20 Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, wakuu wa makuhani, walimu wa sheria na wazee walifika Hekaluni wakamwuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?”

Akawajibu, “Na mimi nitawauliza swali. Je, mamlaka ya Yohana ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa wanadamu? ” Wakaanza kubishana wao kwa wao wakisema, “Tukisema, ‘Kwa Mungu’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ Na tukisema ‘Kwa wana damu,’ watu wote watatupiga mawe kwa sababu wanaamini kabisa kwamba Yohana alikuwa nabii.” Basi wakajibu, “Hatujui mamlaka yake yalitoka wapi.” Yesu akawaambia, “Na mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.’ ’

Mfano Wa Shamba La Mizabibu Na Wakulima

Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda mizabibu katika shamba lake, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu. 10 Wakati wa mavuno akamtuma mtumishi kwa hao wakulima aliowakodisha shamba ili wampatie sehemu ya mavuno. Lakini wale wakulima wakampiga na kumfukuza mikono mitupu. 11 Akamtuma mtumishi mwingine; naye pia wakam piga, wakamfanyia mambo ya aibu na kumfukuza. 12 Akampeleka wa tatu; wakamjeruhi na kumtupa nje ya shamba.

13 “Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu nimpendaye, bila shaka yeye watamhesh imu.’ 14 Lakini wale wakulima walipomwona, wakashauriana, ‘Huyu ndiye mrithi, hebu tumwue ili sisi turithi hili shamba.’ 15 Kwa hiyo wakamtoa nje ya shamba, wakamwua.” Ndipo Yesu akauliza, “Sasa yule mwenye shamba atawafanyia nini wakulima hawa?

16 Atakuja awaue awapatie watu wengine shamba hilo.” Watu waliposikia hayo wakasema, “Jambo hili lisi tokee!”

17 Lakini Yesu akawakazia macho akasema, “Basi ni nini maana ya maandiko haya, ‘Lile jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe la msingi.’

18 “Kila aangukaye kwenye jiwe hilo atakatika vipande vipande, na ye yote ambaye litamwangukia atasagika sagika.”

19 Waalimu wa sheria na wakuu wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja kwa sababu walifahamu kwamba huo mfano aliou toa uliwahusu wao. Lakini waliwaogopa watu.

Kuhusu Kulipa Kodi

20 Kwa hiyo wakawa wanamvizia. Wakawatuma wapelelezi wal iojifanya kuwa wana nia njema ya kujifunza. Walitumaini kumtega kwa maswali ili wamkamate kwa lo lote atakalosema, walitumie kumshtaki kwa Gavana. 21 Wale wapelelezi wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba maneno yako na mafundisho yako ni ya haki, kwamba huna upendeleo, na kwamba unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. 22 Je, sheria ya Musa inaturuhusu au haituruhusu kulipa kodi kwa

Kaisari?”

23 Lakini Yesu akatambua kwamba wanamtega, kwa hiyo akawaam bia, 24 “Nionyesheni sarafu ya fedha. Je, picha hii na maand ishi haya ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” 25 Aka waambia, “Basi, mpeni Kaisari vilivyo vyake na mpeni Mungu vil ivyo vyake.” 26 Wakashindwa kumkamata kwa maneno aliyosema mbele ya watu. Jibu lake liliwashangaza mno, wakakosa la kusema. Yesu Afundisha Kuhusu Ufufuo

27 Baadhi ya Masadukayo , wale wanaosema kwamba hakuna ufu fuo wa wafu, wakamjia Yesu wakamwuliza, 28 “Mwalimu, katika sheria ya Musa , tunasoma kwamba kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi kaka yake amwoe huyo mjane ili amzalie marehemu watoto. 29 Walikuwepo ndugu saba. Wa kwanza akafa bila kuzaa mtoto. 30 Kaka wa pili akamwoa huyo mjane 31 na wa tatu pia. Ikawa hivyo mpaka ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mama na wote wakafa pasipo kupata mtoto. 32 Mwishowe mama huyo naye akafa. 33 Je, siku ya ufufuo, mwanamke huyo ambaye aliolewa na wote saba atahesabiwa kuwa ni mke wa nani?”

34 Yesu akawajibu , “Katika maisha haya watu huoa na kuol ewa, 35 lakini wale ambao Mungu atawaona wanastahili kufufuka kutoka kwa wafu, watakapofika mbinguni hawataoa au kuolewa. 36 Hawa hawawezi kufa tena kwa sababu wao ni kama malaika; wao ni wana wa Mungu kwa kuwa wamefufuka kutoka kwa wafu. 37 Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka. Alimwita Bwana, ‘Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo,’ wakati Mungu aliposema naye katika kile kichaka kilichokuwa kikiwaka bila kuungua. 38 Yeye ni Mungu wa watu walio hai na si Mungu wa wafu kwa sababu kwa Mungu watu wote ni hai.” 39 Baadhi ya walimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umesema sawa kabisa!” 40 Na hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.

