Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba akaja akaniambia, “Njoo, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aliyeketi juu ya maji mengi. Wafalme wa dunia wamezini naye, na watu waishio duniani walilewa divai yake ya uzinzi.” Kisha nikiwa katika Roho malaika akanipeleka nyikani, nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumtukana Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu na kujipamba kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya kuchukiza na uchafu wa uasherati wake. Na kwenye kipaji cha uso wake yaliandikwa maneno yenye maana iliyofichika: “Babiloni Mkuu, Mama wa Makahaba na wa Machukizo yote ya Duniani.” Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa damu ya watu wa Mungu na damu ya watu waliouawa kwa kumshuhudia Yesu. Nilipomwona, nilistaajabu sana. Lakini yule malaika akaniambia, “Kwa nini unastaajabu? Nitakufunulia siri ya huyo mwanamke na huyo mnyama aliyembeba, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Huyo mnyama uliyemwona alikuwapo lakini sasa hayupo , naye atapanda kutoka katika shimo la kuzimu kwenda maangamizoni. Na watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu ulimwengu kuumbwa, watashangaa kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwapo, na hayupo, na kwamba atakuwapo.

Jambo hili linahitaji hekima na maarifa. Vile vichwa saba ni milima saba ambapo huyo mwanamke ameketi. 10 Pia hivyo vichwa saba ni wafalme saba ambao kati yao watano wamekwisha kuanguka, mmoja yupo na mmoja hajaja bado, naye akija, atalazimika kukaa kwa muda mfupi tu. 11 Na huyo mnyama aliyekuwapo ambaye hayupo, yeye ni wa nane, lakini ni wa kundi la wale saba naye pia ataan gamizwa.

12 Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao hawaja tawazwa bado, lakini watatawazwa kwa muda wa saa moja tu pamoja na yule mnyama. 13 Hawa wana nia moja nao watampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. 14 Watampiga vita Mwana-Kondoo na Mwa na-Kondoo atawashinda kwa kuwa yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme, na wale walio pamoja naye wanaitwa wateule na waami nifu.”

15 Kisha akaniambia, “Yale maji uliyoyaona alipokuwa amekaa yule kahaba, ni watu na umati wa watu na mataifa na lugha. 16 Na zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama watamchukia huyo kahaba; watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kabisa kwa moto. 17 Maana Mungu amefanya mioyo yao kutimiza mapenzi yake, kwa kuwafanya wawe na nia moja ya kumpa mamlaka yao ya kifalme huyo mnyama, mpaka maneno ya Mungu yataka potimizwa. 18 Na yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkuu wenye mamlaka juu ya wafalme wa dunia.”