Basi, mimi niliye mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mu ishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa. Muwe wanyenyekevu, wapole, wenye subira, mkivumiliana ninyi kwa ninyi katika upend o. Muwe wepesi wa kutaka kudumisha umoja wa Roho kwa sababu ya amani inayowafunga pamoja. Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, k ama mlivyoitwa mpokee tumaini moja. Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja; na Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wot e, aliye juu ya wote, anayefanya kazi katika yote na aliye ndani ya yote. Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo alichogawiwa na Kristo. Kwa hiyo Maandiko yanasema: “Alipopaa juu, aliongoza mateka wengi, na akawapa watu zawadi.” Maandiko yanaposema, “Alipaa juu’ 10 Yeye aliyeshuka ndiye aliyepaa juu sana, kupita mbingu zote, ili apate kujaza vitu vyote. 11 Yeye ndiye aliyewapa watu vipawa, wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na walimu; 12 wapate kuwatayarisha watu wa Mungu kwa kazi za huduma, kwa ajili ya kujenga kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo. 13 Kazi hiyo itaende lea mpaka sote tuufikie umoja katika imani na katika kumjua Mwana wa Mungu; tupate kuwa watu waliokomaa kiroho kwa kufikia kiwango cha ukamilifu wote ulio ndani ya Kristo. 14 Hapo ndipo tutaacha kuwa tena kama watoto wadogo, wanaorushwarushwa huku na huko na kupeperushwa na kila upepo wa mafundisho na hila za watu wadan ganyifu. 15 Badala yake, tukiambiana ukweli kwa upendo, tutakua kwa kila hali, tufanane na Kristo ambaye ndiye kichwa. 16 Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeunganishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo vyake, hukua na kujengeka katika up endo, kila sehemu ikifanya kazi yake. Maisha Mapya Ndani Ya Kristo

17 Kwa hiyo nawaambia na kusisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa mataifa wasiomjua Mungu, ambao wanaon gozwa na mawazo yao yasiyofaa. 18 Watu hao akili zao zimetiwa giza wasiweze kuelewa; nao wametengwa mbali na uhai wa Mungu kwa sababu ya ujinga walionao na ugumu wa mioyo yao. 19 Kwa kuwa hawajali kuhusu mema na mabaya, wamekuwa sugu na kutawaliwa na uasherati, wakiwa na tamaa ya kutenda kila aina ya uchafu. 20 Lakini ninyi hamkujifunza hivyo kutoka kwa Kristo, 21 kama kweli mlisikia habari zake na kufundishwa kumhusu, kufuatana na kweli itokayo kwa Yesu. 22 Vueni maisha yenu ya zamani muweke kando hali yenu ya asili ambayo huharibiwa na tamaa potovu. 23 Nia zenu zifanywe upya 24 na mvae utu upya ulioumbwa kwa mfano wa Mungu katika haki na utakatifu. 25 Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja. 26 Mkikasirika, msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima 27 na kumpa she tani nafasi. 28 Mwizi asiibe tena, bali afanye kazi halali kwa mikono yake ili aweze kuwa na kitu cha kuwapa wenye kuhitaji msaada. 29 Msiruhusu maneno machafu yatoke vinywani mwenu, bali mazungumzo yenu yawe ya msaada katika kuwajenga wengine kufuatana na mahitaji yao, ili wale wanaowasikiliza wapate kufaidika. 30 Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi. 31 Ondoeni kabisa chuki yote, ghadhabu, hasira, ugomvi na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. 32 Muwe wema na wenye mioyo ya upendo kati yenu, na kusameheana kama Mungu alivyowasamehe kwa ajili ya Kristo. Watoto Wa Nuru