Add parallel Print Page Options

Kwa hiyo Yuda akaongoza kundi la askari hadi katika bustani hiyo pamoja na walinzi wengine kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Hawa walikuwa wamebeba mienge, taa, na silaha.

Yesu alikwisha kujua yote ambayo yangempata. Hivyo aliwaendea na kuwauliza, “Je, ni nani mnayemtafuta?”

Wakamjibu, “Yesu kutoka Nazareti.”

Akawaambia, “Mimi ni Yesu.”[a] (Yuda yule aliyehusika kumsaliti Yesu alikuwa amesimama hapo pamoja nao.) Yesu aliposema, “Mimi ni Yesu,” wale watu walirudi nyuma na kuanguka chini.

Akawauliza tena, “Je, ni nani mnayemtafuta?”

Wakasema, “Yesu kutoka Nazareti.”

Yesu akasema, “Nimewaambia kwamba mimi ndiye Yesu. Hivyo kama mnanitafuta mimi, basi waacheni huru watu hawa waende zao.” Hii ilikuwa kuonesha ukweli wa yale aliyosema Yesu mapema: “Sikumpoteza hata mmoja wa wale ulionipa.”

10 Simoni Petro akauchomoa upanga aliokuwa ameufunga kiunoni. Akampiga nao mtumishi wa Kuhani Mkuu, na kulikata sikio lake la kulia. (Jina la mtumishi huyo lilikuwa ni Maliko.) 11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha jambia lako mahali pake! Ninapaswa kunywa toka kikombe[b] ambacho Baba amenipa nikinywee.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 18:5 Mimi ni Yesu Kwa maana ya kawaida, “Mimi ndimi”, ambayo inaweza kuwa na maana ile ile hapa kama ilivyo katika 8:24,28,58; 13:19. Pia katika mstari wa 8.
  2. 18:11 kikombe Kikombe ni ishara ya mateso. Yesu alitumia dhana ya kukinywea kikombe akimaanisha kuyakubali mateso ambayo angeyapata katika matukio ya kutisha ambayo yangetokea muda mfupi ujao.