Add parallel Print Page Options

Yesu Amweka Huru Mvulana Kutoka Pepo Mchafu

(Mk 9:14-29; Lk 9:37-43a)

14 Yesu na wafuasi walirudi kwa watu. Mtu mmoja akamjia Yesu na kuinama mbele zake. 15 Akasema, “Bwana, umwonee huruma mwanangu. Anateswa sana na kifafa alichonacho. Anaangukia kwenye moto au maji mara kwa mara. 16 Nilimleta kwa wafuasi wako, lakini wameshindwa kumponya.”

17 Yesu akajibu, “Ninyi watu mnaoishi katika nyakati hizi cha kizazi kisicho na imani. Maisha yenu ni mabaya sana! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kijana hapa.” 18 Yesu akamwamuru pepo aliye ndani ya kijana, na pepo akamtoka na yule kijana akapona.

19 Kisha wafuasi wakamjia Yesu wakiwa peke yao. Wakasema, “Tulijaribu kumtoa pepo kwa kijana, lakini tulishindwa. Kwa nini tulishindwa kumtoa pepo?”

20 Yesu akajibu, “Mlishindwa kumtoa pepo kwa sababu imani yenu ni ndogo sana. Niaminini ninapowaambia, imani yenu ikiwa na ukubwa wa mbegu ya haradali mtaweza kuuambia mlima huu, ‘Ondoka hapa na uende kule,’ nao utaondoka. Nanyi mtaweza kufanya jambo lolote.”

Read full chapter

Yesu Amponya Kijana Mwenye Kifafa

14 Alipofikia ulipokuwa umati wa watu, mtu mmoja alimjia Yesu akapiga magoti mbele yake akasema, 15 “Bwana, mwonee huruma mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara nyingi huan guka motoni na kwenye maji. 16 Nimemleta kwa wanafunzi wako laki ni hawakuweza kumponya.”

17 Yesu akajibu, “Ninyi kizazi kipotovu msioamini, nitakaa nanyi mpaka lini na nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kijana hapa kwangu.” 18 Yesu akamkemea yule pepo mchafu, akamtoka yule kijana, naye akapona tangu wakati huo. 19 Kisha wanafunzi wakam wendea Yesu kwa siri wakamwuliza, “Kwa nini sisi hatukuweza kum toa? ” 20 Akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Nina waambieni kweli, mkiwa na imani kama punje ndogo ya haradali, mtauambia mlima huu, ‘Ondoka hapa uende pale’ nao utaondoka; na hakuna ambalo halitawezekana kwenu.” [

Read full chapter