Kutoka kwa Paulo, mtumwa wa Yesu Kristo na mtume niliyecha guliwa na kuitwa kuhubiri Habari Njema ya Mungu. Habari hii aliiahidi tangu zamani kwa njia ya manabii wake katika Maandiko matakatifu.

Habari hii njema ni kuhusu Mwana wa Mungu ambaye kimwili alizaliwa katika ukoo wa Daudi, na ambaye alidhihiri shwa kuwa Mwana wa Mungu kwa uwezo wa Roho wa utakatifu kwa kufufuliwa kutoka kwa wafu. Yeye ndiye Yesu Kristo Bwana wetu, ambaye kutoka kwake, na kwa ajili yake, tumepokea neema na agizo la kuwaongoza watu wa mataifa yote wasiomjua Mungu, wapate kumwamini na kumtii. Ninyi pia ni miongoni mwa watu walioitwa kuwa wafuasi wa Yesu Kristo.

Basi, nawatakieni ninyi nyote mlioko huko Roma, ambao ni wapendwa wa Mungu mlioitwa muwe watakatifu, neema na amani ito kayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Maombi Na Shukrani

Kwanza kabisa, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inatangazwa duniani kote. Mungu ninayemtumikia kwa moyo wangu wote ninapo hubiri Habari Njema ya Mwanae, anajua jinsi ninavyowakumbuka siku zote 10 katika sala zangu kila ninapoomba. Namwomba Mungu, akipenda, hatimaye sasa nipate nafasi ya kuja kwenu. 11 Ninata mani sana kuwaona ili niwagawie zawadi ya kiroho ya kuwaima risha, 12 yaani tuimarishane: mimi nitiwe moyo kwa imani yenu na ninyi mtiwe moyo kwa imani yangu.

13 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba mara nyingi nimeku sudia kuja kwenu, ingawa mpaka sasa nimezuiliwa. Ningependa kupata mavuno ya waamini kati yenu kama nilivyofanikiwa kupata waamini kati ya watu wa mataifa mengine.

14 Ninawajibika kwa watu wote, Wagiriki na wasiokuwa Wagi riki; wenye elimu na wasiokuwa na elimu. 15 Ndio maana ninata mani sana kuhubiri Injili kwenu ninyi pia mlioko Roma.

16 Mimi siionei aibu Injili kwa maanani nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia. 17 Kwa maana Habari hii Njema inaonyesha wazi haki inayotoka kwa Mungu. Haki hii hupatikana kwa imani tangu mwanzo hadi mwisho. Kama ilivyoandikwa: “Wenye haki wataishi kwa imani.”

Ghadhabu Ya Mungu Kwa Wanadamu

18 Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wa wanadamu ambao kwa uovu wao wanauficha ukweli usijulikane. 19 Kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao kwa sababu Mungu mwenyewe ameyaweka wazi. 20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uwezo wake wa milele na Uungu wake, umedhihirika wazi wazi kutokana na vitu alivyoviumba. Kwa hiyo watu hawana kisingizio.

21 Ingawa walimjua Mungu, hawakumpa heshima na utukufu anaostahili wala kumshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao zilizopumbaa zikatiwa giza. 22 Wakijidai kuwa ni werevu, wakawa wajinga. 23 Wakauacha utukufu wa Mungu aishiye milele wakageukia sanamu zinazofanana na mwanadamu ambaye hufa, na ndege na wanyama na viumbe vitambaavyo.

24 Kwa hiyo, Mungu aliwaacha waendelee kufuata tamaa mbaya za mioyo yao na kutenda matendo ya unajisi nakufanyiana mambo ya aibu katika miili yao. 25 Hii ni kwa sababu walikataa ukweli ku husu Mungu wakaamua kuamini uongo; wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Muumba ahimidiwaye milele! Amina.

26 Kwa hiyo, Mungu aliwaachia wafuate tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao waliacha matumizi ya asili ya maumbile yao wakatumia miili yao isivyokusudiwa. 27 Hali kadhalika wanaume waliacha uhusiano wa asili kati ya waume na wake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume walifanyiana mambo ya aibu, nao waka pata katika miili yao adhabu waliyostahili kama matokeo ya uovu wao.

28 Zaidi ya hayo, kwa sababu walikataa kumtambua Mungu, yeye aliwaacha katika nia zao za upotovu watende mambo yasiyosta hili kutendwa. 29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu, tamaa na ubaya. Wamejawa na husuda, uuaji, fitina, hadaa, nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, 30 wasingiziaji, wanaomchukia Mu ngu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno; wenye hila, wasiotii wazazi wao; 31 niwajinga, wasioamini, wasio na huruma nawaka tili. 32 Ingawa wanafahamu sheria ya Mungu kwamba watu wanaoishi maisha ya namna hii wanastahili mauti, bado wanaendelea kutenda mambo haya na kuwasifu wengine wafanyao kama wao.

