Add parallel Print Page Options

Karamu ya Pasaka

(Mt 26:17-25; Mk 14:12-21; Yh 13:21-30)

Siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu[a] ilifika. Hii ni siku ambayo Wayahudi daima walichinja kondoo kwa ajili ya Pasaka. Yesu aliwaambia Petro na Yohana, “Nendeni mkaandae mlo wa Pasaka ili tule.”

Wakamwambia, “Unataka tukauandae wapi?”

Akawaambia, 10 “Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mtu amebeba mtungi wa maji. Mfuateni. Ataingia katika nyumba. 11 Mwambieni mmiliki wa nyumba, ‘Mwalimu anakuomba tafadhali utuoneshe chumba ambacho yeye na wafuasi wake wanaweza kulia mlo wa Pasaka.’ 12 Mmiliki atawaonesha chumba kikubwa ghorofani kilicho tayari kwa ajili yetu. Andaeni mlo humo.”

13 Hivyo Petro na Yohana wakaondoka. Kila kitu kilitokea kama Yesu alivyosema. Na hivyo wakauandaa mlo wa Pasaka.

Chakula cha Bwana

(Mt 26:26-30; Mk 14:22-26; 1 Kor 11:23-25)

14 Wakati ulifika kwa wao kula mlo wa Pasaka. Yesu na mitume walikuwa wamekaa pamoja kuzunguka meza ya chakula.

Read full chapter

Footnotes

  1. 22:7 Siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu Pasaka.