Add parallel Print Page Options

Yesu Kuhani Wetu Mkuu

Hii ndiyo hoja tunayosema: Tunaye kuhani mkuu wa jinsi hiyo, anayeketi upande wa kuume[a] wa kiti cha enzi cha Mungu Mkuu mbinguni. Kuhani wetu mkuu anahudumia katika Patakatifu pa Patakatifu.[b] Anahudumia katika mahali pa hakika kwa ibada[c] palipotengenezwa na Bwana, siyo na mtu yeyote duniani.

Kila kuhani mkuu anayo kazi ya kutoa sadaka na sadaka kwa Mungu. Hivyo kuhani wetu mkuu pia anahitajika kutoa kitu kwa Mungu. Kama kuhani wetu mkuu angekuwa anaishi duniani, asingekuwa kuhani. Nasema hivi kwa sababu tayari hapa wapo makuhani ambao wanafuata sheria kwa kutoa sadaka kwa Mungu. Kazi ambayo makuhani hawa wanafanya hakika ni nakala tu na kivuli cha yaliyoko mbinguni. Ndiyo sababu Mungu alimwonya Musa alipokuwa amejiandaa kujenga Hema Takatifu: “Uwe na uhakika kufanya kila kitu sawasawa na kielelezo nilichokuonesha kule mlimani.”(A) Lakini kazi ambayo tayari imetolewa kwa Yesu ni kuu zaidi ya kazi iliyotolewa na makuhani hao. Kwa jinsi hiyo hiyo, agano jipya ambalo Yesu alilileta kutoka kwa Mungu kuja kwa watu wake ni kuu zaidi kuliko lile la zamani. Na agano jipya limeelemea katika ahadi bora zaidi.

Kama kusingekuwa na makosa katika agano la kwanza, kisha kusingekuwa na haja ya agano la pili. Lakini Mungu aligundua kitu kilichokuwa na kasoro kwa watu, akasema:

“Wakati unakuja, asema Bwana,
    nitakapofanya agano jipya na watu wa Israeli na watu wa Yuda.
Halitakuwa sawa na agano lililotengenezwa na baba zao.
    Hilo ni agano nililowapa nilipowachukua kwa mkono na kuwatoa Misri.
Hawakuendelea kufuata agano nililowekeana nao,
    na nikageuka mbali nao, asema Bwana.
10 Hili ni agano jipya nitakalofanya
    na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana:
Nitaziweka sheria zangu katika fahamu zao,
    na nitaandika sheria zangu katika mioyo yao.
Nitakuwa Mungu wao,
    nao watakuwa watu wangu.
11 Hakuna tena atakayemfundisha jirani yake au familia yake kumjua Bwana.
    Watu wote, wakuu zaidi na wasio na umuhimu kabisa, watanijua.
12 Na nitawasamehe makosa waliyotenda,
    na sitazikumbuka dhambi zao.”(B)

13 Mungu aliliita hili ni agano jipya, hivyo amelifanya agano la kwanza kuwa la zamani. Na chochote kilicho cha zamani na kisichokuwa na matumizi kiko tayari kutoweka.

Footnotes

  1. 8:1 upande wa kuume Mahali pa heshima na mamlaka (nguvu).
  2. 8:2 Patakatifu pa Patakatifu Kwa maana ya kawaida, “patakatifu” kwa “Patakatifu pa patakatifu”, mahali pa kiroho ambapo Mungu anaishi na anaabudiwa. Mahali hapa pa kiroho kiliwakilishwa na chumba ndani ya Hema Takatifu katika Agano la Kale. Tazama Hema Takatifu na Patakatifu pa Patakatifu katika Orodha ya Maneno.
  3. 8:2 mahali pa hakika kwa ibada Kwa maana ya kawaida, “Hema ya kuabudia” au “hema”.