Mfano Wa Karamu Ya Harusi

22 Yesu akazungumza nao tena kwa kutumia mifano, akasema, “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja ali yemwandalia mwanae karamu ya harusi. Akawatuma watumishi wake wakawaite wageni walioalikwa lakini wakakataa kuja. Akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni waalikwa kwamba karamu iko tayari, nimekwisha chinja fahali wangu na ng’ombe wanono kwa ajili yenu, karibuni karamuni.’ Lakini waalikwa wakadharau, mmoja akaenda shambani kwake, mwingine akaenda kwenye miradi yake, na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatendea mambo ya aibu na kuwaua.

“Yule mfalme akakasirika, akapeleka jeshi lake likawaanga miza wale wauaji na kuteketeza mji wao. Kisha akawaambia watum ishi wake, ‘Karamu ya harusi ni tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja karamuni. Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkawaalike harusini wote mtakaowakuta.’ 10 Wale watumishi wakaenda mabarabarani wakawakusanya wote waliowakuta, wema na wabaya. Ukumbi wa sherehe ya harusi ukajaa wageni.

11 “Lakini mfalme alipoingia kutazama wageni, alimwona mle ndani mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la harusi. 12 Mfalme akamwuliza, ‘Rafiki, umeingiaje humu bila vazi la harusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema. 13 Basi mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’ 14 Kwa maana walioitwa ni wengi lakini walioteuliwa ni wachache.”

Kuhusu Kulipa Kodi

15 Mafarisayo walifanya mbinu za kumtega Yesu katika mafundi sho yake. 16 Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode wakam wambie, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu wa haki na unafundisha njia za Mungu kwa uaminifu bila kumjali mtu, kwa maana cheo si kitu kwako. 17 Basi tuambie, wewe unaonaje? Ni halali, au si halali kulipa kodi kwa Kaisari?”

18 Yesu alifahamu hila yao kwa hiyo akawaambia, “Ninyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19 Nionyesheni sarafu mnayolipia kodi.” Wakamletea sarafu. 20 Yesu akawauliza, “Picha hii na sahihi hii ni za nani?” 21 Wakamjibu, “Ni za Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kais ari; na ya Mungu mpeni Mungu.”

22 Waliposikia haya wakashangaa; wakamwacha, wakaondoka.

Ufufuo Wa Wafu

23 Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wanaoamini kwamba wafu hawafufuki, walikuja kwa Yesu wakamwuliza, 24 “Mwalimu, Musa alitufundisha kwamba mtu akifariki pasipo kupata watoto, ndugu yake amwoe huyo mjane ili ampatie kaka yake watoto. 25 Hapa kwetu walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, kisha akafariki na kwa kuwa hakuwa na watoto, yule mjane alichukuliwa na ndugu yake. 26 Ikatokea hivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili hadi wote saba wakamwoa huyo mjane bila kupata watoto. 27 Baadaye, yule mjane naye akafariki. 28 Sasa tuambie, siku ile ya ufufuo, ata hesabiwa kuwa ni mke wa nani? Maana aliolewa na wote saba!”

29 Yesu akawajibu, “Mnakosea kwa sababu hamjui Maandiko wala uwezo wa Mungu. 30 Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa; kwa maana watakuwa kama malaika wa mbinguni. 31 Na kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma Mungu alivyowaambia kwamba, 32 ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.”

33 Ule umati wa watu waliposikia hayo, walishangazwa sana na mafund isho yake.

Amri Kuu Kuliko Zote

34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazi sha Masadukayo, walikutana wakamjia pamoja. 35 Mmoja wao, mtaalamu wa sheria akajaribu kumtega kwa kumwuliza, 36 “Mwali mu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote?”

37 Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38 Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40 Amri hizi mbili ndio msingi wa sheria zote na Maandiko ya manabii.”

Kristo Ni Mwana Na Bwana Wa Daudi

41 Mafarisayo walipokuwa pamoja Yesu aliwauliza, 42 “Mnaonaje kuhusu Kristo? Yeye ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.”

43 Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi anapozungumza kwa Roho anamwita Kristo ‘Bwana,’ kwa kusema, 44 ‘Bwana alimwam bia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.’ 45 Kama Daudi anamwita ‘Bwana 46 Hakuna aliyeweza kumjibu Yesu hata neno moja. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kum wuliza maswali.

