Ikiwa mtu anakushtaki na ninyi nyote mnaongozana kwenda mahakamani. Jitahidi kadri inavyowezekana kupatana naye mkiwa njiani. Usipopatana naye, atakupeleka kwa hakimu. Na hakimu atakutia hatiani na maofisa wa mahakama watakutupa gerezani.
Kama mtu akikushtaki mahakamani, jitahidi sana kupatana na mshtaki wako wakati mkiwa mnaenda mahakamani, ili asikufikishe mbele ya hakimu, na hakimu akakukabidhi kwa polisi, na polisi wakakutia gerezani.