Add parallel Print Page Options

Yesu Azungumza na Wafuasi Wake

(Mk 16:14-18; Lk 24:36-49; Yh 20:19-23; Mdo 1:6-8)

16 Wale wafuasi kumi na mmoja walikwenda Galilaya, kwenye mlima ambao Yesu aliwaambia waende. 17 Wakiwa mlimani, wafuasi wale walimwona Yesu na wakamwabudu. Lakini baadhi ya wafuasi hawakuwa na uhakika kama alikuwa Yesu. 18 Kisha Yesu akawajia na akasema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Hivyo nendeni ulimwenguni kote mkawafanye watu kuwa wafuasi wangu. Mkiwabatiza katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. 20 Wafundisheni kutii kila kitu nilichowaambia. Na tambueni hili: Niko pamoja nanyi daima. Na nitaendelea kuwa pamoja nanyi hata mwisho wa wakati.”

Read full chapter

Yesu Awatuma Wanafunzi Wake

16 Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya kwe nye ule mlima ambao Yesu aliwaagiza. 17 Walipomwona, walimwabu du. Lakini baadhi yao waliona mashaka.

18 Yesu akawakaribia akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu: mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.

Read full chapter