Uhusiano Kati Ya Kristo Na Daudi

41 Kisha akawaambia, “Inakuwaje watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 42 Maana Daudi mwenyewe katika kitabu cha Zaburi anasema, ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: kaa kulia kwangu 43 mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’

44 Sasa ikiwa Daudi anamwita Kristo ‘Bwana

Yesu Aonya Kuhusu Walimu Wa Sheria

45 Watu wote walipokuwa wakimsikiliza, Yesu akawaambia wana funzi wake, 46 “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa kanzu ndefu na kuamkiwa kwa heshima maso koni. Wao huchagua viti vya mbele katika masinagogi na kukaa kwe nye sehemu za wageni rasmi katika sherehe. 47 Wanawadhulumu wajane mali zao na kisha wanasali sala ndefu ili waonekane wao ni watu wema. Mungu atawaadhibu vikali zaidi kwa ajili ya haya.” Sadaka Ya Mjane

Viongozi Wawa na Mashaka Kuhusu Mamlaka ya Yesu

(Mt 21:23-27; Mk 11:27-33)

20 Siku moja Yesu alikuwa anawafundisha watu katika eneo la Hekalu. Alikuwa anawahubiri Habari njema. Viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na viongozi wazee wa Kiyahudi walikwenda kuzungumza na Yesu. Wakamwambia, “Tuambie, una mamlaka gani kutenda mambo haya! Ni nani aliyekupa mamlaka hii?”

Yesu akawajibu, “Nami nitawauliza swali pia. Niambieni: Yohana alipobatiza watu, mamlaka yake ilitoka kwa Mungu au kwa watu fulani?”

Makuhani, walimu wa sheria na viongozi wa Kiyahudi wakajadiliana kwa pamoja kuhusu hili. Wakasema, “Kama tukijibu ‘Ubatizo wa Yohana ulitoka kwa Mungu,’ atasema, ‘Sasa kwa nini hamkumwamini Yohana?’ Lakini kama tukisema ulitoka kwa watu fulani, watu hawa watatupiga kwa mawe mpaka tufe. Kwa sababu wote wanaamini Yohana alikuwa nabii.” Hivyo wakajibu, “Hatujui.”

Ndipo Yesu akawaambia, “Hata mimi sitawaambia ni nani alinipa mamlaka kufanya mambo haya.”

Yesu Atoa Simulizi Kuhusu Shamba la Mzabibu

(Mt 21:33-46; Mk 12:1-12)

Yesu akawaambia watu kisa hiki; “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Kisha akalikodisha kwa wakulima, kisha akasafiri kwa muda mrefu. 10 Wakati wa kuvuna zabibu ulipofika, alimtuma mmoja wa watumishi wake kwa wakulima wale ili wampe sehemu yake ya zabibu. Lakini wakulima wale walimpiga yule mtumishi na wakamfukuza bila kumpa kitu. 11 Hivyo mtu yule akamtuma mtumishi mwingine. Wakulima walimpiga mtumishi huyu pia, wakamwaibisha na kumfukuza bila kumpa kitu. 12 Hivyo mtu yule akamtuma mtumishi wa tatu. Wakulima wakampiga sana mtumishi huyu na wakamtupa nje ya shamba la mizabibu.

13 Mmiliki wa shamba la mizabibu akasema, ‘Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa. Yumkini watamheshimu.’ 14 Lakini wakulima walipomwona mwana wa mwenye shamba, wakajadiliana wakisema, ‘Huyu ni mwana wa mmiliki wa shamba. Shamba hili la mizabibu litakuwa lake. Tukimwua, litakuwa letu.’ 15 Hivyo wakulima wakamtupa mwana wa mmiliki wa shamba nje ya shamba la mizabibu na wakamwua.

Je, mmiliki wa shamba la mizabibu atafanya nini? 16 Atakuja na atawaua wale wakulima, kisha atalikodisha shamba kwa wakulima wengine.”

Watu waliposikia mfano huu, wakasema, “Hili lisije kutokea!” 17 Lakini Yesu akawakazia macho na akasema, “Hivyo basi, Maandiko haya yanamaanisha nini:

‘Jiwe lililokataliwa na wajenzi,
    limekuwa jiwe kuu la pembeni?’[a]

18 Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika na ikiwa jiwe hilo litaangukia, litakusaga!”

19 Walimu wa sheria na wakuu wa makuhani waliposikia kisa hiki, walijua unawahusu wao. Hivyo walitaka kumkamata Yesu wakati huo huo, lakini waliogopa watu wangewadhuru.

Yesu Ajibu Swali Lenye Mtego

(Mt 22:15-22; Mk 12:13-17)

20 Hivyo viongozi wa Kiyahudi walitafuta namna ya kumtega Yesu. Walituma watu waliojifanya kuwa wenye haki, ili waweze kumnasa ikiwa angesema jambo ambalo wangeweza kutumia kinyume naye. Ikiwa angesema jambo lolote baya, wangemkamata na kumpeleka kwa gavana wa Kirumi, mwenye mamlaka ya kumhukumu na kumwadhibu. 21 Hivyo wale watu wakamwambia Yesu, “Mwalimu, tunafahamu kwamba yale unayosema na kufundisha ni kweli. Haijalishi ni nani anasikiliza, unafundisha sawa kwa watu wote. Daima unafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. 22 Tuambie, ni sahihi sisi kulipa kodi kwa Kaisari, au si sahihi?”