Simulizi Kuhusu Watu Walioalikwa Kwenye Sherehe

(Lk 14:15-24)

22 Yesu aliendelea kuwajibu viongozi wa Kiyahudi kwa mifano zaidi. Akasema, “Ufalme wa Mungu unafanana na jambo lililotokea mfalme alipoandaa sherehe ya harusi kwa ajili ya mwanaye. Aliwaalika baadhi ya watu. Wakati ulipofika mfalme aliwatuma watumwa wake kuwaambia watu waende kwenye sherehe. Lakini walikataa kwenda kwenye sherehe ya mfalme.

Ndipo mfalme aliwaita baadhi ya watumishi wengine zaidi na akawaambia namna ya kuwaambia wale aliowaalika: ‘Njooni sasa! Sherehe imeandaliwa. Nimechinja ng'ombe wangu madume na ndama wanono waliolishwa nafaka, na kila kitu kiko tayari kuliwa. Njooni kwenye sherehe ya harusi.’

Lakini watu walioalikwa hawakujali yale waliyoambiwa na watumwa wa mfalme. Wengine waliondoka wakaenda kufanya mambo mengine. Mmoja alikwenda shambani na mwingine alikwenda kwenye shughuli zake. Wengine waliwakamata watumwa wa mfalme, wakawapiga na kuwaua. Mfalme alikasirika sana na akatuma jeshi lake kuwaua wale waliowaua watumwa wake. Na jeshi likauchoma moto mji wao.

Kisha mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Sherehe ya harusi iko tayari. Niliwaalika wale watu lakini hawakustahili. Hivyo nendeni kwenye pembe za mitaa na mwalikeni kila mtu mtakayemwona, waambieni waje kwenye sherehe yangu.’ 10 Hivyo watumwa wake waliingia mitaani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wabaya na wema na kuwaleta kwenye sherehe. Na jumba la sherehe likawa na wageni wengi.

11 Mfalme alipoingia ili kuwasalimu wageni, alimwona mtu ambaye hakuwa amevaa vazi rasmi la harusi. 12 Mfalme akamwuliza, ‘Rafiki ilikuwaje ukaruhusiwa kuingia humo? Hujavaa vazi nadhifu kwa arusi!’ Lakini mtu yule hakuwa na neno la kusema. 13 Hivyo mfalme akawaambia baadhi ya wale waliokuwa wanawahudumia watu kwa chakula, ‘Mfungeni mtu huyu mikono na miguu yake na mtupeni gizani, ambako watu wanalia na kusaga meno yao kwa maumivu.’

14 Ndiyo, watu wengi wamealikwa, lakini wachache tu ndiyo waliochaguliwa.”

Yesu Ajibu Swali Lenye Mtego

(Mk 12:13-17; Lk 20:20-26)

15 Kisha Mafarisayo wakaondoka mahali ambapo Yesu alikuwa anafundisha. Wakapanga mpango wa kumfanya aseme kitu ambacho wangekitumia dhidi yake. 16 Wakawatuma kwake baadhi ya wafuasi wao na baadhi ya watu kutoka katika kundi la Maherode. Watu hawa walipofika kwa Yesu wakasema, “Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mtu mwema na kwamba daima unafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu, bila kujali ni nani anakusikiliza. Huna wasiwasi namna ambavyo wengine wanaweza wakasema. 17 Sasa tuambie, unadhani ni sahihi kulipa kodi kwa Kaisari au la?”

18 Lakini Yesu alijua kuwa watu hawa walikuwa wanamtega. Hivyo akasema, “Enyi wanafiki! Kwa nini mnajaribu kunitega ili niseme jambo lililo kinyume? 19 Nionesheni sarafu inayotumika kulipa kodi.” Wakamwonesha Yesu sarafu iliyotengenezwa kwa fedha. 20 Kisha Yesu akauliza, “Picha iliyo kwenye sarafu hii ni ya nani? Na jina lililo kwenye sarafu hii ni la nani?”

21 Wakajibu, “Ni picha ya Kaisari na ni jina la Kaisari.”

Ndipo Yesu akawajibu, “Mpeni Kaisari vilivyo vyake na mpeni Mungu vilivyo vyake.”

