Add parallel Print Page Options

43 Watu wote wakaushangaa ukuu wa nguvu ya Mungu.

Yesu Azungumza Kuhusu Kifo Chake

(Mt 17:22-23; Mk 9:30-32)

Watu walipokuwa bado wanayashangaa mambo yote aliyofanya Yesu. Akawaambia wanafunzi wake, 44 “Msiyasahau nitakayowaambia sasa: Mwana wa Adamu yu karibu kukamatwa na kuwekwa katika mikono ya watu wengine.” 45 Lakini wanafunzi hawakuelewa alichomaanisha. Maana ilifichwa kwao ili wasitambue. Lakini waliogopa kumwuliza Yesu kuhusiana na alilosema.

Read full chapter

43 Watu wote walishangaa walipoona huo uweza mkuu wa Mungu. Wakati watu walipokuwa wanas taajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Yesu, yeye aliwaambia wanafunzi wake: 44 “ Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: mimi Mwana wa Adamu nitasalitiwa na kuwekwa mikononi mwa wanadamu.” 45 Lakini wanafunzi wake hawakuyaelewa maneno hayo. Maana ya maneno hayo ilikuwa imefichwa ili wasiweze kuelewa, nao waliogopa kumwuliza.

Read full chapter