23 Lakini Yesu alitambua watu hawa walikuwa wanajaribu kumtega. Akawaambia, 24 “Nionesheni sarafu ya fedha,” Kisha akauliza, “Jina na picha katika sarafu hii ni ya nani?”

Wakamjibu, “Ya Kaisari.”

25 Akawaambia, “Basi mpeni Kaisari vilivyo vya Kaisari, na mpeni Mungu vilivyo vya Mungu.”

26 Watu wale wakashangaa jibu lake la hekima. Hawakusema kitu. Hawakuweza kumtega Yesu pale mbele za watu. Hakusema chochote kibaya ambacho wangekitumia ili kumnasa.

Baadhi ya Masadukayo Wajaribu Kumtega Yesu

(Mt 22:23-33; Mk 12:18-27)

27 Baadhi ya Masadukayo walimwendea Yesu. (Masadukayo wanaamini watu hawatafufuka kutoka kwa wafu.) Wakamwuliza, 28 “Mwalimu, Musa aliandika kwamba mtu aliyeoa akifa na hakuwa na watoto, kaka au mdogo wake amwoe mjane wake, ili wawe na watoto kwa ajili ya yule aliyekufa.[b] 29 Walikuwepo ndugu saba. Wa kwanza alioa mke lakini akafa bila ya kuwa na watoto. 30 Wa pili akamuoa yule mwanamke kisha akafa. 31 Na wa tatu akamwoa mwanamke na akafa. Kitu kile kile kikawatokea ndugu wote saba. Walikufa bila ya kuwa na watoto. 32 Mwanamke akawa wa mwisho kufa. 33 Lakini ndugu wote saba walimwoa. Sasa, watu watakapofufuka kutoka kwa wafu, atakuwa mke wa yupi?”

34 Yesu akawaambia Masadukayo, “Watu huoana katika ulimwengu huu. 35 Baadhi ya watu watastahili kufufuliwa kutoka kwa wafu na kuishi tena katika ulimwengu ujao. Katika maisha yale hawataoa kamwe. 36 Katika maisha hayo, watu watakuwa kama malaika na hawatakufa. Ni watoto wa Mungu, kwa sababu wamefufuliwa kutoka kwa wafu. 37 Musa alionesha dhahiri kwamba watu hufufuliwa kutoka kwa wafu. Alipoandika kuhusu kichaka kilichokuwa kinaungua,[c] alisema kwamba Bwana ni ‘Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.’(A) 38 Ni Mungu wa wanaoishi tu. Hivyo watu hawa kwa hakika hawakuwa wamekufa. Ndiyo, kwa Mungu watu wote bado wako hai.”

39 Baadhi ya walimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, jibu lako ni zuri.” 40 Hakuna hata mmoja aliyekuwa na ujasiri wa kumwuliza swali jingine.

Je, Masihi ni Mwana wa Daudi?

(Mt 22:41-46; Mk 12:35-37)

41 Kisha Yesu akasema, “Kwa nini watu husema kwamba Masihi ni Mwana wa Daudi? 42 Katika kitabu cha Zaburi, Daudi mwenyewe anasema,

‘Bwana Mungu alimwambia Bwana wangu:
Keti karibu nami upande wangu wa kulia,
43     na nitawaweka adui zako chini ya mamlaka yako.’[d](B)

44 Hivyo ikiwa Daudi anamwita Masihi, ‘Bwana’. Inawezekanaje Masihi awe mwana wa Daudi?”

Tahadhali Juu ya Walimu wa Sheria

(Mt 23:1-36; Mk 12:38-40; Lk 11:37-54)

45 Watu wote walipokuwa wanamsikiliza Yesu, akawaambia wafuasi wake, 46 “Iweni waangalifu dhidi ya walimu wa sheria. Wanapenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi yanayoonekana ya heshima. Na wanapenda pale watu wanapowasalimu kwa heshima maeneo ya masoko. Wanapenda kukaa sehemu za heshima katika masinagogi na sehemu za watu maarufu katika sherehe. 47 Lakini huwalaghai wajane na kuchukua nyumba zao. Kisha kujionesha kuwa waongofu wa mioyo kuomba sala ndefu. Mungu atawaadhibu kwa hukumu kuu.”

Footnotes

  1. 20:17 Zab 118:22. Yesu, ambaye ndiye “Jiwe” katika Zaburi hii, anajitambulisha mwenyewe kama mwana katika simulizi hii ambapo anauawa na wakulima wale. Tazama Mdo 4:11.
  2. 20:28 kwa ajili ya yule aliyekufa Tazama Kum 25:5-6.
  3. 20:37 kichaka kilichokuwa kinaungua Tazama Kut 3:1-12.
  4. 20:43 chini ya mamlaka yako Kwa maana ya kawaida, “mpaka nitakapowafanya maadui zako kuwa kiti cha kuweka miguu yako”.