22 Waliposikia yale Yesu aliyosema, wakashangaa na kuondoka.

Baadhi ya Masadukayo Wajaribu Kumtega Yesu

(Mk 12:18-27; Lk 20:27-40)

23 Siku hiyo hiyo baadhi ya Masadukayo walimjia Yesu. (Masadukayo hawaamini kuwepo kwa ufufuo wa wafu.) Masadukayo walimwuliza Yesu swali. 24 Wakasema, “Mwalimu, Musa alituambia kuwa ikiwa mwanaume aliyeoa atakufa na hana watoto, ndugu yake lazima amwoe mkewe ili aweze kuzaa watoto kwa ajili ya nduguye aliyekufa.[a] 25 Walikuwepo ndugu saba miongoni mwetu. Ndugu wa kwanza alioa lakini akafa bila ya kupata watoto. Hivyo ndugu yake akamwoa mkewe. 26 Na ndugu wa pili akafa pia, jambo hili hilo likatokea kwa ndugu wa tatu na ndugu wengine wote. 27 Mwanamke akawa wa mwisho kufa. 28 Lakini wanaume wote saba walikuwa wamemwoa. Sasa watu watakapofufuliwa kutoka kwa wafu, mwanamke huyu atakuwa mke wa yupi?”

29 Yesu akajibu, “Mnakosea sana! Hamjui kile ambacho Maandiko yanasema. Na hamjui lolote kuhusu nguvu ya Mungu. 30 Watu watakapofufuliwa kutoka kwa wafu, wanaume hawataoa wake na wanawake hawataozwa kwa wanaume. Kila mtu atakuwa kama malaika walio mbinguni. 31 Someni kile ambacho Mungu alikisema kuhusu watu kufufuliwa kutoka kwa wafu. 32 Mungu alisema, ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.’(A) Ni Mungu wa walio hai tu, hivyo hakika watu hawa hawakuwa wafu.”

33 Watu waliposikia hili, waliyashangaa mafundisho ya Yesu.

Amri ipi ni ya Muhimu Zaidi?

(Mk 12:28-34; Lk 10:25-28)

34 Mafarisayo waliposikia kuwa Yesu amewafanya Masadukayo waonekane wajinga nao wakaacha kumwuliza maswali. Kwa hiyo Mafarisayo wakafanya mkutano. 35 Ndipo mmoja wao, aliye mtaalamu wa Sheria ya Musa, akamwuliza Yesu swali ili kumjaribu. 36 Akasema, “Mwalimu, amri ipi katika sheria ni ya muhimu zaidi?”

37 Yesu akajibu, “‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na akili yako yote.’(B) 38 Hii ndiyo amri ya kwanza na ya muhimu zaidi. 39 Na amri ya pili ni kama ya kwanza: ‘Mpende jirani yako[b] kama unavyojipenda wewe mwenyewe.’(C) 40 Sheria yote na maandiko ya manabii yamejengwa katika amri hizi mbili.”

Je, Masihi ni Mwana wa Daudi?

(Mk 12:35-37; Lk 20:41-44)

41 Hivyo Mafarisayo walipokuwa pamoja, Yesu aliwauliza swali. 42 Akasema, “Nini mawazo yenu juu ya Masihi? Je, ni mwana wa nani?” Mafarisayo wakajibu, “Masihi ni Mwana wa Daudi.”

43 Yesu akawaambia, “Sasa ni kwa nini Daudi anamwita ‘Bwana’? Daudi alikuwa anazungumza kwa nguvu ya Roho. Aliposema,

44 ‘Bwana Mungu alimwambia Bwana Mfalme wangu:
Keti karibu nami upande wangu wa kuume,
    na nitawaweka adui zako chini ya udhibiti wako.’[c](D)

45 Ikiwa Daudi anamwita Masihi ‘Bwana’. Inakuwaje Masihi ni mwana wa Daudi?”

46 Hakuna Farisayo aliyeweza kumjibu Yesu. Na baada ya siku hiyo, hakuna aliyekuwa jasiri kumwuliza maswali zaidi.

Footnotes

  1. 22:24 nduguye aliyekufa Tazama Kum 25:5,6.
  2. 22:39 jirani yako Mafundisho ya Yesu katika Lk 10:25-37 yanaonesha kwa uwazi kuwa hii ni pamoja na yeyote mwenye uhitaji.
  3. 22:44 chini ya udhibiti wako Kwa maana ya kawaida, “kuweka chini ya miguu”.