Add parallel Print Page Options

Muhuri wa Saba

Mwanakondoo alipoufungua muhuri wa saba, kulikuwa ukimya mbinguni kama nusu saa hivi. Niliwaona malaika saba wanaosimama mbele ya Mungu. Walipewa tarumbeta saba.

Malaika mwingine akaja na kusimama kwenye madhabahu. Malaika huyu alikuwa na chetezo ya dhahabu. Malaika alipewa ubani mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote wa Mungu. Malaika akaweka sadaka hii juu ya madhabahu ya dhahabu mbele ya kiti cha enzi. Moshi kutoka kwenye ubani ukatoka kwenye mikono ya malaika kwenda kwa Mungu. Moshi ukaenda kwa Mungu ukiwa na Maombi ya watakatifu. Kisha malaika akaijaza chetezo moto kutoka madhabahuni na kuitupa chini duniani, kukatokea miali, radi na ngurumo zingine na tetemeko la ardhi.

Sauti ya Tarumbeta ya Kwanza

Kisha malaika saba wenye tarumbeta walijiandaa kupuliza tarumbeta zao.

Malaika wa kwanza alipuliza tarumbeta yake. Mvua ya mawe na moto uliochanyanyikana na damu vilimwagwa chini duniani. Theluthi moja ya dunia na nyasi zote za kijani na theluthi ya miti vikaungua.

Malaika wa pili alipopuliza tarumbeta yake. Kitu fulani kilichoonekana kama mlima mkubwa unaowaka moto kilitupwa baharini. Na theluthi moja ya bahari ikawa damu. Na theluthi moja ya viumbe walioumbwa wanaokaa baharini wakafa na ya meli theluthi moja zikaharibika.

10 Malaika wa tatu alipopuliza tarumbeta yake. Nyota kubwa, inayowaka kama tochi ikaanguka kutoka mbinguni. Ilianguka kwenye theluthi moja ya mito na chemichemi za maji. 11 Jina la nyota hiyo lilikuwa Uchungu.[a] Na theluthi moja ya maji yote yakawa machungu. Watu wengi wakafa kutokana na kunywa maji haya machungu.

12 Malaika wa nne alipopuliza tarumbeta yake. Theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota vikapigwa. Hivyo theluthi moja yao vikawa giza. Theluthi moja ya mchana na usiku ikakosa mwanga.

13 Nilipokuwa ninatazama, nilimsikia tai aliyekuwa anaruka juu sana angani akisema kwa sauti kuu, “Ole! Ole! Ole kwa wale wanaoishi duniani! Shida kuu zitaanza baada ya sauti za tarumbeta ambazo malaika wengine watatu watapuliza.”

Footnotes

  1. 8:11 Uchungu Kwa maana ya kawaida, “mti mchungu”, mti mchungu sana; hapa, inaashiria huzuni yenye uchungu mwingi.