Salamu kutoka kwa Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu.[a]

Mungu alinichagua niwe mtume na akanipa kazi ya kuhubiri Habari Njema yake. Tangu zamani, kwa vinywa vya manabii katika Maandiko Matakatifu, Mungu aliahidi kwamba angewaletea Habari Njema watu wake. Habari Njema hii inahusu Mwana wa Mungu, ambaye kama mwanadamu, alizaliwa katika ukoo wa Mfalme Daudi. Na alipofufuliwa na Roho Matakatifu[b] kutoka kwa wafu, alipewa mamlaka kamili ya kutawala kama Mwana wa Mungu. Ni Yesu Kristo, Bwana wetu.

Kupitia kwa Yesu, Mungu amenionyesha wema wake. Na amenipa mamlaka ya kuwaendea watu wa mataifa yote na kuwaongoza kumwamini na kumtii yeye. Kazi yote hii ni kwa ajili yake. Nanyi pia ni miongoni mwa waliochaguliwa na Mungu ili mmilikiwe na Yesu Kristo.

Waraka huu ni kwa ajili yenu ninyi nyote mlio huko Rumi. Kwani Mungu anawapenda na amewachagua kuwa watu wake watakatifu.

Ninamwomba Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo, wawape ninyi neema na amani.

Maombi ya Shukrani

Kwanza, ninamshukuru Mungu wangu kupitia Yesu Kristo kwa ajili yenu ninyi nyote. Ninamshukuru yeye kwa sababu kila mahali ulimwenguni watu wanazungumza kuhusu imani yenu kuu. 9-10 Kila wakati ninapoomba, ninawakumbuka ninyi daima. Mungu anajua kuwa hii ni kweli. Yeye ndiye ninayemtumikia kwa moyo wangu wote nikiwaambia watu Habari Njema kuhusu Mwanaye. Hivyo ninaendelea kuomba kwamba mwishowe Mungu atanifungulia njia ili niweze kuja kwenu. 11 Ninataka sana niwaone na niwape zawadi ya kiroho ili kuimarisha imani yenu. 12 Ninamaanisha kuwa ninataka tusaidiane sisi kwa sisi katika imani tuliyo nayo. Imani yenu itanisaidia mimi, na imani yangu itawasaidia ninyi.

13 Kaka zangu na dada zangu, ninataka mjue kwamba nimepanga mara nyingi kuja kwenu, lakini jambo fulani hutokea na kubadili mipango yangu kila ninapopanga kuja. Juu ya kazi yangu miongoni mwenu, ningependa kuona matokeo yale yale mazuri yakitokea ya kazi yangu miongoni mwa watu wengine wasio Wayahudi.

14 Imenilazimu kuwatumikia watu wote; waliostaarabika na wasiostaarabika,[c] walioelimika na wasio na elimu. 15 Ndiyo sababu ninataka sana kuzihubiri Habari Njema kwenu ninyi pia mlio huko Rumi.

16 Kwa mimi hakuna haya[d] katika kuhubiri Habari Njema. Ninayo furaha kwa sababu Habari Njema ni nguvu ya Mungu inayomwokoa kila anayeamini, yaani inawaokoa Wayahudi kwanza, na sasa inawaokoa Mataifa.[e] 17 Ndiyo, wema wa uaminifu wa Mungu umedhihirishwa katika Habari Njema kwa uaminifu wa mmoja, ambao huongoza imani ya wengi. Kama Maandiko yanavyosema, “Aliye na haki mbele za Mungu[f] ataishi kwa imani.”[g]

Mungu ni Mwaminifu Na Atauadhibu Uovu

18 Mungu huonesha hasira yake kutokea mbinguni dhidi ya mambo mabaya ambayo waovu hutenda. Hawamheshimu na wanatendeana mabaya. Maisha yao maovu yanasababisha ukweli kuhusu Mungu usijulikane. 19 Hili humkasirisha Mungu kwa sababu wamekwisha oneshwa Mungu alivyo. Ndiyo, Mungu ameliweka wazi kwao.

20 Yapo mambo yanayoonekana kuhusu Mungu, kama vile nguvu zake za milele na yale yote yanayomfanya awe Mungu. Lakini tangu kuumbwa kwa ulimwengu, mambo haya yamekuwa rahisi kwa watu kuyaona. Maana yake ni kuwa, watu wanaweza kumwelewa Mungu kwa kuangalia yale aliyoumba. Hivyo watu hawana udhuru kwa uovu wanaotenda.

