Basi, maadamu ahadi ya Mungu ya kuingia katika pumziko lake bado ipo, tujihadhari asije mmoja wenu akakutwa ameshindwa kuin gia huko. Maana sisi tumehubiriwa Habari Njema kama vile wao walivyohubiriwa. Lakini ujumbe waliosikia haukuwasaidia kwa sababu hawakuupokea kwa imani. Kwa kuwa sisi tulioamini tunain gia katika pumziko hilo, kama Mungu alivyosema, “Na katika hasira yangu nikaapa, ‘Hawataingia kwenye pumziko langu kamwe.’ Mungu alisema hivyo ingawa kazi yake ilikamilika tangu ulimwengu ulipoumbwa. Maana mahali fulani akizungumza kuhusu siku ya saba, alisema: “Mungu alipumzika siku ya saba baada ya kazi zake zote.” Na tena mahali hapo alisema: “Hawataingia kwenye pum ziko langu kamwe.” Basi kwa kuwa wapo watakaoingia kwenye pum ziko hilo, na wale ambao walihubiriwa Habari Njema hapo mwanzo lakini wakashindwa kuingia kwa sababu ya kutokutii kwao, kwa hiyo Mungu aliweka tena siku nyingine akaiita “Leo”; akasema kwa maneno ya Daudi miaka mingi baadaye, kama yalivyokwisha kukaririwa: “Leo mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu.”

Maana, kama Yoshua angalikuwa amekwisha kuwapatia pumziko, Mungu asingalizungumzia baadaye kuhusu siku nyingine. Kwa hiyo basi ipo bado sabato ya mapumziko waliyowekewa watu wa Mungu; 10 kwa maana, mtu anayeingia katika pumziko la Mungu, pia hupum zika kutoka katika kazi zake kama vile Mungu alivyopumzika baada ya kazi zake.

11 Basi tujitahidi kuingia kwenye pumziko hilo asije mtu akaanguka kwa kutokuamini kama hao. 12 Kwa maana neno la Mungu ni hai tena lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili, linachoma kabisa na kutenganisha nafsi na roho, viungo vya mwili na mafuta yaliyomo ndani yake; na kutambua nia na mawazo ya mioyo ya watu. 13 Hakuna kiumbe cho chote kilichofi chika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye hatuna budi kueleza habari zetu zote kwake.

Kuhani Mkuu Yesu Kristo

14 Hivyo basi, kwa kuwa tunaye kuhani mkuu aliyepitia mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, tushikilie kwa uthabiti imani yetu tunayoikiri. 15 Kwa maana huyu kuhani wetu mkuu si kuhani ambaye hawezi kutuhurumia katika udhaifu wetu, bali ni kuhani ambaye kwa kila hali amejaribiwa kama sisi, lakini pasipo kutenda dhambi. 16 Kwa hiyo basi, tusogelee kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa shida.

Na bado tunayo ahadi ambayo Mungu aliwapa watu wake. Ahadi hiyo ni kwamba tuweze kuingia katika sehemu ya pumziko. Hivyo tunapaswa kuwa waangalifu ili asiwepo atakayeikosa ahadi hiyo. Ndiyo, habari njema kuhusu hilo zilielezwa kwetu kama ilivyokuwa kwao. Lakini ujumbe waliousikia haukuwasaidia. Waliusikia lakini hawakuupokea kwa imani. Ni sisi tu tunaoamini tunaoweza kuingia katika sehemu ya pumziko ya Mungu. Kama Mungu alivyosema:

“Nilikasirika na nikaweka ahadi:
    ‘Hawataingia kamwe kwenye sehemu yangu ya pumziko.’”(A)

Lakini kazi ya Mungu ilikamilika tangu wakati ule alipoumba ulimwengu. Ndiyo, mahali fulani katika Maandiko alizungumza juu ya siku ya saba ya juma. Alisema, “Hivyo katika siku ya saba, Mungu alipumzika kazi zake zote.”(B) Lakini katika Maandiko ya hapo juu Mungu alisema, “Hawataingia kamwe katika sehemu yangu ya pumziko.”

Hivyo fursa bado ipo kwa baadhi kuingia na kufurahia pumziko la Mungu. Lakini waliosikia kwanza habari njema juu yake hawakuweza kuingia, kwa sababu hawakutii. Hivyo Mungu akapanga siku nyingine maalumu. Inaitwa “leo.” Alizungumza juu ya siku hiyo kupitia kwa Daudi siku nyingi zilizopita kutumia maneno tuliyonukuu mwanzoni:

“Kama leo mtaisikia sauti ya Mungu,
    msiifanye migumu mioyo yenu.”(C)

Tunajua kuwa Yoshua hakuwaongoza watu hadi sehemu ya pumziko ambayo Mungu aliwaahidi. Tunalijua hili kwa sababu Mungu alisema baadaye kuhusu siku ya pumziko. Hii inaonesha kuwa pumziko la siku ya saba[a] kwa watu wa Mungu bado linakuja. 10 Mungu alipumzika alipokamilisha kazi yake. Hivyo kila mmoja anayeingia katika sehemu ya pumziko ya Mungu vilevile atapata pumziko kutoka katika kazi yake kama Mungu alivyofanya. 11 Hivyo hebu na tujitahidi tuwezavyo kuingia katika sehemu ya pumziko ya Mungu. Tunapaswa kujitahidi ili asiwepo miongoni mwetu atakayepotea kwa kufuata mfano wa wale waliokataa kumtii Mungu.

12 Neno la Mungu[b] liko hai na linatenda kazi. Lina ukali kupita upanga ulio na makali sana na hukata hadi ndani yetu. Hukata ndani hadi sehemu ambayo nafsi na roho huwa zimeunganishwa pamoja. Neno la Mungu hukata hadi katikati ya maungio na mifupa yetu. Linahukumu mawazo na hisia ndani ya mioyo yetu. 13 Hakuna chochote ulimwenguni mwote kinachoweza kufichika mbele za Mungu. Anaweza kuviona vitu vyote kwa uwazi kabisa. Kila kitu kiko wazi mbele zake. Na kwake tutapaswa kujieleza jinsi tulivyoishi.

Yesu Kristo Ndiye Kuhani Wetu Mkuu

14 Tunaye kuhani mkuu sana ambaye ameenda kuishi na Mungu kule mbinguni. Yeye ni Yesu Mwana wa Mungu. Hivyo tuendelee kuitamka imani yetu katika yeye. 15 Yesu, kuhani wetu mkuu, anaweza kuuelewa udhaifu wetu. Yesu alipoishi duniani, alijaribiwa katika kila njia. Alijaribiwa kwa njia hizo hizo tunazojaribiwa, lakini hakutenda dhambi. 16 Tukiwa na Yesu kama kuhani wetu mkuu, tunaweza kujisikia huru kuja mbele za kiti cha enzi cha Mungu ambako kuna neema. Hapo tunapata rehema na neema ya kutusaidia tunapokuwa tunahitaji.

Footnotes

  1. 4:9 pumziko la siku ya saba Kwa maana ya kawaida, “pumziko la Sabato”, ikimaanisha kushirikiana katika pumziko aliloanzisha Mungu baada ya kuumba ulimwengu.
  2. 4:12 Neno la Mungu Mafundisho na amri za Mungu.