21 Watu walimjua Mungu, lakini hawakumheshimu kama Mungu. Na hawakumpa shukrani. Badala yake waliyageukia mambo ya hovyo yasiyo na manufaa. Akili zao zilichochanganyikiwa zilijaa giza. 22 Walisema kuwa wana hekima, lakini wakawa wajinga. 23 Hawakuuheshimu ukuu wa Mungu, anayeishi milele. Wakaacha kumwabudu Mungu wakaanza kuabudu sanamu, vitu vilivyotengenezwa vikaonekana kama wanadamu, ambao wote mwisho hufa, au kwa mfano wa ndege na wanyama wanaotembea na wanaotambaa.

24 Hivyo Mungu akawaacha wazifuate tamaa zao chafu. Wakawa najisi na wakaivunjia heshima miili yao kwa njia za uovu walizotumia. 25 Waliibadili kweli kuhusu Mungu kwa uongo. Wakasujudu na kuabudu vitu alivyoviumba Mungu badala ya kumwabudu Mungu aliyeviumba vitu hivyo. Yeye ndiye anayepaswa kusifiwa milele yote. Amina.

26 Hivyo, kwa kuwa watu hawakumheshimu Mungu, Mungu akawaacha wafuate tamaa zao za aibu. Wanawake wao wakabadili namna ya kujamiiana na wakawatamani wanawake wenzao na wakajamiiana wao kwa wao. 27 Wanaume wakafanya vivyo hivyo. Wakaacha kujamiiana na wanawake kwa mfumo wa asili, wakaanza kuwawakia tamaa wanaume wenzao. Wakafanya mambo ya aibu na wanaume na wavulana. Wakajiletea aibu hii juu yao wenyewe, wakapata yale waliyostahili kwa kutelekeza kweli.

28 Watu hawa waliona kuwa haikuwa muhimu kwao kumkubali Mungu katika fikra zao. Hivyo Mungu akawaacha wayafuate mawazo yao mabaya. Hivyo hufanya mambo ambayo mtu yeyote hapaswi kufanya. 29 Maisha yao yamejaa kila aina ya matendo mabaya, uovu, tamaa na chuki. Wamejaa wivu, uuaji, ugomvi, uongo na hamu ya kuwadhuru wengine. Wanasengenya 30 na kusemana maovu wao wenyewe. Wanamchukia Mungu. Ni wakorofi, wana kiburi na hujivuna. Hubuni njia za kufanya maovu. Hawawatii wazazi wao. 31 Ni wapumbavu, hawatimizi ahadi zao. Hawawaoneshi wema wala huruma wengine. 32 Wanajua amri ya Mungu kuwa yeyote anayeishi kwa namna hiyo lazima afe. Lakini si tu kwamba wanaendelea kufanya mambo haya wenyewe, bali wanakubaliana na wengine wanaofanya mambo hayo.

Footnotes

  1. 1:1 Kristo Yesu Au “Mfalme Yesu”. Neno “Kristo” ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania “Masihi”, ambao ni wadhifa wa kifalme. Tazama Mk 15:32: Lk 23:2. Tazama pia Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno.
  2. 1:4 Roho Matakatifu Kwa maana ya kawaida, “Roho wa Utakatifu”.
  3. 1:14 waliostaarabika na wasiostaarabika Kwa maana ya kawaida, “Wayunani na wasio Wayunani”. Tazama Wayunani katika Orodha ya Maneno.
  4. 1:16 hakuna haya Paulo anazungumzia suala la kuona haya kwa kuihubiri Habari Njema (injili) kwa sababu, nyakati zake, Habari Njema zilileta mshtuko na fadhaa kwa watu wengi. Kama anavyoandika katika barua zake nyingine, msingi wa ujumbe wake ulikuwa “Kristo (Mfalme toka kwa Mungu) aliuawa msalabani.” Anaongeza, “Ujumbe huu ni kikwazo kwa Wayahudi, na kwa watu wengine ni upuuzi.” Tazama 1 Kor 1:22-25.
  5. 1:16 Mataifa Yaani watu wasio Wayahudi.
  6. 1:17 Aliye na haki mbele za Mungu Au “Mwenye haki”, mara nyingi hutumika kama cheo cha Masihi, Mfalme Mteule wa Mungu aliyeahidiwa katika Agano la Kale. Tazama Isa 53:11; Hab 2:4; Zek 9:9; Mdo 3:14; 7:52; 22:14.
  7. 1:17 ataishi kwa imani katika Hab 2:4, ambayo pia, inaweza kutafsiriwa kuwa, “Mwenye haki ataishi kwa uaminifu.”